Dunia inao wachache mno wenye haki, na watenda maovu hujivuna kwa uovu wao, huutetea uovu wao, wako tayati kumwaga damu nyingine kutetea ujangili wao
Na siku zote mtu muoga wa kusemwa kwa sababu anasimamia ukweli, hawezi kuwatetea watu hadharani, mtu huyo huchagua njia ya kuabudu uovu na hayuko tayari kuitetea haki maana haki haipendwi na wengi, Haki ni adui mkubwa sana ya watu wengi waovu
Na ndiyo maana leo, tunaviongozi wengi wanaabudu uovu wa matendeo ya watishao kwa uovu wao, hawana kauli yoyote mbele ya watishao kwa maovu
Kuna kiongozi mmoja alidiriki kusema, ukiwagusa mafisadi, unaua nchi, hiyo ni ibada kamili ya mtu muovu dhidi ya waovu wenzake
Siku zote dhambi kuu, hubebwa na mabwanyeye yaliyoshimdikana, yana ukwasi na yanatisha, hayo haywezi kukemewa hata kwenye nyumba za Ibada, lakini ni kwa faida ya Nani?
Ni kwa faida ya njaa tu za viongozi, wakati wao wakiamini wanamtumikia huyo, naye huyo hawaju hao,
Ushetani kuugeuza ili uwe wema, ni gharama kubwa mno, ni nani awezaye kuvumilia matusi ya waovu?
Duniani, tunaishi kwa muda mufupi mno ukilinganisha na tulikotokea kabla ya kuweko Duniani na baada ya kutoka tena Duniani
Chukia uovu kwa nguvu zote ili uwe mingoni mwa wale wanao na matumiani ya amani kutumika bila dhuluma huku wakijua, kufanya hivyo, ni kuwa upande wa wale wachache mno walio na tunda la Mungu ndani yao
Makonda, endele hivyo hivyo, hata kama heshima yako itakuwa ziro kabisa duniani, ila kwa kuwa unajipambanua kwa kuchukia dhuluma, Mungu anathawabu yako