Makondakta ni wahasibu wana haki ya kulipa Kodi na Tozo hapa Tanzania

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
1,446
Reaction score
1,645
Habari Tanzania !

Ujambo; NBAA, TRA na Wizara ya Fedha !.

Makondakta wa magari ni Maafisa Hesabu wanaofanya miamala ya fedha kwenye Daladala na Mabasi ndani na nje ya Mikoa; na nje ya Nchi ni wadau wenu nyinyi hasa NBAA, TRA na Wizara ya Fedha.

1. Naomba ikiwapendeza muwaunde kwenye "Database Sheet" ya Makondakta wote nchi nzima. Lengo hapa ni wawe walipa kodi wazuri tofauti na ilivyo sasa na pia wawe wanachama rasmi wa Bodi ya Uhasibu Tanzania (NBAA).

2. Napendekeza wapewe elimu fupi ya Uhasibu kwa malipo (Ukondakta Tozo) walau Tsh.20,000/= kwa Mwaka kwaajili ya kupewa mafunzo pamoja na kupata huduma za Uhasibu toka NBAA, Wizara ya Fedha na TRA.

3. Wapate Ajira za mikataba toka Sekta ya Usafirishaji kwani wao ni watu muhimu na wenye chachu kwenye mnyororo wa uchumi kwa wamiliki wa usafiri na nchi kwa ujumla.

4. Wasaidiwe kuunda Umoja wa Makondakta nchini ili wawe rasmi; yaani Sekta rasmi.

5. Iwe ni sharti kuu; hakuna Kondakta atakayefanya kazi ya Ukonda pasipo kuwa kwenye "Ukondakta Database" na pia lazima apate mafunzo ya Uhasibu. Hapa tutakuwa tumeongeza umakini kwenye Sekta hii.

Karibuni.
 
Mwenye kikubwa ataongezewa, mwenye kidogo atanyang'anywa hata hicho kidogo alichonacho! Bongo nyoso.
 
Haaaaahaaaaa
Wamiliki wengi wa Vyombo vya Usafirisaji Umma ni wanasiasa - wafanyabiashara; imani ni kuwa wakiipenda Tanzania hakuna linaloshindikana.
 
Habari Tanzania !

Ujambo; NBAA, TRA na Wizara ya Fedha !.

Makondakta wa magari ni Maafisa Hesabu wanaofanya miamala ya fedha kwenye Daladala na Mabasi ndani na nje ya Mikoa; na nje ya Nchi ni wadau wenu nyinyi hasa NBAA, TRA na Wizara ya Fedha.

1. Naomba ikiwapendeza muwaunde kwenye "Database Sheet" ya Makondakta wote nchi nzima. Lengo hapa ni wawe walipa kodi wazuri tofauti na ilivyo sasa na pia wawe wanachama rasmi wa Bodi ya Uhasibu Tanzania (NBAA).

2. Napendekeza wapewe elimu fupi ya Uhasibu kwa malipo (Ukondakta Tozo) walau Tsh.20,000/= kwa Mwaka kwaajili ya kupewa mafunzo pamoja na kupata huduma za Uhasibu toka NBAA, Wizara ya Fedha na TRA.

3. Wapate Ajira za mikataba toka Sekta ya Usafirishaji kwani wao ni watu muhimu na wenye chachu kwenye mnyororo wa uchumi kwa wamiliki wa usafiri na nchi kwa ujumla.

4. Wasaidiwe kuunda Umoja wa Makondakta nchini ili wawe rasmi; yaani Sekta rasmi.

5. Iwe ni sharti kuu; hakuna Kondakta atakayefanya kazi ya Ukonda pasipo kuwa kwenye "Ukondakta Database" na pia lazima apate mafunzo ya Uhasibu. Hapa tutakuwa tumeongeza umakini kwenye Sekta hii.

Karibuni.
Kufanya miamala hakuwafanyi kuwa wahasibu
 
Nimeamini wewe ni "Tax Collector" kwelikweli....🤣🤣🤣
Kiongozi kila mtu anapaswa hii nchi aitolee jasho kwa njia yoyote. Unajua Madereva wao tunawalima Leseni ya Udereva tunawatoza. Sasa hawa Makondakta wanalipa wapi wao?
 
Na kwa kweli hawalipi popote....

Hoja Yako inamashiko sana Mkurugenzi...
 
Wizara ya Fedha na TRA wasihangaike sana; Wadau wao wapo tu. Ni jambo la elimu ya Mlipa kodi iwafikie na wajivunie nchi yao kwa kweli.
 
Back
Top Bottom