KERO Makonde-Dar: Baada ya Greda kupita kabla ya Uchaguzi wa Mitaa, sasa kifusi laini cha tope kimemwagwa, tunachezewa au?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Barabara ya Makonde inayoelekea Kanisa Katoliki Mbezi Juu imekuwa kero ya muda mrefu kwa watumiaji wake, hususan wa vyombo vya moto, kutokana na mashimo mengi na miundombinu duni. Hivi karibuni, kumemwagwa kifusi laini cha udongo mtupu ambacho, endapo mvua zikinyesha, kitazidisha hali mbaya badala ya kuleta unafuu.

Hali hii inazua maswali kuhusu iwapo kuna mkandarasi ambaye amelipwa fedha bila kutekeleza kazi kwa viwango vinavyokubalika. Ikiwa hilo ni kweli, basi ni wazi kuwa kuna dalili za ubadhirifu wa fedha za umma.
photo_2025-07-06_16-34-56.jpg

photo_2025-07-06_16-34-54.jpg

photo_2025-07-06_16-34-49.jpg
Ni muhimu kukumbuka kuwa siku chache kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, barabara hiyo ilikwanguliwa kwa kutumia greda, lakini haikuwekewa kifusi chochote. Ndani ya miezi miwili, mashimo yalirejea kama awali.

Sasa, tunaona juhudi zisizo na tija zikirejewa bila mpango wa kudumu. Jambo hili linanifanya niwaze kama barabara hii imekuwa mtaji wa kisiasa, inayotumiwa kuwadanganya wananchi kila uchaguzi unapokaribia. Bado nawaza, lakini sipati majibu.

Napendekeza Mamlaka husika, hususan TARURA Mkoa wa Dar es Salaam, kuitengea bajeti maalum kwa ajili ya ujenzi wa kudumu wa barabara hii, kwa kuzingatia umuhimu wake kwa wananchi wanaoitumia kila siku. Eneo hili pia lipo katika mwelekeo rafiki kwa utekelezaji wa miradi ya miundombinu bila kusababisha bughudha kwa jamii inayolizunguka.

Ni wakati sasa wa kuzingatia maslahi ya wananchi na kuachana na hatua za muda mfupi zisizotoa suluhisho endelevu lenye tija kwa umma.
 
Tuambie, wewe ni mwenyeji hapo?
Au ni mpiga tontolilo tu?
 
Mtoa mada, unashauriwa utoe mrejesho.
Je unaishi hapo?
Kwa taarifa yako kazi hiyo hakuna TARURA WALA TANROADS.
Wananchi wamejitolea hivyo vifusi baada ya kukosa msaada toka serikalini.
Nawe unstakiwa kuchangia hizo juhudi badala ya kupiga domo.
Sasa, nenda leo na uone kazi iliyofanyika

Umasikini wa mawazo na kukosa dhamira ya kujisaidia mwenyewe inakusumbua sana mtoa mada.
 
Barabara ya Makonde inayoelekea Kanisa Katoliki Mbezi Juu imekuwa kero ya muda mrefu kwa watumiaji wake, hususan wa vyombo vya moto, kutokana na mashimo mengi na miundombinu duni. Hivi karibuni, kumemwagwa kifusi laini cha udongo mtupu ambacho, endapo mvua zikinyesha, kitazidisha hali mbaya badala ya kuleta unafuu.

Hali hii inazua maswali kuhusu iwapo kuna mkandarasi ambaye amelipwa fedha bila kutekeleza kazi kwa viwango vinavyokubalika. Ikiwa hilo ni kweli, basi ni wazi kuwa kuna dalili za ubadhirifu wa fedha za umma.
Ni muhimu kukumbuka kuwa siku chache kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, barabara hiyo ilikwanguliwa kwa kutumia greda, lakini haikuwekewa kifusi chochote. Ndani ya miezi miwili, mashimo yalirejea kama awali.

Sasa, tunaona juhudi zisizo na tija zikirejewa bila mpango wa kudumu. Jambo hili linanifanya niwaze kama barabara hii imekuwa mtaji wa kisiasa, inayotumiwa kuwadanganya wananchi kila uchaguzi unapokaribia. Bado nawaza, lakini sipati majibu.

Napendekeza Mamlaka husika, hususan TARURA Mkoa wa Dar es Salaam, kuitengea bajeti maalum kwa ajili ya ujenzi wa kudumu wa barabara hii, kwa kuzingatia umuhimu wake kwa wananchi wanaoitumia kila siku. Eneo hili pia lipo katika mwelekeo rafiki kwa utekelezaji wa miradi ya miundombinu bila kusababisha bughudha kwa jamii inayolizunguka.

Ni wakati sasa wa kuzingatia maslahi ya wananchi na kuachana na hatua za muda mfupi zisizotoa suluhisho endelevu lenye tija kwa umma.
Bwana majungu kumbe hata mtaani kwako hujui kinachoendelea?
Naona kam kuna michango ambayo wewe hushiriki, kazi yako kueneza majungu tu, bila kushiriki kujikwamua.
Nyie ndo mnaolewaga!
 
Back
Top Bottom