donlucchese
JF-Expert Member
- Mar 23, 2011
- 17,128
- 21,885
- Thread starter
-
- #21
Mr Mayebe a.k.a Masta huo moto ogopa sana ni hatariii, Siku moja nikachelewa ilikuwa zamu ya asubuhi class kwetu kuna teacher nikadivert nikiogopa kuchezea, si nikazama darasa la watu ambalo lilikuwa hakuna mwalimu kumbe mule nilipoingia masta ndo alikuwa anakipindi, akazama akaanza fundisha harafu kama jana yake alikuwa amewapa home work, akaanza kagua kwa kila mmoja du bahati nzuri alipitiwa hakunitazama lakini mi moyoni ilikuwa balaa.
Ha ha ha daaah nakumbuka kipindi kile nisipojisikia kukaa class naenda zangu Nyambiz hall kupiga buku......lol Yeye alikuwa na kelele ile mbaya,Wapi Kisarika ni noma mbayaa,Mataula kitu black ile mbaya.
Makongo enzi ile bwana........
Hahah hatari mkuu bruce ni balaa, mimi nilikamatwa kwenye msala wa kupiga machata na mwenzangu Pap2 sitasahu aisee.
"Makongo ilikuwa kipindi cha Col. KIPINGU, alivyotoka tu, na baadhi wa walimu 'vichwa' wakadorora na wengine wakaondoka. Zile adhabu za kuchimba visiki barabarani asubuhi na mchana wakati jua lachoma...zilikuwa zinasaidia na kurudisha wanafunzi kwenye mstari.
MAKONGO ya Col Kipindu ilikuwa MFUMO SAHIHI wa kimasomo".
Kuna mwalimu mmoja anaitwa Mr Chuwa anatembea kama kiberenge!!!!
Wapi Mwashiga....,Mr Mayebe a.k.a Masta,wapi Nyalusi.....,Madeghe,....,Malongoli....,Mgongolwa.....,Kaimbe....,Mchwampaka.....,Kombaa mwalimu wa French!!!!!
"Makongo ilikuwa kipindi cha Col. KIPINGU, alivyotoka tu, na baadhi wa walimu 'vichwa' wakadorora na wengine wakaondoka. Zile adhabu za kuchimba visiki barabarani asubuhi na mchana wakati jua lachoma...zilikuwa zinasaidia na kurudisha wanafunzi kwenye mstari.
MAKONGO ya Col Kipindu ilikuwa MFUMO SAHIHI wa kimasomo".
Salam wakuu,
Kwa muda wa miaka mingi enzi za zamani, ukitaja katika shule ambazo zilikua zinafanya vizuri kitaaluma na kimichezo, makongo nayo ilikuepo kwenye list. Nakumbuka enzi za headmaster Col Iddi Omary Kipingu, alijitahidi kuiweka makongo katika ramani ya kimichezo na kitaaluma. Ni wanasport wengi sana ambao wamepitia shule ya sekondari ya makongo ambao waliwika au wanawika katika nyanja za michezo mbali mbali. Nakumbuka wimbo wa shule kidogo," Najivunia shule yangu makongo, sekondari ing'aayo kielimu, pia na kwa fani nyingine zote makongo sekondari oye oye". Enzi hizo ukitaka uone cha mtema kuni kutoka kwa marehemu afande miraji au babu chacha basi wewe uchelewe asembo au usiwe unaimba wakati wenzako wanaimba. Wapi wale wazee wa JORO? Hiki kilikua ni chakula cha wabishi peke yake. Kiukweli shule zamani ilikua ina perfomance nzuri tu, lakini kwa miaka ya karibuni hali imebadilika sana. Makongo sasa hivi imekua mdebwedo sana kuliko hata baadhi ya shule za kata. Imagine kama mwaka jana division one kidato cha nne ilikua moja tu..!! Nashindwa kuelewa what went wrong mpaka shule imefikia kushika mkia kiasi hiki. Anyways, kwa wale ex-makongo je nio kitu gani unakikumbuka zaidi pale makongo? Au ni adhabu gani ambayo ulishawahi kuipata ambayo kamwe hautoisahau? Nawasilisha.
Ndugu umenikumbusha mbali sana,huo wimbo wa shule aliutunga mwalimu Pongwe,mimi mwenyewe ni kati ya wazee wa joro pale nyuma kwa dada blandina,Makongo ya sasa haiwezi kuwa km ya zamani
Kumbe vijana wa Makongo tupo wengi humu?!
Mimi nilisoma O level pale, nilikuwa nikiishi pale pale shule, bweni la Timba. Namkumbuka sana Master Mayebe na magwanda yake, Malongoli na sauti lake, Yule babu wa french (I heard he's dead now, R.I.P).
Kuna mwalimu mmoja anaitwa Mr Chuwa anatembea kama kiberenge!!!!
Hahah, mkuu dada blandina alikua anakinukisha sana kuliko hata Siso muuza mihogo.
Hahaa aloo umenkumbusha mbali sana, me bana sintosahau afande blusi wa mabweni ya wavulana alinkuta room mida ya class nili dodge, alinipa adhabu ya kuruka kichurachura niuzunguke mti mara 50,
Aftr those rounds sikuweza simama kabisa misuli iligoma hadi nkakandwa na ice,
"makongo ooye elimu ni ulinzi"
2004-2007
Siso nilimkimbia muda sasa,kwa wale wa bweni mnamkumbuka master scout,jamaa alikuwa mnoko mbaya