donlucchese
JF-Expert Member
- Mar 23, 2011
- 17,128
- 21,885
- Thread starter
- #21
Mr Mayebe a.k.a Masta huo moto ogopa sana ni hatariii, Siku moja nikachelewa ilikuwa zamu ya asubuhi class kwetu kuna teacher nikadivert nikiogopa kuchezea, si nikazama darasa la watu ambalo lilikuwa hakuna mwalimu kumbe mule nilipoingia masta ndo alikuwa anakipindi, akazama akaanza fundisha harafu kama jana yake alikuwa amewapa home work, akaanza kagua kwa kila mmoja du bahati nzuri alipitiwa hakunitazama lakini mi moyoni ilikuwa balaa.
Mkuu sitasahau siku masta mayebe alikusanya majina ya wapiga kelele akatubakiza jioni. Huwezi amini kila mtu alipewa darasa moja kupiga deki mpaka akikagua yeye mwenyewe na kutoa ruhusa. Nakumbuka tuliondoka saa tatu usiku.