Makosa 13 Yanayowafanya Wateja Wasinunue Hata Wakikufuata

Makosa 13 Yanayowafanya Wateja Wasinunue Hata Wakikufuata

youngkato

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
3,811
Reaction score
3,888
kufunga mauzo (closing sales) ni hatua nyeti sana. Unaweza ukawa umewekeza muda, pesa na nguvu nyingi kutangaza, lakini kosa dogo kwenye hatua ya mwisho likakugharimu kila kitu. Hii ndiyo sababu makala hii ni muhimu kwako.
mambo ya kuzingatia ili kuuza sanaaa.png


Makosa yanayofanywa na wafanyabiashara wengi bila kujua, na namna bora ya kuyaepuka. Lengo letu ni kuhakikisha unapofikia hatua ya kumaliza mazungumzo na mteja, hauachi pesa mezani.

1. Kumlazimisha mteja kununua​

Hakuna mteja anayetaka kushinikizwa. Watu hununua kwa sababu wanataka, si kwa sababu wamesukumwa. Badala ya kumsukuma mteja, muonyeshe namna bidhaa au huduma zako zinatatua tatizo lake. Toa suluhisho, sio presha.

2. Kuwasema vibaya wapinzani wako​

Wafanyabiashara wengine huamini kuwa kwa kuisema vibaya kampuni nyingine, wanajiongezea nafasi ya kuuza. Ukweli ni kwamba hii huondoa uaminifu. Badala ya kuponda wengine, elezea kwa ufasaha faida na tofauti za bidhaa zako. Uaminifu hujengwa kwa kuonyesha thamani yako mwenyewe, sio kwa kuporomosha wengine.

3. Kutojiuliza maswali (Lack of Discovery Questions)​

Badala ya kutoa maamuzi ya haraka kama “Tukutane kesho saa nane,” ni bora kuuliza: “Je muda wa saa tisa unakufaa kesho?” Hii inaonyesha heshima kwa muda wa mteja na inasaidia kupanga ratiba inayoeleweka kwa pande zote.

4. Haraka haraka kufunga mauzo​

Wengine hujaribu kufunga mauzo mapema sana kabla hata mteja hajawa tayari. Hii ni sawa na kumposa mtu mnapokutana kwa mara ya kwanza. Hakikisha umejibu maswali yote, umeondoa mashaka yote, ndipo uombe mteja afanye maamuzi ya kununua.

5. Kutofuatilia (Not Following Up)​

Si kila mteja anasema “nitafikiria” anamaanisha hapendi. Wengine kweli wanahitaji muda. Usimwache hivyo hivyo. Mfate kwa heshima. Mfano: “Hi! Nilitaka kujua kama bado uko na interest na huduma yetu kuhusu XYZ.” Hii ni follow-up yenye adabu na matokeo.

6. Kutokua na walengwa sahihi​

Unaweza kuongea na watu wengi, lakini kama sio walengwa wako (target market), hautafunga mauzo. Epuka kujaribu kuuza kwa kila mtu. Chuja — tafuta watu wenye shida halisi ambayo bidhaa zako zinaweza kutatua. Hawa ndio walengwa sahihi.

7. Kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya bidhaa unayouza​

Kama hujui bidhaa yako ndani na nje, hutajenga imani kwa mteja. Mteja atagundua tu. Akiuliza swali na jibu lako linakuwa “sijui vizuri,” umepoteza uaminifu. Hakikisha unajua faida, vipengele, matokeo, na tofauti ya bidhaa zako na nyingine sokoni.

8. Kubishana na wateja​

Wafanyabiashara wanaopenda kushindana na wateja kwa hoja hukosa dili. Lengo sio kushinda hoja, ni kushinda mauzo. Badala ya kubishana, uliza maswali: “Naona unahisi bei ipo juu, je ni nini hasa unachoangalia kwenye bidhaa kama hii?” Hii itakusaidia kuelewa mzizi wa mashaka yake.

9. Kutoa ahadi kubwa zisizotimia​

Ahadi kubwa hazina maana kama hazitimizwi. Usimwambie mteja, “Utanona upungue kilo 5 kwa wiki moja” kama huwezi kuthibitisha. Mteja atarudi kusema ulimdanganya, na utaharibu jina la biashara yako. Toa ahadi ndogo zenye matokeo makubwa, si ahadi kubwa zisizo na msingi.

10. Kuweka mkazo kwenye bei badala ya thamani​

Wateja hawako after bei ndogo pekee — wanatafuta value. Badala ya kusema “bei yetu ni nafuu kuliko ya wengine,” sema: “Bidhaa hii inasaidia A, B, na C, na ndiyo maana inathamani hiyo.” Ukieleza thamani vizuri, hata bei ya juu haitakuwa kikwazo.

11. Kuchelewa kujibu mteja​

Mteja akikuandikia leo halafu unamjibu kesho — tayari ameshaongea na mpinzani wako. Kasi ya response ni sehemu ya huduma bora kwa mteja (customer experience). Wateja wanapenda kuhudumiwa kwa haraka na kwa heshima. Usichelewe — jibu kwa wakati.

12. Kutokuelewa ‘Timing’ ya mteja​

Wapo walengwa ambao wakikupa ishara kwamba “usinitafute tena” au “sitaki huduma yako” — ni lazima uheshimu hilo. Usimlazimishe follow-up zisizo na tija. Kusoma alama za nyakati (reading client signals) ni sehemu ya ujuzi wa kibiashara.

13. Kuona kila mtu ni mteja​

Biashara ni sayansi na sanaa. Sio kila mtu atakuwa mteja wako. Ukijaribu kuuza kwa kila mtu utapoteza muda, nguvu na pesa. Elekeza nguvu zako kwa watu wanaopaswa kupokea huduma zako.

Kila kosa katika orodha hii lina gharama ya muda, fedha, jina lako, na uaminifu wa mteja. Kila unapotengeneza mfumo wa kufunga mauzo, rudi kwenye orodha hii, jikague, jikosoe, na rekebisha mapungufu yako.
 
Back
Top Bottom