Mkemia Fred James
Member
- Jul 31, 2022
- 45
- 98
1. Usivichukulie "POA" vitu vidogovidogo kwasababu vitakugharimu.
2.Usiseme Uongo kwa kumfurahisha mtu ni heri kumuumiza kwa ukweli.Hio itasawasaidia kuokoa muda na maumivu hapo baadae.
3.Wanadamu wa leo hawaaminiki na hawazoeleki.Usimwambie kila mtu siri za maisha yako hasa katika maswala nyeti hasa Uchumi wako.
4.Usivute sigara na pombe kwasababu ni hatari kwa afya yako. Hupangiwi, Chaguo ni lako.
5. Usijiambie maneno mabaya na magumu kwasababu yatakuharibu kuliko maneno ya watu wa nje.Mungu anakusikiliza.
6.Usiwaze kupitiliza bali fanya mambo yako kupitiliza upate matokeo unayoyataka.
7.Usipoteze "ASILI" yako kwasababu ya watu. Kubali kuwa wa kipekee pasipo kuwafurahisha watu kwa kuvaa koti "FAKE"
8. Usiangalie picha au video za "NGONO"kwasababu zitaathiri akili yako na kufyonza nguvu zako za kimwili na kiroho.
9. Usijitengenezee marafiki wengi kupitiliza kwasababu kati yao watakuharibu.
10. Usitegemee "VYETI" vya taaluma yako pekee kwasababu zipo mbegu zilizokuwa ndani yako kabla hujapata vyeti,Ukiotesha utavuna.
11.Usiingie au kubaki kwenye mahusiano "FAKE".Utalizwa.
12.Usijitie upofu kwa Kung"ania mtu au watu UNAOJUA wataweza kuharibu maisha/taaluma yako.Waache waende.
13.Usijilinganishe "MTU".Kila mtu ni wa kipekee duniani na kila mtu ana kilele cha udhaifu wake.Jilinganishe na wewe mwenyewe.
14.Usipoteze "MATUMAINI" kwasababu "Kila siku tunalala bila kujua tutaamka au la ! Japokuwa tunaweka alarm.
15. Usiogope"MABADILIKO" kwasababu yatakufanya "UKUE".
16.USIOGOPE,Amini uwezo wako.Ziamini mbawa zako,hutajuta.
17.Usilumbane na watu kwani hio ni dalili ya "UTOTO"
18.Usimtegemee mtu/ vitu kwasababu kila kitu ni cha "MUDA"
19.Usijali ni "KIPI" watu watasema juu yako kwasababu huwezi kuwazuia kuongea juu yako.
20."USIGHAIRISHE"malengo yako kwasababu hutayafikia.Kumbuka hilo.
22.Usiwe "CHANZO" cha uharibifu wa vitu vya watu mfano ,Mali ,ndoa za watu,elimu za watu, watoto wa watu,kazi na maono ya watu,nk.Utalipa.
23. Usijinyime "FURAHA" maisha ni mafupi.Fanyika furaha kwa watu sio huzuni na mateso.
24. Usikubali KUOA AU KUOLEWA" na mtu usiyempenda.Chagua type yako.Utaenjoy.
25."USIMUACHE MUNGU"zishike amri zake kwasababu wewe ni mavumbi na mavumbini utarudi..Hujafa hujaumbika.
Vipo vingi vya kuacha kufanya ili maisha yawe bora zaidi ya jana. Unaweza kuongeza mengine ambayo HUPASWI KUFANYA.
Kura yako ni muhimu.
Tuendelee kujifunza.
Enjoy.