Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,526
- 34,057
Kazi yoyote ya mikono ya binadamu itakuwa na makosa.
Kazi iliyokamilika ni yake Allah peke yake.
Yameonekana makosa katika kitabu cha Mwalimu Nyerere.
Prof. Kabudi ana haya ya kusema kuhusu makosa hayo:
"Mzee wa Atikali" (MwA) amepigiwa simu na Mhe Prof. Palamagamba Kabudi. Baada ya kuongea kwa saa nzima, itoshe kufupisha alichonena Mhe Waziri kama ifuatavyo:
"Mzee wa Atikali" "nimetua tu hapa Arusha nikakuta rafiki yangu wa Ujerumani kanitumia makala yako. Ni makala nzuri na nashukuru sana kwa yote uliyoyaandika. Tunafanya tafsiri ya Kitabu cha Kiswahili na naahidi kasoro zote ulizozianisha tutaziweka kwenye kitabu hicho. Pia, tunaangalia namna ya kukutumia uwe unapitia. Mimi huwa nasoma sana Atikali zako. Ni nzuri sana."
"Najua Tabitha Siwale, Mwanamke wa Kwanza kuwa Waziri ni mama yako mkubwa na humo kuna picha zake za kipekee. Nikirudi tu Dar es Salaam ntakupa nakala moja ya Kitabu hiki umpe Mama yako, najua atafurahi kumuona dada yake. Basi nikupongeze kwa kazi nzuri uifanyayo".
Prof. PALAMAGAMBA KABUDI, Aprili 28, 2025, Saa 9 Alasiri.
Hebu tuangalie niliyoandika hapo chini baada ya kumsoma Prof. Kabudi:
PROF. KABUDI, ATIKALI NA HISTORIA YA TABITHA SIWALE
Nimepokea msg nyingi kutoka kwa watu wengi kuhusu makosa aliyoyaona Atikali katika kitabu, "Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Photographic Journey," ambayo Prof. Kabudi kayatolea maelezo.
Kuna mengi ningeweza kusema lakini hapa nataka In Shaa Allah kueleza hili la Tabitha Siwale.
Hakika huyu mama kakosewa historia yake.
Lakini muhimu ni kuwa juu ya makosa hayo Tabitha Siwale yumo katika kitabu cha Mwalimu Nyerere.
Angalau yeye yumo katika historia na kuhusishwa na Baba wa Taifa.
Wako wanawake wamefanya makubwa tena katika kipindi kigumu cha kupigania uhuru wa Tanganyika.
Hawa si tu kuwa hawamo katika kitabu cha Mwalimu Nyerere bali wamefutika kabisa katika historia nzima ya Tanzania.
Nani anawajua akina mama hawa wazalendo hapo chini?:
Hawa hawamo katika kitabu cha Mwalimu Nyerere wala hawapo popote.
Shariffa bint Mzee wa Lindi hayumo kwenye kitabu cha Mwalimu Nyerere.
Halikadhalika Bi. Aza wa Kilwa, Zarula bint Abdulrahman, Nyange bint Chande (Tabora), Chiku bint Said Kisusa, Tatu bint Mzee, Hawa bint Maftah, Halima Khamis, Bi. Mwamtoro bint Chuma (Kariakoo), Halima Selengia, Mama bint Mwalimu, Amina Kinabo (Moshi), Fatma bint Matola (Mbeya) kwa kuwataja wachache ninaowajua mimi.
Wanawake hawa wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika walikuwako nchi nzima.
Nini ndugu zangu kifanyike ili tuwe na historia iliyokamilika angalau kidogo?
Hebu angalia video hiyo hapo chini:
View: https://youtu.be/p1ZdZl1wwic