Metronidazole 400mg
JF-Expert Member
- Aug 25, 2016
- 941
- 2,062
- Thread starter
-
- #21
1...Vipi ngoma,mzamiru na kanoute waanza kwa pamoja, mmoja aanze kukabia juu??Ni kweli ulio dhahiri Simba ina tatizo la kiungo mkabaji aina ya Lwanga au Fraga. Haihitaji ufundi sana kujua haya mapungufu pale Simba kwani kwa kuhesabu tu idadi ya "clean sheets" kwenye mashindano yote iliyoshiriki Simba msimu huu unapata jibu hapo hapo. Pia ijulikane wazi kuwa sio mechi zote timu inatakiwa icheze na kiungo asili mkabaji kwani baadhi ya mechi timu inapokutana na timu dhaifu au timu iliyopaki basi sio lazima icheze na kiungo mkabaji asili.
Lakini kama Simba ina benchi la ufundi lenye weledi hilo tatizo linaweza tu kupunguzwa kwa kiasi kikubwa kwa muda huu mpaka kipindi cha usajili kwa kufanya yafuatayo:-
1. Kutafuta mchezaji mwingine mwenye uelekeo wa ukabaji "kumtrain" na kumpa majukumu hayo mapya kwa muda mpaka usajili ufike. Kwa benchi la ufundi lenye watalaam hii sio kazi kubwa na ndio maana halisi ya kuitwa benchi la ufundi inapodhihirika. Hapa bila chenga benchi la ufundi limkamate Muzamiru limtengeneze apunguze baadhi ya makosa atawasaidia mpaka mwishoni mwa msimu bila wasiwasi wowote. Kuna watu watasema mbona Muzamiru ndio nafasi yake anayocheza kila siku jibu ni ndio. Lakini bado anatakiwa aongezewe vitu viwili vitatu ili aweze kuiilinda "back four" yake vizuri.
2. Timu kukaba pamoja na kushambulia kwa pamoja. Swali kubwa hapa tujiulize je Simba hii ya sasa ina pumzi na stamina ya kushambulia na kukaba pamoja kwa dakika tisini za mchezo? Jibu ni hapana kwani timu huwa inakata moto kuanzia dakika ya 60/65. Sina hakika sana na uwezo wa makocha wa viungo wa Simba kama wanalingana na hadhi ya timu hii bora kabisa Afrika.
3. Benchi la ufundi kufanya maamuzi magumu ya kuwachezesha kwa pamoja Inonga na Kennedy kama mabeki wa kati halafu kumsogeza Che Malone acheze mbele yao kwenye zile mechi ambazo Simba inaamua kuzuia zaidi na kushambulia kwa kushtukiza.
4. Benchi la ufundi liache kukariri kumchezrsha Saidoo kama namba kumi wakati hawezi kuichezesha timu kuanzia katikati kwenda mbele na anapoteza mipira mingi sana bila sababu za msingi. Matokeo yake ndio hayo mipira mingi inayopotea kwa Saidoo ndio inawatesa mabeki na makipa pale Simba japo haionekanii haraka kwa sababu tu inakuwa imenyangánywa kwenye upande wa goli la adui. Hii kiufundi hauwezi kuiona kiurahisi mpaka uangalie mpira kwa kutulia sana. Simba inao namba kumi wengi wa kutosha ambao wanaweza kukaa na mipira miguuni na kuichezesha timu vizuri tu sijui kwani benchi la ufundi halitaki kuwatumia pale kati badala yake linawapanga pembeni na kumwacha Saidoo aendelee kuiumiza timu kwa kuwachosha wenzake muda wote wa mchezo. Kama benchi la ufundi linaona Simba ni Saidoo na Saidoo ni Simba basi limpange acheze pembeni walau akipoteza mipira huko inakuwa haina madhara sana kulinganisha na kati kati ya uwanja.
Yote kwa yote hata mtu aliyecheza mpira mchangani kwa hawa makocha wetu ambao hawajaenda darasa hata moja la ukocha bado angefanya yote niliyoeleza hapo juu ili kuficha madhaifu ya usajili yaliyofanyika wakati wa usajili ya kuacha kusajili kiungo mkabaji asili. Sijajua kwa nini mpaka sasa ambapo Simba imecheza takribani mechi zaidi ya tano lakini bado hayo madhaifu hayajapunguzwa kitu ambacho ni hatari sana hasa siku Simba itakapokutana na mpinzani mwenye kuujua mchezo na mwenye uwezo wa kutumia nafasi zinazpotikana vizuri. Je Simba ina kamati ya ufundi? Kama ipo na yenyewe haijaona hili tatizo?
Ni mtizamo tu.
2....chama,saidoo waanzie benchi(tunajua ndio waamuzi wa mechi hilo halina Shaka)....pale mbele waanze bocco na phiri(4-4-2) lengo Ni kutengeneza balance ya kuzuia zaidi, Alafu kuanzia dakika ya 70, kutegemeana na matokeo unachomoa kiungo mmoja au wawili Alafu unaingiza mashine za kazi
Hasa kwa hi mechi ya Al Ahly inabidi inabidi tuwe makini Sanaa......