Makosa kikosi cha Simba haya hapa

Makosa kikosi cha Simba haya hapa

Ni kweli ulio dhahiri Simba ina tatizo la kiungo mkabaji aina ya Lwanga au Fraga. Haihitaji ufundi sana kujua haya mapungufu pale Simba kwani kwa kuhesabu tu idadi ya "clean sheets" kwenye mashindano yote iliyoshiriki Simba msimu huu unapata jibu hapo hapo. Pia ijulikane wazi kuwa sio mechi zote timu inatakiwa icheze na kiungo asili mkabaji kwani baadhi ya mechi timu inapokutana na timu dhaifu au timu iliyopaki basi sio lazima icheze na kiungo mkabaji asili.

Lakini kama Simba ina benchi la ufundi lenye weledi hilo tatizo linaweza tu kupunguzwa kwa kiasi kikubwa kwa muda huu mpaka kipindi cha usajili kwa kufanya yafuatayo:-
1. Kutafuta mchezaji mwingine mwenye uelekeo wa ukabaji "kumtrain" na kumpa majukumu hayo mapya kwa muda mpaka usajili ufike. Kwa benchi la ufundi lenye watalaam hii sio kazi kubwa na ndio maana halisi ya kuitwa benchi la ufundi inapodhihirika. Hapa bila chenga benchi la ufundi limkamate Muzamiru limtengeneze apunguze baadhi ya makosa atawasaidia mpaka mwishoni mwa msimu bila wasiwasi wowote. Kuna watu watasema mbona Muzamiru ndio nafasi yake anayocheza kila siku jibu ni ndio. Lakini bado anatakiwa aongezewe vitu viwili vitatu ili aweze kuiilinda "back four" yake vizuri.
2. Timu kukaba pamoja na kushambulia kwa pamoja. Swali kubwa hapa tujiulize je Simba hii ya sasa ina pumzi na stamina ya kushambulia na kukaba pamoja kwa dakika tisini za mchezo? Jibu ni hapana kwani timu huwa inakata moto kuanzia dakika ya 60/65. Sina hakika sana na uwezo wa makocha wa viungo wa Simba kama wanalingana na hadhi ya timu hii bora kabisa Afrika.
3. Benchi la ufundi kufanya maamuzi magumu ya kuwachezesha kwa pamoja Inonga na Kennedy kama mabeki wa kati halafu kumsogeza Che Malone acheze mbele yao kwenye zile mechi ambazo Simba inaamua kuzuia zaidi na kushambulia kwa kushtukiza.
4. Benchi la ufundi liache kukariri kumchezrsha Saidoo kama namba kumi wakati hawezi kuichezesha timu kuanzia katikati kwenda mbele na anapoteza mipira mingi sana bila sababu za msingi. Matokeo yake ndio hayo mipira mingi inayopotea kwa Saidoo ndio inawatesa mabeki na makipa pale Simba japo haionekanii haraka kwa sababu tu inakuwa imenyangánywa kwenye upande wa goli la adui. Hii kiufundi hauwezi kuiona kiurahisi mpaka uangalie mpira kwa kutulia sana. Simba inao namba kumi wengi wa kutosha ambao wanaweza kukaa na mipira miguuni na kuichezesha timu vizuri tu sijui kwani benchi la ufundi halitaki kuwatumia pale kati badala yake linawapanga pembeni na kumwacha Saidoo aendelee kuiumiza timu kwa kuwachosha wenzake muda wote wa mchezo. Kama benchi la ufundi linaona Simba ni Saidoo na Saidoo ni Simba basi limpange acheze pembeni walau akipoteza mipira huko inakuwa haina madhara sana kulinganisha na kati kati ya uwanja.

Yote kwa yote hata mtu aliyecheza mpira mchangani kwa hawa makocha wetu ambao hawajaenda darasa hata moja la ukocha bado angefanya yote niliyoeleza hapo juu ili kuficha madhaifu ya usajili yaliyofanyika wakati wa usajili ya kuacha kusajili kiungo mkabaji asili. Sijajua kwa nini mpaka sasa ambapo Simba imecheza takribani mechi zaidi ya tano lakini bado hayo madhaifu hayajapunguzwa kitu ambacho ni hatari sana hasa siku Simba itakapokutana na mpinzani mwenye kuujua mchezo na mwenye uwezo wa kutumia nafasi zinazpotikana vizuri. Je Simba ina kamati ya ufundi? Kama ipo na yenyewe haijaona hili tatizo?

Ni mtizamo tu.
1...Vipi ngoma,mzamiru na kanoute waanza kwa pamoja, mmoja aanze kukabia juu??

2....chama,saidoo waanzie benchi(tunajua ndio waamuzi wa mechi hilo halina Shaka)....pale mbele waanze bocco na phiri(4-4-2) lengo Ni kutengeneza balance ya kuzuia zaidi, Alafu kuanzia dakika ya 70, kutegemeana na matokeo unachomoa kiungo mmoja au wawili Alafu unaingiza mashine za kazi

Hasa kwa hi mechi ya Al Ahly inabidi inabidi tuwe makini Sanaa......
 
Tukiwa ugenini syo shida, Ila hapa nyumbani hakuna haja ya kujilinda kwani Al ahly hapa atakuja kujilinda, HIVYO tukitumia wachezaji wanao press kwa kas na akil Kama chama tunawaweza, nao pia wanahofu kucheza na Simba kwa mkapa.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]sawa mkuu....ila Al Ahly popote Africa Ni Kama nyumbani tu
 
Hawa Al ahly, hata timu nyingine za waarabu, wakiwa ugenini hujilinda Zaid Ila nyumban ndio hufunguka, ndio maana hata hao Al ahly hajawah mfunga Simba kwa Mkapa, lakini kwao Simba kapigwa 5 hata Yanga kashamfunga Al ahly kwa mkapa. Ndugu nikuhakikishie game ya kwa Mkapa Simba atadominate, kazi itakuwa Misri
 
Wakuu,

Haya ni makosi ya kiufundi ambayo Mimi binafsi nimeyaona toka msimu huu kuanza na huenda yakatu cost hasa kwenye mechi za kimataifa.

1. Kiungo mkabaji (DM)
Umejiuliza Ni kwanini tunaruhusu Sana magoli ligi kuu?

JIBU ni rahisi hatuna kiungo mkabaji mwenye utukutu flani aina ya lwanga, aucho au bajana wa Azam hivyo safu ya ulinzi inafikiwa kirahisi sana.

Binafsi naona Che Malone anafanya majukumu yanayomzidi kwani unaweza kusema yeye ndio DM kumbe Ni center back. Natarajia kuona makosa mengi hasa mwenye mechi za kimataifa kama safu ya ulinzi itaendelea kuwa hivi ni ngumu sana kutoboa

Mzamiru,kanoute na ngoma ni wachezaji wenye kaliba zinazoendana. Ngoma hapendi mpira wa kugongana kabisaa na pia timu ikiwa haina mpira afu akutane na timu yenye kasi anapotea Sana sababu yupo slow.

2. WITHOUT BALL
Kwanini robertinho anamwamini Kibu?
  • Upambanaji (toughness)
  • Without ball huyu jamaa anafanya kazi kubwa Sana anapress,anakaba mpaka mda mwingine anaingia ndani kuwa Kama kiungo
Kingine; Saido, Chama, Phiri, Onana, Hawa Ni wachezaji utawaona timu ikiwa na mpira Sanasana bila mpira huwaoni hata ukiona kwenye kukaba wana struggle na wakijitahidi wanaishia kutoa faulu

Tupeane Moyo tu ila kwenye Mechi za kimataifa kazi ipoo.....inabidi kocha afanye kazi kubwa Sanaa hasa kwenye kiungo.
Hivi,ni timu ya Simba tu ndiyo ipo kwenye mashindano?Hakuna nyingine/zingine?Hizo zingine ni bora na hazina upungufu wowote?Kwa nini kila uzi ni Simba tu?Nauliza kwa uzuri tu nipate jawabu.
 
Sababu kubwa Simba ndiye Mwakilishi pekee wa nchi yetu, Katika hayo mashindano, hvyo haya mapungufu pengine husemwa kwa ubaya ama kwa uzuri.
 
1...Vipi ngoma,mzamiru na kanoute waanza kwa pamoja, mmoja aanze kukabia juu??

2....chama,saidoo waanzie benchi(tunajua ndio waamuzi wa mechi hilo halina Shaka)....pale mbele waanze bocco na phiri(4-4-2) lengo Ni kutengeneza balance ya kuzuia zaidi, Alafu kuanzia dakika ya 70, kutegemeana na matokeo unachomoa kiungo mmoja au wawili Alafu unaingiza mashine za kazi

Hasa kwa hi mechi ya Al Ahly inabidi inabidi tuwe makini Sanaa......
Imekaa poa sana na mpira unaujua. Naamini siku ambayo benchi la ufundi litakapoamua kumjaribu Ngoma kucheza namba kumi basi huenda ndio siku hiyo ikawa mwisho wa mtoto wao pendwa Saidoo kucheza kila mechi na mbao ndefu itamhusu kwa muda mrefu sana sio kwa kupoteza kule mpira halafu mwisho wa mechi kila Robertino akihojiwa lazima amsifu eti kacheza vizuri wakati mpira ni mchezo wa wazi. Mbaya zaidi anapomtoa Kibu uwanjani mwenye "workrate" kubwa na kumuacha Saido amalize dakika zote 90 ilihali unakuta kachoka hoi hata akipiga pasi ya mita mbili haifiki.

Na mabadiliko ya namba kwa wachezaji ni kitu cha kawaida sana kwenye benchi la ufundi lenye watu wenye weledi lakini kwa Simba wamekariri wachezaji wale wale kama vile timu zote pinzani wanazokutana nazo zina cheza mfumo mmoja. "No wonder" sasa hivi tofauti ya ushindi ni goli moja au mawili na timu inapelekewa moto mbaya kiasi inabidi benchi la ufundi liingize watu wa kulinda matokeo saa nyingine unakuta ndio kwanza mpira upo dakika ya 70.
 
Mkubwa hutizamwa zaidi na huzungumzwa zaidi, Sasa Africa nzima kwenye Mpira wa miguu wanaongelewa Al ahly na Simba zaidi, ijapo mashindano haya Yana shirikisha timu 8, sababu kubwa NI kuwa wafunguzi, timu Kama singida Bado Haina legacy kwenye Mpira wa Africa labda cku za usoni.
 
Kwa sasa hivi Simba kuzungumziwa ndio wakati wake maana ana mechi kubwa sana hivi karibuni. Yakianza makundi zitazungumziwa timu zote mbili kubwa Simba na Yanga.
 
Tukiwa ugenini syo shida, Ila hapa nyumbani hakuna haja ya kujilinda kwani Al ahly hapa atakuja kujilinda, HIVYO tukitumia wachezaji wanao press kwa kas na akil Kama chama tunawaweza, nao pia wanahofu kucheza na Simba kwa mkapa.
Anajilinda na nini sasa?
 
Wakuu,

Haya ni makosi ya kiufundi ambayo Mimi binafsi nimeyaona toka msimu huu kuanza na huenda yakatu cost hasa kwenye mechi za kimataifa.

1. Kiungo mkabaji (DM)
Umejiuliza Ni kwanini tunaruhusu Sana magoli ligi kuu?

JIBU ni rahisi hatuna kiungo mkabaji mwenye utukutu flani aina ya lwanga, aucho au bajana wa Azam hivyo safu ya ulinzi inafikiwa kirahisi sana.

Binafsi naona Che Malone anafanya majukumu yanayomzidi kwani unaweza kusema yeye ndio DM kumbe Ni center back. Natarajia kuona makosa mengi hasa mwenye mechi za kimataifa kama safu ya ulinzi itaendelea kuwa hivi ni ngumu sana kutoboa

Mzamiru,kanoute na ngoma ni wachezaji wenye kaliba zinazoendana. Ngoma hapendi mpira wa kugongana kabisaa na pia timu ikiwa haina mpira afu akutane na timu yenye kasi anapotea Sana sababu yupo slow.

2. WITHOUT BALL
Kwanini robertinho anamwamini Kibu?
  • Upambanaji (toughness)
  • Without ball huyu jamaa anafanya kazi kubwa Sana anapress,anakaba mpaka mda mwingine anaingia ndani kuwa Kama kiungo
Kingine; Saido, Chama, Phiri, Onana, Hawa Ni wachezaji utawaona timu ikiwa na mpira Sanasana bila mpira huwaoni hata ukiona kwenye kukaba wana struggle na wakijitahidi wanaishia kutoa faulu

Tupeane Moyo tu ila kwenye Mechi za kimataifa kazi ipoo.....inabidi kocha afanye kazi kubwa Sanaa hasa kwenye kiungo.
MBUMBUMBU WOTE WABOVU HAO
 
Ni Mara 1000 ukampa nafasi Kanoute kuliko Ngoma... Kwa amayefuatilia mpira kwenye kikosi Cha Simba mchezaji anayeongoza kupoteza pasi na kukabia macho ni Ngoma...., Simba wanaogopa kumsema kwasababu walishangilia walipodanganywa ati kaibiwa Airport!!.
Kanoute ana risk kuwalinda mabeki ila Ngoma anajilinda yeye, Kama ataanzisha mechi ya trh 20 basi hamsa hamsa tunaziona hizoooooo😀
 
Hivi,ni timu ya Simba tu ndiyo ipo kwenye mashindano?Hakuna nyingine/zingine?Hizo zingine ni bora na hazina upungufu wowote?Kwa nini kila uzi ni Simba tu?Nauliza kwa uzuri tu nipate jawabu.
Mimi Ni Simba damu ivyo naiongelea timu yangu....wenye singida,yanga n.k nao watapata nafasi ya kuongelea timu zao kwa muda wao
 
Imekaa poa sana na mpira unaujua. Naamini siku ambayo benchi la ufundi litakapoamua kumjaribu Ngoma kucheza namba kumi basi huenda ndio siku hiyo ikawa mwisho wa mtoto wao pendwa Saidoo kucheza kila mechi na mbao ndefu itamhusu kwa muda mrefu sana sio kwa kupoteza kule mpira halafu mwisho wa mechi kila Robertino akihojiwa lazima amsifu eti kacheza vizuri wakati mpira ni mchezo wa wazi. Mbaya zaidi anapomtoa Kibu uwanjani mwenye "workrate" kubwa na kumuacha Saido amalize dakika zote 90 ilihali unakuta kachoka hoi hata akipiga pasi ya mita mbili haifiki.

Na mabadiliko ya namba kwa wachezaji ni kitu cha kawaida sana kwenye benchi la ufundi lenye watu wenye weledi lakini kwa Simba wamekariri wachezaji wale wale kama vile timu zote pinzani wanazokutana nazo zina cheza mfumo mmoja. "No wonder" sasa hivi tofauti ya ushindi ni goli moja au mawili na timu inapelekewa moto mbaya kiasi inabidi benchi la ufundi liingize watu wa kulinda matokeo saa nyingine unakuta ndio kwanza mpira upo dakika ya 70.
Akiwa Al hilal omdurman ya Sudan(kiboko ya Utopoloz) kocha florent ibenge alipenda zaidi kumtumia juu na alikuwa anafanya vizuri Ila Mara nyingi kwenye dakika65 kuendelea anamtoa.....hii ni wazi inamaanisha Ni mtu wa kukata upepo mapema
 
Ni Mara 1000 ukampa nafasi Kanoute kuliko Ngoma... Kwa amayefuatilia mpira kwenye kikosi Cha Simba mchezaji anayeongoza kupoteza pasi na kukabia macho ni Ngoma...., Simba wanaogopa kumsema kwasababu walishangilia walipodanganywa ati kaibiwa Airport!!.
Kanoute ana risk kuwalinda mabeki ila Ngoma anajilinda yeye, Kama ataanzisha mechi ya trh 20 basi hamsa hamsa tunaziona hizoooooo[emoji3]
Weakness ya Fabrice anakataa moto mapema/anachoka huwezi mchezesha Kama namba6 Alafu ukamuamini kwa dk zote 90.....BIG NO KWANGU!!!!
 
  • Thanks
Reactions: Exy
Back
Top Bottom