Makosa makubwa ya Uaandaaji wa Maonyesho ya Kilimo Nane Nane

Makosa makubwa ya Uaandaaji wa Maonyesho ya Kilimo Nane Nane

Dar wanalima nini
Hahaha! tunalima sana huku nakufuga. Kuna haja ya kuwa na mtazamo mpana wa kilimo na ufugaji. Sekta ya Kilimo na ufugaji inatakiwa iwe integrated na other sectors. Nadhani Kuna wataalamu wenye uelewa mpana kwenye jambo hili, hapo ndio tunapata msingi wa maonyesho ya kilimo kufanyika Dar Es Salaam
 
Mwaka wa Kwa yalifanyika morogoro bila kuwepo na hizo kanda na idea ilikuwa yatakuwa yanafanyika hapo tu na watu tulishauriwa kujenga mabanda ya kudumu kwani maonyesho yatakuwa yakifanyika hapo kitaifa permanent ghafla walamba asali wakaiona fursa tukasikia Kanda nikachoka kabisa ndio ujenzi wa vibanda na maonyesho kukosa seriousness kukaanza
Mbona hata Arusha kuna Mabanda ya Kudumu?
 
Samahani bingwa, naona umekomaa na "MAONYESHO", hapo post #8, ilimradi tu kusema una EKSIPOSHA, rifaaringi to "Wabongo Bhana"

  • Onesho, -on-
  • Onyo, -ony-
Punguza ujuaji wa kipimbi? Nazani wewe huna ulicho ambulia zaodi ya hio?
 
huna ulicho ambulia
Ni kweli ila matusi hayo ya reja reja ndo yamekufanya ukahangaika kutafuta ID nyingine? Zote ni fake.

Ebu tukana vizuri, na kwa nguvu kidogo ukiwa umegangamala ili ku-justify energy dissipated
 

Yakiwa Morogoro Itakuwa Sawa Sawa Wajenge Ya Kudumu

 
Ni kweli ila matusi hayo ya reja reja ndo yamekufanya ukahangaika kutafuta ID nyingine? Zote ni fake.

Ebu tukana vizuri, na kwa nguvu kidogo ukiwa umegangamala ili ku-justify energy dissipated
yaani vichwa vinatoa point humu wewe umekomaaa na kukosoa kutafuta makosa, hii ni aina ya utopolo una roho kama ya kenge
 
Ni ushauri mzuri ila ungemuadress waziri wa kilimo moja kwa moja kwa kichwa hiki; BARUA YA WAZI KWA WAZIRI WA KILIMO NA MIFUGO; USHAURI.
Huyo waziri yupo?
Mi naona km ni Bashe tu anafanya kazi.amuaddress bashe direct
 
Wanaokupa hongera, wamejua kuwa wazo lako umelichukua hapa kenya?

Hongera kwa kucopy na kupaste.
Hapo Juu nimeeleza Mbona? Kwamba Kenya ndio wanavyo Fanya, au Tatizo nini? Au unazani wazo nimelitoa Mbinguni?
 
Ukiachana na MUDA na SEHEMU

Kuna suala zima la WASHIRIKI na USHIRIKISHWAJI

Nimehudhuria haya maonyesho tangu yakiitwa SABASABA miaka takriban miaka 35 iliyopitaj, kwa kweli haya maonyesho bado yana taswira ya SIKUKUU zaidi kuliko MAONYESHO

Nasema hivyo kwa sababu kuna vitu vina chukua nafasi ktk maonyesho haya ambavyo havina uhusiano wa moja kwa moja na Kilimo. Kwa mfano wauza mitumba ambao hujazana pale Nanenane Morogoro
Makelele(Sound Pollution)yamekuwa mengi utafikiri tuko Mtaa wa Congo

Naamini waandaaji wana exposure ya kutosha kufanya maonyesho mazuri wapewe nafasi tu
 
Maonyesho ya Kilimo ya Nane Nane yana Makosa mengi sana ya kimkakati na nashindwa kuelewa kwa nini Waandaaji na watalamu hawalioni hili.

Maonyesho ya Nane nane yamekuwa yakifanyika kwenye kanda hizi.

1.Arusha
2.Dodoma
3.Mwanza
4. Tabora
5.Morogoro
6.Mbeya
7.Iringa
Simiyu sina uhakika sana huko kwa Andrea Chenge.

Katika hizo kanda moja huchaguliwa kuandaa kitaifa. Sana Dodoma na kwa nyakati kadhaaa ni huko Simiyu.

Haya Maonyesho hizo kanda zote huanza kwa wakati mmoja yaani tarehe 1 mwezi wa 8 na kumalizika tarehe 8.

Nikiwa kama mtalamu, Mvumbuzi, au Mfanya Biashara inabidi katika hizo kanda zote nichague kwa kwenda, hapa sana wengi huchagua Morogoro na Arusha ambako kuna Power sana na kuna kuwa na wahudhuriaji wengi sana.

Maana yake hizo kanda zingine zinazo bakia sitaweza kwenda kabisa, au nituma timu yangu watajigawa, hawa hawana utalamu na ninacho kizalisha wataishia kusema chukua namba mpigie mtalamu.Hii sio sawa kabisa.

Waandaaji kumbe wange gawa haya Maonyesho ya kanda katika tarehe tofauti.

Mfano:
Mwanza- Mwezi wa 5
Simiyu- mwezi wa 5 baada ya Mwanza kuisha
Tabora- mwezi wa 6 baada ya simiyu kuisha
Dodoma Mwezi 6 yakiisha ya Tabora
Mbeya Mwezi wa 7
Lindi mwezi wa 7 baada ya Mbeya
Arusha mwezi wa 7 wiki ya mwisho
Morogoro mwezi wa 8 Yanakuwa ni International au Arusha Mwezi wa 8 yanakuwa ni International


Kuwe na Perment place ya Maonyesho ya Kimataifa ya Kilimo pia yanaweza hata fanyikia Dar uwanja wa Sabasaba au Morogoro au Arusha.
Na yatambuliwe kabisa ni Maonyesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Either Dar, Morogoro au Arusha au Dodoma.

Kuwe na sehemu moja na sio kuhama hama mara Shinyanga mara Dodoma, siasa ziachwe kwenye maonyesho.

Na ukweli ni kwamba lazima yawe sehemu iliendelea na yenye Biashara kama Dar, au Arusha au Morogoro au Dodoma.

Yakianza maonyesho ya Kimataifa maana yake hizo kanda zingine zinakuwa zisha maliza so wanaweza Move wakaja kushowa sasa kwa lile onyesho la Kimataifa.

Kenya wanatumia hii system na Maonyesho yao huanza kuanzia mwezi wa 4 au 5 huwa kuna ya Elidoreti, Kisumu, Nakuru, Mombasa na lile la Kimaitafa huwa ni la Nairobi International Agriculture Show.Hii hufanya mtu kuweza ku attend maonyesho yote.


Hii ya kufanya maonyesho nchi nzima kwa wakati mmoja hayana tija sana.
Kwa ajili ya Per diems sio?
 
Back
Top Bottom