Makosa matano yaliyoonekana kwenye video ya muziki ya Zuwena ya msanii Diamond Platinumz

Makosa matano yaliyoonekana kwenye video ya muziki ya Zuwena ya msanii Diamond Platinumz

kua mchawi sio mpaka ubebe matunguli ama uvae kaniki hiki unacho kifanya ni uchawi na majungu bwana mdogo
nime pitia thread zako za humu jf sijaona hata moja uliyo wahi kueleza mazuri ya Diamond zaidi tu unaleta ujuaji mwiingi wa kuchambua video yake ajabu n kua kabla ya hii video kutoka kuna video za wasanii mbali mbali ambazo pia zili tangulia kutoka je hazikua na makosa?
maana sijaona popote ulipo chambua alafu pia diamond ni kama maji alisha waambia mna mchukia lakin haishi midomoni mwenu playlist zenu zime jamaa nyimbo zake

Ujuaji mwiiingi kumbe ni mabogas empty head kabisa
Pambafff wewe
 
kua mchawi sio mpaka ubebe matunguli ama uvae kaniki hiki unacho kifanya ni uchawi na majungu bwana mdogo
nime pitia thread zako za humu jf sijaona hata moja uliyo wahi kueleza mazuri ya Diamond zaidi tu unaleta ujuaji mwiingi wa kuchambua video yake ajabu n kua kabla ya hii video kutoka kuna video za wasanii mbali mbali ambazo pia zili tangulia kutoka je hazikua na makosa?
maana sijaona popote ulipo chambua alafu pia diamond ni kama maji alisha waambia mna mchukia lakin haishi midomoni mwenu playlist zenu zime jamaa nyimbo zake

Ujuaji mwiiingi kumbe ni mabogas empty head kabisa
Pambafff wewe
Sasa hii nalo balaa.

kwani Mwamba kachili kile kipindi chake cha banda la video kina dhamira gani .

majungu , entertainment au kuelimisha madirector juku ya umakini wakiwa eneo lao la kazi.

nasubiri jibu lako ZUWENA
 
Ushauri wako ni Mzuri ILA kwa nyimbo iliyoimbwa kwa mazingira ya kitanzania na kulenga soko la watanzania, Hiyo nyimbo ipo vizuri sana na wala hakuna tatizo lolote
Kimsingi kwenye mziki/video nk ina angaliwa ni soko gani umelenga, Utamaduni wa hilo soko ukoje, na kinachotokea kwenye video kina adhari gani kwenye soko nk. Nakuhakikishia 98% ya watazamaji hawana muda wakufikiria coca, wala maji, wala toyo nk

Mwisho: Kama umefuatilia mashindano ya kuimba huko ulaya/Marekani, utakubaliana na mimi kuwa tukitumia vile vigezo vyao top 10 wa kwetu wanaweza wasionekane.
Ninacho maanisha ni kuwa, tupo kwenye ulimwengu ambapo stage tuliyoko sasa hivi wenzetu walipita miaka pengine 62 iliyopita hivyo tusijilinganganishe kila kitu na wao, Sisi ndio bado tuna nyanyua mguu..... ila tupo vizuri
Nimeipenda hii na nadhani wewe ni mmoja wa ulieelewa zaidi hii lengo la hii threads
 
Imechambuliwa na kuandikwa na Ally Nassor Px .

Tarehe 5 February 2023.

Sehemu ya kwanza kuipost ni hapa JF sehemu ya pili itakuwa ni Facebook na mwisho kabisa nitamalizia Twitter.

...........................................................


Video imetoka juzi Tarehe 4 mwezi wa pili mwaka 2023.

Saa 4 kamili asubuhi.

ikiwa imeongozwa na director ivan.

mpaka sasa tarehe 5 mwezi wa pili 2023 video hii ina jumla ya watazamaji
Milioni 2.4

nilichopenda kwenye video ya zuwena ni video ambayo inaonesha uhalisia wa kinachoimbwa na ningependa kuoana zaidi na zaidi video zenye uhalisia na kile kinachoimbwa inawezekana kikatutambulisha jamii ya watanzania kirahisi kwa jamii nyingine.

Twende moja kwa moja kwenye uchambuzi wa video yenyewe.

video ni kali sana kwa upande wangu naipa rate ya 8 / 10. kuna baadhi ya makosa ya ufundi yalionekana kwenye video lakini hauwezi kuyaona mpaka utulie ila mimi nataka nikuoneshe.

..........................................................
1. MMASAI WA BANDIA

Mwanzo wa video sekunde ya 33 ( 00:33).

anaonekana jamaa wenye asili ya kimasai akikimbiza punda wawili.

ila kama utakuwa makini utangundua kuwa yule sio Mmasai halisi. wakati mmasai halisi alikuwepo kwenye video alionekana alipiga gitaa mwanzo kabisa Sekunde ya 3 ( 00: 03).
View attachment 2506707

mmasai aliyekuwa akikimbiza punda alionekana wa kutengeneza ukitazama alikuwa kavaa soksi chini na buti la Timberland (rangi ya bagia ).

View attachment 2506684
...............................................................

2. MUHUSIKA MMOJA KUOENEKANA SEHEMU MBILI TOFAUTI.

Ukitazama video sekunde ya 46 ( 00: 46).

kuna mzee utamuona alikuwa anasoma urithi. na inajulikana siku zote mtu ambaye anapewa jukumu la kusoma urithi ni mtu wenye heshima zake na anaaminiwa sana.

Sasa ukitazama video ya zuwena utamuona yule mzee aliyekuwa anasoma hosia wa urithi.

aonekana akiwa bar anamtunza zuwena alivyokuwa anacheza juu ya meza dakika ya (1 : 40).

View attachment 2506687

View attachment 2506688
...............................................................

3. TATOO ZA DIAMOND NA KIPINI PUANI.

Inawezekana ni ngumu sana kumpiga diamond make up ambayo itaficha tattoo zake. ila inaonesha director alisahau pia ata kumwambia diamond atoe japo kile kipini chake pale puani mwanzo mpaka mwisho wa video diamond anaonekana na kipini puani.

kumbuka video imebeba uhalisia wa maisha ya watu wa kipato cha chini ni ngumu sana kumkuta mtu wa kipato cha chini ana tatoo mwilini na kipini puani.

View attachment 2506689
............................................................

4. MTU KUCHEKA KWENYE TUKIO LA KUSHTUA.

Ukitazama vizuri dakika ya ( 2: 14).

kipande ambacho diamond anaenda kumuokoa zuwena alivyokuwa anataka kubakwa.

kuna jamaa mmoja kati ya wale wabakaji wanne kuna jamaa kavaa koti jeusi na suruali nyeupe. wakati wenzake wameshituka mmoja anapandisha suruali fasta fasta yeye alikuwa anamtazama mwenzake anayepandisha suruali huku akicheka.

View attachment 2506691
..............................................................

5. MATANGAZO YA MAKAMPUNI MBALIMBALI .

Mwaka 2012 Ronaldinho Gaucho alifutiwa mkataba na company ya Cocacola baada ya kuonekana chupa za Pepsi kwenye mkutano wake na waandishi wa habari.

View attachment 2506692

kuonekana chupa ya soda ya Pepsi. ila habari za Ronaldinho tuachane nazo.

Kila mtu anajua kuwa Diamond ukiachana na kujishusisha na sekta ya muziki lakini pia ni Company ambassador wa company mbalimbali.

sasa sijajua kuwa diamond ana mkataba na kampuni mbalimbali zilizoonekana kwenye video yake.

Dakika ya (1:00) Yanaonekana madish mawili ya Azam Tv juu ya mabanda yanayouza nguo.

View attachment 2506693

Dakika ya ( 2: 06) linaonekana tangazo la TTCL na DOUBLEMINT
View attachment 2506697

Dakika ya ( 2: 10 ) Diamond anaonekana anandesha pikipiki ya kutoka company ya TOYO.
View attachment 2506698

Dakika ya ( 2: 12) hadi dakika ya 2: 22) akiwa kaingia kumuokoa zuwena na anatoka pia yanaoenaka maboksi ya company ya MSAFI, KASUKU na JUMBO

View attachment 2506701

Dakika ya ( 3: 33) akiwa bar anaimba kwa mbali yanaonekana mafriji ya Coca-cola wakati kila mtu anajua diamond ni Ambassador wa Pepsi.

View attachment 2506702
....................................

6. KUONEKANA KWA NEMBO YA SERENGETI LAGER.

Uwenda point hii isiwe na nguvu sana ila point hii ndio inaweza ukaipa nguvu zaidi point namba 5 kuonekana kwa matangazo mbalimbali ya makampuni mbalimbali.

ukitazama bar watu wote walikuwa wanakunywa bia ambazo zilikuwa hazina utambulisho wa nembo kuwa ni bia za aina gani na zinatokea kampuni gani.

hii yote ilikuwa kutoonesha nembo ya kampuni ambayo diamond ana ubalozi nayo.

ila dakika ya ( 3:50) kuna kosa lilifanyika kuna muhudumu anatembea na chupa za bia. kuna chupa mmoja inaaonekana na nembo la SERENGETI LAGER.

View attachment 2506703
_____________________________________


Lengo la kuandika uzi huu sio kukosoa na kuishusha hadhi video ya msanii husika ila ni kukumbusha uwepo umakini zaidi kwa waongozi ( Madirector).

Nadhani Msanii husika hana kosa katimiza wajibu wake kwa asilimia kubwa sana kaimba nyimbo kali lakini pia ka act vizuri sana kwenye video kwa maelekezo ya director.
Mchambuzi chambua hii....Leo ni Tarehe 5...juzi ilikuwa Tarehe 4..
je..? Jana ilikuwa Tarehe ngapi..

Au sijaelewa...maana nimesoma huu uzi kidogo sana.

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Mwamba bado ataendelea kuwatesa , angalia ushauri wa kiujumla huna lengo jema, ushauri wa kimaudhui ungekuwa na ushauri wa kiujumla na sio ushauri kwa Kivuli cha chuki na wivu, na takwimu za 2.4M ni wivu wa kaburi lako mwenyewe. it was 5+M
 
Kwahiyo wenye busara hawaendi bar wala hawapokei mialiko ya sherehe ili wasikutane na machangudoa sio
kukutana na changudoa ni moja kuanza kumtunza changudoa ni la pili.

mfano wewe kukutana na shoga kwenye mizunguko yako hilo sio kosa la kwa maadili yetu ya kitanzania.

ila kumchukua na kumpa pesa kwa lengo la kwenda kumzagamua hilo ni kosa kwa maadili yetu
 
Mwamba bado ataendelea kuwatesa , angalia ushauri wa kiujumla huna lengo jema, ushauri wa kimaudhui ungekuwa na ushauri wa kiujumla na sio ushauri kwa Kivuli cha chuki na wivu, na takwimu za 2.4M ni wivu wa kaburi lako mwenyewe. it was 5+M
Screenshot_20230205-092216~2.png


wewe macho na akili zako zipo tarehe 12 ya mwezi wa pili 2023 sio leo tar 5
 
Back
Top Bottom