Makosa matano yaliyoonekana kwenye video ya muziki ya Zuwena ya msanii Diamond Platinumz

Makosa matano yaliyoonekana kwenye video ya muziki ya Zuwena ya msanii Diamond Platinumz

Badilisha simu yako upo Juba wasafi inaburuza washamba wote
😁😁😁 kumbe unaleta ushabiki sasa hapa sheikh hatuengelei ushabiki tunaongelea swala la uhalisia na ukweli.

sasa hapa itakuwa ngumu kunielewa na mimi itakuwa ngumu kukuelewa kwa sababu tuongea lugha mbili tofauti
 
kukutana na changudoa ni moja kuanza kumtunza changudoa ni la pili.

mfano wewe kukutana na shoga kwenye mizunguko yako hilo sio kosa la kwa maadili yetu ya kitanzania.

ila kumchukua na kumpa pesa kwa lengo la kwenda kumzagamua hilo ni kosa kwa maadili yetu
Mkuu.. busara ni matumizi ya akili katika kutoa maamuzi... Kama huna akili hizo ata ushinde kwenye nyumba za ibada bado hutakuwa nazo tu....
Nenda vijijini kaone wazee wa kimila wale.. jioni huwa wanalewa tu lkn wakiwa fit wanatoa maamuzi sahihi...
 
Mkuu.. busara ni matumizi ya akili katika kutoa maamuzi... Kama huna akili hizo ata ushinde kwenye nyumba za ibada bado hutakuwa nazo tu....
Nenda vijijini kaone wazee wa kimila wale.. jioni huwa wanalewa tu lkn wakiwa fit wanatoa maamuzi sahihi...
kulewa ni starehe ikiwa haumkeri mtu na wala haufanyi matendo ya ovyo

ukifanikiwa kudhjbiti starehe yako usilete kero kwa wengine/ na wala hauvunji maadili ya jamii yako hapo lazima utaonekana na unazo busara.

wazee wa mila wanapiga mbege, ulanzi, mnazi, wanzuki na pombe za aina kibao lakini je wananunua wanawake wanaojiuza au ayo matendo ambayo yanakazwa na jamii yao wanayafanya mbele za watu wengi ( watu wawili na kuendelea).

kama vile mitaa , hospital , mashuleni au hata eneo kama bar
 
😁😁😁 kumbe unaleta ushabiki sasa hapa sheikh hatuengelei ushabiki tunaongelea swala la uhalisia na ukweli.

sasa hapa itakuwa ngumu kunielewa na mimi itakuwa ngumu kukuelewa kwa sababu tuongea lugha mbili tofauti
Iendike tena shekhe bila kisa mafunzo cha wimbo wetu, andika katika namna elimishi bila ainisho hili, umetukwaza, kwa nini wimbo huu tu?
 
Iendike tena shekhe bila kisa mafunzo cha wimbo wetu, andika katika namna elimishi bila ainisho hili, umetukwaza, kwa nini wimbo huu tu?
sio wimbo huu tu wowote ule wa msanii yeyote yule utakao kuja nitaundikia.

sasa kama mutakasirika pia litakuwa sio kosa langu hilo ni kosa lenu
 
Kisekta unaitwa Curator. Yaani unaweza kuijadili kazi na concept ya sanaa in a way ya kumsaidia creator wa content ya sanaa kufanya vizuri zaidi.

Nimesoma kila neno na nimejiridhisha umeotendea haki video ya Zuwena.

Kwa ushauri wangu nadhani itakuwa busara wasanii wanapotoa video na filamu zao wawaalike critiquers kabla hawajazitoa ili waweze kushauri au kukosoa kazi zao. Hili linafanyika duniani kwa ufanisi mkubwa.

Comment yako ndio comment yangu...
 
Imechambuliwa na kuandikwa na Ally Nassor Px .

Tarehe 5 February 2023.

Sehemu ya kwanza kuipost ni hapa JF sehemu ya pili itakuwa ni Facebook na mwisho kabisa nitamalizia Twitter.

...........................................................


Video imetoka juzi Tarehe 3 mwezi wa pili mwaka 2023.

Saa 4 kamili asubuhi.

ikiwa imeongozwa na director ivan.

mpaka sasa tarehe 5 mwezi wa pili 2023 video hii ina jumla ya watazamaji
Milioni 2.4

nilichopenda kwenye video ya zuwena ni video ambayo inaonesha uhalisia wa kinachoimbwa na ningependa kuoana zaidi na zaidi video zenye uhalisia na kile kinachoimbwa inawezekana kikatutambulisha jamii ya watanzania kirahisi kwa jamii nyingine.

Twende moja kwa moja kwenye uchambuzi wa video yenyewe.

video ni kali sana kwa upande wangu naipa rate ya 8 / 10. kuna baadhi ya makosa ya ufundi yalionekana kwenye video lakini hauwezi kuyaona mpaka utulie ila mimi nataka nikuoneshe.

..........................................................
1. MMASAI WA BANDIA

Mwanzo wa video sekunde ya 33 ( 00:33).

anaonekana jamaa wenye asili ya kimasai akikimbiza punda wawili.

ila kama utakuwa makini utangundua kuwa yule sio Mmasai halisi. wakati mmasai halisi alikuwepo kwenye video alionekana alipiga gitaa mwanzo kabisa Sekunde ya 3 ( 00: 03).
View attachment 2506707

mmasai aliyekuwa akikimbiza punda alionekana wa kutengeneza ukitazama alikuwa kavaa soksi chini na buti la Timberland (rangi ya bagia ).

View attachment 2506684
...............................................................

2. MUHUSIKA MMOJA KUOENEKANA SEHEMU MBILI TOFAUTI.

Ukitazama video sekunde ya 46 ( 00: 46).

kuna mzee utamuona alikuwa anasoma urithi. na inajulikana siku zote mtu ambaye anapewa jukumu la kusoma urithi ni mtu wenye heshima zake na anaaminiwa sana.

Sasa ukitazama video ya zuwena utamuona yule mzee aliyekuwa anasoma hosia wa urithi.

aonekana akiwa bar anamtunza zuwena alivyokuwa anacheza juu ya meza dakika ya (1 : 40).

View attachment 2506687

View attachment 2506688
...............................................................

3. TATOO ZA DIAMOND NA KIPINI PUANI.

Inawezekana ni ngumu sana kumpiga diamond make up ambayo itaficha tattoo zake. ila inaonesha director alisahau pia ata kumwambia diamond atoe japo kile kipini chake pale puani mwanzo mpaka mwisho wa video diamond anaonekana na kipini puani.

kumbuka video imebeba uhalisia wa maisha ya watu wa kipato cha chini ni ngumu sana kumkuta mtu wa kipato cha chini ana tatoo mwilini na kipini puani.

View attachment 2506689
............................................................

4. MTU KUCHEKA KWENYE TUKIO LA KUSHTUA.

Ukitazama vizuri dakika ya ( 2: 14).

kipande ambacho diamond anaenda kumuokoa zuwena alivyokuwa anataka kubakwa.

kuna jamaa mmoja kati ya wale wabakaji wanne kuna jamaa kavaa koti jeusi na suruali nyeupe. wakati wenzake wameshituka mmoja anapandisha suruali fasta fasta yeye alikuwa anamtazama mwenzake anayepandisha suruali huku akicheka.

View attachment 2506691
..............................................................

5. MATANGAZO YA MAKAMPUNI MBALIMBALI .

Mwaka 2012 Ronaldinho Gaucho alifutiwa mkataba na company ya Cocacola baada ya kuonekana chupa za Pepsi kwenye mkutano wake na waandishi wa habari.

View attachment 2506692

kuonekana chupa ya soda ya Pepsi. ila habari za Ronaldinho tuachane nazo.

Kila mtu anajua kuwa Diamond ukiachana na kujishusisha na sekta ya muziki lakini pia ni Company ambassador wa company mbalimbali.

sasa sijajua kuwa diamond ana mkataba na kampuni mbalimbali zilizoonekana kwenye video yake.

Dakika ya (1:00) Yanaonekana madish mawili ya Azam Tv juu ya mabanda yanayouza nguo.

View attachment 2506693

Dakika ya ( 2: 06) linaonekana tangazo la TTCL na DOUBLEMINT
View attachment 2506697

Dakika ya ( 2: 10 ) Diamond anaonekana anandesha pikipiki ya kutoka company ya TOYO.
View attachment 2506698

Dakika ya ( 2: 12) hadi dakika ya 2: 22) akiwa kaingia kumuokoa zuwena na anatoka pia yanaoenaka maboksi ya company ya MSAFI, KASUKU na JUMBO

View attachment 2506701

Dakika ya ( 3: 33) akiwa bar anaimba kwa mbali yanaonekana mafriji ya Coca-cola wakati kila mtu anajua diamond ni Ambassador wa Pepsi.

View attachment 2506702
....................................

6. KUONEKANA KWA NEMBO YA SERENGETI LAGER.

Uwenda point hii isiwe na nguvu sana ila point hii ndio inaweza ukaipa nguvu zaidi point namba 5 kuonekana kwa matangazo mbalimbali ya makampuni mbalimbali.

ukitazama bar watu wote walikuwa wanakunywa bia ambazo zilikuwa hazina utambulisho wa nembo kuwa ni bia za aina gani na zinatokea kampuni gani.

hii yote ilikuwa kutoonesha nembo ya kampuni ambayo diamond ana ubalozi nayo.

ila dakika ya ( 3:50) kuna kosa lilifanyika kuna muhudumu anatembea na chupa za bia. kuna chupa mmoja inaaonekana na nembo la SERENGETI LAGER.

View attachment 2506703
_____________________________________


Lengo la kuandika uzi huu sio kukosoa na kuishusha hadhi video ya msanii husika ila ni kukumbusha uwepo umakini zaidi kwa waongozi ( Madirector).

Nadhani Msanii husika hana kosa katimiza wajibu wake kwa asilimia kubwa sana kaimba nyimbo kali lakini pia ka act vizuri sana kwenye video kwa maelekezo ya director.
Umetisha bro
 
Mkuu uko vizuri sana,umechambua Kwa ufasaha,umakini na usahihi Kwa asilimia kadhaa.Hongera kwako!

Ila hiyo ni Moja ya sanaa ya msanii natambua imefanywa na msanii makini,mwenye intelligencia kubwa sana kwenye sanaa yake.

Siyo kwamba hawajui walichokifanya! lahasha wanatambua kira kitu na wanajua Nini wananafanya.

Kwakuwa ni wasanii hivyo wanaweka na kausanii kidogo kwenye kazi zao Ili kuwapa nafasi watu kama ninyi Ili kuipa nafasi kazi Yao iweze kufuatiliwa na watu wengi zaidi (uwenda ndiyokitengo chako.!..utani tu)

Kwasababu wapo watu wataofuatialia jambo Baada yakusikia/kuona kasoro Fulani Kwa lengo la kukosoa mbele ya safari Yao,Lakini pia Kuna watu ambao wanafuatilia jambo Baada ya kisikia/kuona Uzuri wa kazi na lengo ni kupata ushaidi wakwenda kuongelea kubishania mbele ya safari.

Hivyo Dai ni mtu mjanja na mwenye akili kubwa sana,hivyo usishangae akawa anaitaji kuongeza Idadi ya watazamaji kupitia Kwa watu waaina zote(wakosoaji na wanaomkubari).

Lengo kuu la msanii ni kupata fedha Kwanjia ya sana yake mkuu.Hivyo Kuna uwezekano mkubwa wayeye wakujua Yale yanayo hitajika Dunia iliyoendelea katika kazi yake.
 
Hongera Sana mkuu kwa uchambuzi wako mzuri, hakika umeitendea Hali Sana.
 
Back
Top Bottom