LGE2024 Makosa Matatu ya Mdude Nyagali: Kujeruhi, Matusi na Kuvuruga Uchaguzi, Wakili Boniface Mwabukusi kumtetea

LGE2024 Makosa Matatu ya Mdude Nyagali: Kujeruhi, Matusi na Kuvuruga Uchaguzi, Wakili Boniface Mwabukusi kumtetea

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Haya ndiyo yatavunja heshima ya rais wa TLS, kukaa desk moja na wahuni ambao wanatakiwa kuchapwa bakora kwa utovu wa nidhamu, nashauri atume wakili mwingine!
Mhuni ni wewe unaetetea mafisadi na wezi wa mali za umma.
 
Binafsi huwa sioni mchango wa Mdude kwenye chama, ni mtu anaetaka kukaa kwenye akili za watu kwa matukio yasiyokua na umuhimu.

Nadhani hata uongozi wa chama pia hauoni umuhimu wake, zaidi ni yeye anaejishikiza kwenye shughuli za chama.

Ndio maana hata mawakili wa chama hawajataka kujisumbua kwenda kumtetea.
 
Binafsi huwa sioni mchango wa Mdude kwenye chama, ni mtu anaetaka kukaa kwenye akili za watu kwa matukio yasiyokua na umuhimu.

Nadhani hata uongozi wa chama pia hauoni umuhimu wake, zaidi ni yeye anaejishikiza kwenye shughuli za chama.

Ndio maana hata mawakili wa chama hawajataka kujisumbua kwenda kumtetea.
Ulijuaje? Uletewe picha Mbowe akiwa mahakamani ktk kesi ya Mdude?
 
Definition ya uhuni ni pana. Inawezekana na wewe ukaingia kundi hilo hilo
Ningelikuwa na mamlaka watu wa aina hii, wabovu wa adabu, adhabu yao ingekuwa bakora tu, maana wamechagua - utoto tundu - hawako kwenye ualifu wa kuhatarisha nchi kiasi labda watekwe ni viboko tu.
 
Imeelezwa kuwa kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mdude Nyagali Mdude anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Songwe anatuhumiwa kutenda makosa matatu (3) ikiwemo kujeruhi, kutoa lugha ya matusi na kuvuruga ratiba ya uchaguzi wa serikali za mitaa 2024

Hayo yameelezwa na Wakili wake Boniface Mwabukusi kupitia chapisho aliloweka kwenye mtandao wake binafsi wa kijamii wa X Novemba 24.2024 ambapo ameeleza kuwa yeye binafsi akiwa ameambatana na Mbunge wa zamani wa Mbozi (CHADEMA) Paschal Haonga na mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la Abdulkareem kwa pamoja wamefika kwenye kwenye kituo cha Polisi Itumba, Ileje anachoshikiliwa Mdude na kusimamia mahojiano yake

Amesema licha ya kwamba Jeshi la Polisi limeanza kumuhoji lakini Mdude yeye amegoma kutoa maelezo ya ziada kituoni hapo badala yake ametaka afikishwe Mahakamani ili akatolee huko maelezo hayo, jambo ambalo Wakili Mwabukusi amesema ni haki yake ya kisheria.
Kupitia chapisho hilo, Wakili Mwabukusi ambaye pia ni Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) ameendelea kufafanua kuwa makosa anayoshtakiwanayo mteja wake yanadhaminika hivyo waliomba apatiwe dhamana hiyo lakini hata hivyo jambo hilo liligonga mwamba kutokana na kile walichoelezwa kuwa maafisa wengine wa Polisi wanataka kumuhoji kutokana na makosa mengine anayodaiwa kuyatenda mkoani Mbeya

Kutokana na hilo, Wakili Mwabukusi ameahidi kurudi kituoni hapo leo, Jumatatu Novemba 25.2024 ili kuendelea kumsimamia mteja wake na kwamba dhamira ni kuona haki za kisheria na Kikatiba za Mdude Nyagali zinapatikana.
Huyu paka abakie huko huko maana uhuru wake wa kutoa maoni kageuza ni uhuru wa kutukana viongozi na kujeruhi watu.

Kichwa cha Mdude_Nyagali hakina akili
 
Back
Top Bottom