Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MAKALA YA MAMA MARIA NYERERE KUTIMIZA MIAKA 93 NA MAKOSA NDANI YA MAKALA
Kuna makala imewekwa mtandaoni kuhusu Mama Maria Nyerere kutimiza miaka 93 hii leo.
Makala hii imesheheni mengi katika maisha ya Mama Maria.
Nimeisoma na imenifurahisha na kunielimisha katika mengi ambayo sikuwa nayajua vyema.
Juu ya hayo yote makala hii imeruka sehemu muhimu sana katika maisha yake na kwa kweli si yake tu bali na ya mumewe Mwalimu Nyerere na historia ya TANU na pia kuandika mengine ambayo si ya kweli.
Makala hii inazungumza duka alilofungua Mama Maria Magomeni.
Mwandishi anaeleza duka hili kuwa duka lililokuwa linauza bidha kadhaa.
Hii si kweli Mama Maria alikuwa na duka dogo la kuuza mafuta ya taa.
Yako makosa mengi lakini hapa sitayazungumza tutizame hili hapo chini:
‘’In the mid 1950s, Mwalimu & his family were living at Magomeni Mapipa where they rented a small house.
This was after they had stayed in John Rupia's house at Mission Quarter, Kariakoo for one year.
This followed Mwalimu Nyerere's abrupt resignation as a teacher at St. Francis Pugu on March 22, 1955.
Mama Maria, to make ends meet, opened a small shop in their small house at Magomeni to sell sugar, soaps, salt, cooking oil etc.
She believed in living within her means and working hard for everything.
She was a rock to Mwalimu Nyerere's family.’’
Nimerekebisha machache katika historia ya Mama Maria Nyerere kwa kueleza historia yake kwa kutumia maelezo ya wale waliompokea Mwalimu alipofika Dar es Salaam mwaka wa 1952 ili historia muhimu ifahamike vizuri kwa faida ya kizazi hiki na kizazi kijacho:
"Napenda kueleza kitu kidogo katika historia ya Mama Maria Nyerere.
Katika akina mama wa mwanzo kufahamiana na Mama Maria Nyerere alikuwa Bi. Mwamvua bint Mrisho maarufu kwa jina la Mama Daisy.
Walifahamiana kwa kuwa Mama Daisy alikuwa mke wa Abdul Sykes na kama tujuavyo Mwalimu Nyerere baada ya kuacha kazi ya ualimu alikwenda kuishi nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu.
Hapa ndipo Mama Maria na Mama Daisy walipounga udugu.
Hii ilikuwa mwaka wa 1955.
Mama Daisy amenihadithia anasema baada ya miaka mingi kupita alikutana na Mama Maria Ukumbi wa Diamond Jubilee Mwalimu alipotoa hotuba kuwaaga Wazee wa Dar es Salaam.
Mama Maria alichukua fursa hii kuonana na kuzungumza na akina mama wa Dar-es-Salaam.
Mama Maria na Mama Daisy walikumbatiana kwa mapenzi Mama Maria akaieleza hadhira ile kuwa Mama Daisy na mumewe ndiyo waliowapokea yeye na mumewe Dar es Salaam.
Duka la mafuta ya taa la Mama Maria alilifungua Mtaa wa Mchikichi na Livingstone wakati wanaishi nyumbani kwa Abdul Sykes.
Akina mama ambao walikuwa jirani na duka hili walikuwa Bi. Chiku bint Said Kisusa ambae alikuwa anaishi mtaa huo wa Mchikichi kona na New Street (sasa Lumumba Avenue).
Duka la mafuta ya taa la Magomeni Mapipa Mama Maria alilifungua nyumbani kwa Ali Msham Mtaa wa Jaribu.
Ali Msham alikuwa amefungua tawi la TANU nyumbani kwake na Mwalimu alipohamia Maduka Sita Magomeni ikabidi Mama Maria awe anakwenda Kariakoo kila siku.
Ali Msham ndipo alipotoa nafasi nyumbani kwake duka lihamishiwe hapo ili kumpumzisha Mama Maria na shida ya kuparamia mabasi na watoto asubuhi kwenda Kariakoo.
Duka la mafuta ya taa la Mama Maria la hapo Maduka Sita lilikuja baadae.
Tunamtakia Mama Maria umri tawil na afya njema."
Picha hiyo hapo chini ni nyumba ya Mwalimu Maduka Sita Magomeni na huyo anaeingia ndani ya nyumba hiyo ni yeye mwenyewe.
Angalia bango juu ya nyumba linalotangaza duka la mafuta ya taa.