Makosa ndani ya Makala ya Mama Maria Nyerere Kutimiza Miaka 93

MAKALA YA MAMA MARIA NYERERE KUTIMIZA MIAKA 93 NA MAKOSA NDANI YA MAKALA

Kuna makala imewekwa mtandaoni kuhusu Mama Maria Nyerere kutimiza miaka 93 hii leo.

Makala hii imesheheni mengi katika maisha ya Mama Maria.

Nimeisoma na imenifurahisha na kunielimisha katika mengi ambayo sikuwa nayajua vyema.

Juu ya hayo yote makala hii imeruka sehemu muhimu sana katika maisha yake na kwa kweli si yake tu bali na ya mumewe Mwalimu Nyerere na historia ya TANU na pia kuandika mengine ambayo si ya kweli.

Makala hii inazungumza duka alilofungua Mama Maria Magomeni.

Mwandishi anaeleza duka hili kuwa dula lililokuwa linauza bidha kadhaa.

Hii si kweli Mama Maria alikuwa na duka dogo la kuuza mafuta ya taa.

Yako makosa mengi lakini hapa sitayazungumza tutizame hili hapo chini:

‘’In the mid 1950s, Mwalimu & his family were living at Magomeni Mapipa where they rented a small house.

This was after they had stayed in John Rupia's house at Mission Quarter, Kariakoo for one year.

This followed Mwalimu Nyerere's abrupt resignation as a teacher at St. Francis Pugu on March 22, 1955.

Mama Maria, to make ends meet, opened a small shop in their small house at Magomeni to sell sugar, soaps, salt, cooking oil etc.

She believed in living within her means and working hard for everything.

She was a rock to Mwalimu Nyerere's family.’’

Nimerekebisha machache katika historia ya Mama Maria Nyerere kwa kueleza historia yake kwa kutumia maelezo ya wale waliompokea Mwalimu alipofika Dar es Salaam mwaka wa 1952 ili historia muhimu ifahamike vizuri kwa faida ya kizazi hiki na kizazi kijacho:

"Napenda kueleza kitu kidogo katika historia ya Mama Maria Nyerere.

Katika akina mama wa mwanzo kufahamiana na Mama Maria Nyerere alikuwa Bi. Mwamvua bint Mrisho maarufu kwa jina la Mama Daisy.

Walifahamiana kwa kuwa Mama Daisy alikuwa mke wa Abdul Sykes na kama tujuavyo Mwalimu Nyerere baada ya kuacha kazi ya ualimu alikwenda kuishi nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu.

Hapa ndipo Mama Maria na Mama Daisy walipounga udugu.

Hii ilikuwa mwaka wa 1955.

Mama Daisy amenihadithia anasema baada ya miaka mingi kupita alikutana na Mama Maria Ukumbi wa Diamond Jubilee Mwalimu alipotoa hotuba kuwaaga Wazee wa Dar es Salaam.

Mama Maria alichukua fursa hii kuonana na kuzungumza na akina mama wa Dar-es-Salaam.

Mama Maria na Mama Daisy walikumbatiana kwa mapenzi Mama Maria akaieleza hadhira ile kuwa Mama Daisy na mumewe ndiyo waliowapokea yeye na mumewe Dar es Salaam.

Duka la mafuta ya taa la Mama Maria alilifungua Mtaa wa Mchikichi na Livingstone wakati wanaishi nyumbani kwa Abdul Sykes.

Akina mama ambao walikuwa jirani na duka hili walikuwa Bi. Chiku bint Said Kisusa ambae alikuwa anaishi mtaa huo wa Mchikichi kona na New Street (sasa Lumumba Avenue).

Duka la mafuta ya taa la Magomeni Mapipa Mama Maria alilifungua nyumbani kwa Ali Msham Mtaa wa Jaribu.

Ali Msham alikuwa amefungua tawi la TANU nyumbani kwake na Mwalimu alipohamia Maduka Sita Magomeni ikabidi Mama Maria awe anakwenda Kariakoo kila siku.

Ali Msham ndipo alipotoa nafasi nyumbani kwake duka lihamishiwe hapo ili kumpumzisha Mama Maria na shida ya kuparamia mabasi na watoto asubuhi kwenda Kariakoo.

Duka la mafuta ya taa la Mama Maria la hapo Maduka Sita lilikuja baadae.

Tunamtakia Mama Maria umri tawil na afya njema."

Picha hiyo hapo chini ni nyumba ya Mwalimu Maduka Sita Magomeni na huyo anaeingia ndani ya nyumba hiyo ni yeye mwenyewe.

Angalia bango juu ya nyumba linalotangaza duka la mafuta ya taa.

323194726_553729993036637_5201274679647759998_n.jpg
Unajua sana hongera Baba yetu 🙏🙏🙏
 
Alipokelewa na kuishi nyumbani kwa Abdul Sykes .........

Alikuwa na marafiki kina mama wa ukoo maarufu Kariakoo .........

Abdul Sykes na Ally Sykes walitoa mali na kila kitu kumsaidia Nyerere apate Uhuru.

Huyu babu wa kiislam ni aina ya watu ambao ambao akikusaidia UTAJUTA
 
Kwa vile katika Makala ile Sykes hakuandikwa
Naam,
Mtafiti yeyote atakae jaribu kumkwepa Abdul Sykes katika historia ya TAA, TANU na Mwalim Nyerere atakuwa ameacha sehemu kubwa na muhimu ya historia ya uhuru wa Tanganyika.

Wako waliojaribu kufanya hivyo na ndiyo leo unaniona niko hapa naisomesha upya historia ya kupigania uhuru wa Tangnayika kwa makala na picha.
 
Mose...
Kanuni za uandishi ni kuweka dot 3 tu ...
 
Fundi...
Nimepokea taarifa kuwa Mama Maria pamoja na mafuta ya taa alikuwa akiuza Coca-Cola:

"SALESMAN ALIEKUWA ANAMPELEKEA SODA ZA COCA-COLA NI MAREHEMU AMAL BAFADHIL. NI SHEMEJI YAO KINA MOHAMED BAHADORY WA MKUNGUNI STREET."

Ukoo wa Bahadory ni maarufu Dar es Salaam ya miaka ile.

Hapana sababu ya sisi kuvutana na historia ya Abdul Sykes kama unaikubali au la.

Kuwa kulikuwa na wengine ni kweli lakini hawakutajwa popote hadi pale mimi nilipowataja ndani ya kitabu cha Abdul Sykes.
hah
Watu hushangaa ninaandika TANU kadi no. 5 ni ya Denis Phombeah Mnyasa wa Nyasaland, no. 6 Dome Okochi Budohi Mluya kutoka Kenya kisha nikaweka na picha nimepiga na yeye Nairobi 1972 nikiwa na umri wa miaka 20.

Naona hukupenda mimi kujumuishwa na Dr. Salim Ahmed Salim na Brig. Hashim Mbita kuwa ni wenye maktaba kubwa iliyosheheni taarifa za Mwalimu.

Mimi hili pia limenishtusha sana.
Unasema ni la kwangu.

Hapana hili si la kwangu hili ni la taifa lililopoteza historia yake sasa wanaikusanyq upya.

Prof. Shivji anatoka Kigoda Cha Mwalimu Nyerere.

CCM wameniomba niwapatie baadhi ya Nyaraka za Sykes.

Mwakilishi wa Ford Foundation aliwasilana na mimi ili nitoe msaada kwa Nyerere Foundation.

Kuna mambo hujuzuia kusema.

Nina nyaraka za Mwalimu yeye hana na alipata miaka mingi iliyopita kuziomba kwa Ally Sykes.

Baadhi ya nyaraka hizi nimewapa watafiti waliozihitaji na baadhi zipo Library of Congress, Washington DC na vyuo vingi Marekani.

Unajua katika miaka ya 1980 Mwakilishi wa Library of Congress Tanzania alikuwa Ahmed Rashaad Ali.

Mimi huyu ni baba yangu.
Nadhani umenielewa.

Mimi sina kawaida ya kumuita mtu muongo wala kumtukana mtu au kumkejeli mtu katika mnakasha.

Humchukulia kuwa hajui na wajibu wangu ni kumfunza na ikiwa hataki hapana ugomvi.

Nakuwekea picha ya mmoja wa watoto wa Mzee Bahdoury - Ismail ''Gigi'' Bahdoury.

Hili jina la Gigi ni kwa ajili alikuwa na kipaji kikubwa sana cha kucheza mpira katika vijana wa Dar es Salaam.

Gigi lilikuwa jina la mchezaji wa Italy Luigi ''Gigi' Riva katika miaka ya 1960s.

View attachment 2465812
Ismail ''Gigi' Bahdoury Muscat 1999.

View attachment 2465820
Kushoto: Ahmed Rashaad Ali, Dr. Harith Ghassany na Mwandishi

View attachment 2465823
Library of Congress, Washington DC
Sasa kama alikuwa anauza soda kwa nini asiuze vitu vingine? Ndivyo ilivyokuwa maduka yetu ya mtaani wakati ule.
Hayo ya wakina Salim Ahmed Salim, Shivji na Mbita nimekuachia wewe kwa sababu hakuna hata mmoja wao ni historian. Kuwa na vitabu vingi au kuwa librarian hakukufanyi kuwa authority.

Unasema huna kawaida ya kumuita mtu muongo lakini maneno yako kuhusu hizi habari za duka la mama Maria ilikuwa inamuonyesha kuwa yeye ni muongo. Kumuita mtu muongo sio lazima utumie neno muongo.
Asante kwa picha zako pamoja na taarifa kuwa Bwana Rashaad Ali ni mzazi wako. Ni jambo jema.

Amandla...
 
MAKALA YA MAMA MARIA NYERERE KUTIMIZA MIAKA 93 NA MAKOSA NDANI YA MAKALA

Kuna makala imewekwa mtandaoni kuhusu Mama Maria Nyerere kutimiza miaka 93 hii leo.

Makala hii imesheheni mengi katika maisha ya Mama Maria.

Nimeisoma na imenifurahisha na kunielimisha katika mengi ambayo sikuwa nayajua vyema.

Juu ya hayo yote makala hii imeruka sehemu muhimu sana katika maisha yake na kwa kweli si yake tu bali na ya mumewe Mwalimu Nyerere na historia ya TANU na pia kuandika mengine ambayo si ya kweli.

Makala hii inazungumza duka alilofungua Mama Maria Magomeni.

Mwandishi anaeleza duka hili kuwa dula lililokuwa linauza bidha kadhaa.

Hii si kweli Mama Maria alikuwa na duka dogo la kuuza mafuta ya taa.

Yako makosa mengi lakini hapa sitayazungumza tutizame hili hapo chini:

‘’In the mid 1950s, Mwalimu & his family were living at Magomeni Mapipa where they rented a small house.

This was after they had stayed in John Rupia's house at Mission Quarter, Kariakoo for one year.

This followed Mwalimu Nyerere's abrupt resignation as a teacher at St. Francis Pugu on March 22, 1955.

Mama Maria, to make ends meet, opened a small shop in their small house at Magomeni to sell sugar, soaps, salt, cooking oil etc.

She believed in living within her means and working hard for everything.

She was a rock to Mwalimu Nyerere's family.’’

Nimerekebisha machache katika historia ya Mama Maria Nyerere kwa kueleza historia yake kwa kutumia maelezo ya wale waliompokea Mwalimu alipofika Dar es Salaam mwaka wa 1952 ili historia muhimu ifahamike vizuri kwa faida ya kizazi hiki na kizazi kijacho:

"Napenda kueleza kitu kidogo katika historia ya Mama Maria Nyerere.

Katika akina mama wa mwanzo kufahamiana na Mama Maria Nyerere alikuwa Bi. Mwamvua bint Mrisho maarufu kwa jina la Mama Daisy.

Walifahamiana kwa kuwa Mama Daisy alikuwa mke wa Abdul Sykes na kama tujuavyo Mwalimu Nyerere baada ya kuacha kazi ya ualimu alikwenda kuishi nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu.

Hapa ndipo Mama Maria na Mama Daisy walipounga udugu.

Hii ilikuwa mwaka wa 1955.

Mama Daisy amenihadithia anasema baada ya miaka mingi kupita alikutana na Mama Maria Ukumbi wa Diamond Jubilee Mwalimu alipotoa hotuba kuwaaga Wazee wa Dar es Salaam.

Mama Maria alichukua fursa hii kuonana na kuzungumza na akina mama wa Dar-es-Salaam.

Mama Maria na Mama Daisy walikumbatiana kwa mapenzi Mama Maria akaieleza hadhira ile kuwa Mama Daisy na mumewe ndiyo waliowapokea yeye na mumewe Dar es Salaam.

Duka la mafuta ya taa la Mama Maria alilifungua Mtaa wa Mchikichi na Livingstone wakati wanaishi nyumbani kwa Abdul Sykes.

Akina mama ambao walikuwa jirani na duka hili walikuwa Bi. Chiku bint Said Kisusa ambae alikuwa anaishi mtaa huo wa Mchikichi kona na New Street (sasa Lumumba Avenue).

Duka la mafuta ya taa la Magomeni Mapipa Mama Maria alilifungua nyumbani kwa Ali Msham Mtaa wa Jaribu.

Ali Msham alikuwa amefungua tawi la TANU nyumbani kwake na Mwalimu alipohamia Maduka Sita Magomeni ikabidi Mama Maria awe anakwenda Kariakoo kila siku.

Ali Msham ndipo alipotoa nafasi nyumbani kwake duka lihamishiwe hapo ili kumpumzisha Mama Maria na shida ya kuparamia mabasi na watoto asubuhi kwenda Kariakoo.

Duka la mafuta ya taa la Mama Maria la hapo Maduka Sita lilikuja baadae.

Tunamtakia Mama Maria umri tawil na afya njema."

Picha hiyo hapo chini ni nyumba ya Mwalimu Maduka Sita Magomeni na huyo anaeingia ndani ya nyumba hiyo ni yeye mwenyewe.

Angalia bango juu ya nyumba linalotangaza duka la mafuta ya taa.

323194726_553729993036637_5201274679647759998_n.jpg
Jazakallah Mzee kwa masahihisho🙏
 
Sasa kama alikuwa anauza soda kwa nini asiuze vitu vingine? Ndivyo ilivyokuwa maduka yetu ya mtaani wakati ule.
Hayo ya wakina Salim Ahmed Salim, Shivji na Mbita nimekuachia wewe kwa sababu hakuna hata mmoja wao ni historian. Kuwa na vitabu vingi au kuwa librarian hakukufanyi kuwa authority.

Unasema huna kawaida ya kumuita mtu muongo lakini maneno yako kuhusu hizi habari za duka la mama Maria ilikuwa inamuonyesha kuwa yeye ni muongo. Kumuita mtu muongo sio lazima utumie neno muongo.
Asante kwa picha zako pamoja na taarifa kuwa Bwana Rashaad Ali ni mzazi wako. Ni jambo jema.

Amandla...
Fundi...
Tumenufaika na taarifa kuwa Mama Maria pamoja na mafuta ya taa alikuwa anauza na Coca-Cola na jina la mtu aliyekuwa akimpelekea nimetajiwa.

Hili la Shvji kama nilivyokwisha kusema si lake.

Yeye alikuwa Mwenyekiti wa Kigoda Cha Mwalimu Nyerere taasisi ya taifa la Tanzania.

Niliwapa baadhi ya Nyaraka za Sykes na wakaniandikia kunishukuru.

Nyerere Foundation unawajua halikadhalika naamini unawajua Ford Foundation.

Labda usichokijua ni uhisuano wangu na taasisi hizi mbili.

Kigoda Cha Mwalimu na mimi tulikuwa karibu kidogo na licha ya nyaraka tumebadilishana fikra.

Nyaraka nilizowapa walikuwa wakizionyesha hadharani katika shughuli zao nyingi.
 
Hizo kanuni aliweka Mungu?

Hazibadiliki
Hizo kanuni aliweka Mungu?

Hazibadiliki
Mose...
Hapana hakuweka Mungu.
Zimewekwa na binadamu na wakifundisha shule.

Mathalan mwisho wa sentensi unaweka nukta.
Mwanzo wa sentensi unaanza na herufi kubwa.

Kwa kawaida sheria hizi hazibadiliki.

Fikra yangu nilidhani kuwa hujui nikaona nikifahamishe ili iwe unajua na hivyo kuongoza elimu yako.

Bahati mbaya inaelekea umeghadhibika kusahihishwa.
Niwie radhi.
 
Naam,
Mtafiti yeyote atakae jaribu kumkwepa Abdul Sykes katika historia ya TAA, TANU na Mwalim Nyerere atakuwa ameacha sehemu kubwa na muhimu ya historia ya uhuru wa Tanganyika.

Wako waliojaribu kufanya hivyo na ndiyo leo unaniona niko hapa naisomesha upya historia ya kupigania uhuru wa Tangnayika kwa makala na picha.
Una matatizo mzee mwenzangu
 
Una matatizo mzee mwenzangu
Nafungua uzi mpya wa Sykes kuna mtu ameniuliza swali na wewe umenikejeli kuwa nina matatizo.

Ungeweza tu kueleza utakacho kiungwana bila ya kunitusi.

Ingia hapo chini tafadhali:

Mohammed, una kawaida ya kutaka kuaminiwa hata kama ulichokiandika kina mashaka. Kwa vile unaamini kuwa hamna mtu mwingine anayeijua historia ya Nyerere kuliko wewe basi tu akikataa kukubaliana na kila unachosema unaona ana kuchukia. Mimi nimekupinga kutokana na kile ambacho wewe mwenyewe umekiweka kama ushahidi kuwa Mama Maria alikuwa anafanya biashara ya mafuta ya taa. Mimi sipingi kuwa alikuwa anafanya biashara hiyo la hasha. Ninachopinga ni wewe kumpinga muandishi mwenzako ambae alisema alikuwa anauza vitu vingi kidogo, ukikazania kuwa alikuwa anauza mafuta peke yake. Lakini ukiangalia poster zilizo nje ya hilo duka tunaona zinatangaza Coca-Cola na vitu vingine. Na hii ilikuwa ni kawaida na inaendelea mpaka sasa. Ni wafanyabiashara wachache sana wanaoweza kuspecialise kwenye kitu kimoja.

Umepinga pia kuwa hakuishi kwenye nyumba ya Rupia bali aliishi kwa wakina Sykes. Hili nalo unali complicate bila sababu. Inawezekana kabisa kuwa Mwalimu alipoacha kazi alihamia kwa Sykes. Lakini vile vile kuna uwezekano kuwa baada ya hapo alihamia kwenye mojawapo ya nyumba za Rupia ambae inajulikana kuwa alikuwa ana nyumba nyingi tu.

Unatuelezea urafiki wa mke wake Sykes na mama Maria kana kwamba alikuwa rafiki yake pekee. Mama Maria ni mkatoliki na bila shaka alikuwa na marafiki wengi zaidi ya mama Daisy.

Mimi siku zote nakuambia kuwa nafurahia simulizi zako za wazee wako wa Gerezani na ninaamini ni mchango mzuri katika historia yako. Ninachokupinga ni pale unapotaka kuifanya hiyo ndio historia pekee inayotakiwa kupewa uzito.

Amandla...
Hiyo makala yake anayosema anasahihisha makosa ya historia ya mama Maria Nyerere, ina makosa chungu nzima.
 
Kwa vile katika Makala ile Sykes hakuandikwa
Kolola,
Kipande muhimu kimerukwa kukosa kutaja kuwa Mwalimu alikaa kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley.

Akiwa hapo Mama Maria akafungua duka la mafuta ya taa Mtaa wa Mchikichi.

Haikuelezwa kuwa walipohamia Magomeni Maduka Sita Mama Maria akapewa nafasi ya kuweka duka lake la mafuta nyumbani kwa Ali Msham.

Hii ni historia ya wazee wangu na ni jukumu langu kuhakikisha kuwa inahifadhiwa sawasawa.
 
Hivi unadhani kila kitu lazima kiandikwe? Unajua Nyerere aliolea kwa nani akiwa anafundisha Tabora? Huyo Sykes wako unamtukuza hadi unaboa
 
Back
Top Bottom