Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #61
Badee unauliza swali nyeti sana.Mzee...
Vijana wako wanashangaa eti kwanini nyerer hakitaja ukweli wa historia yake.
Hivi mwenye dhamira unajiuliza kwnini anadhamiri tena?
Mzee una kipaji na elimu ya kuwavumilia Waefeso hawa, ila sisi tunawaona wasumbufu kama Walawi wa Musa
Katika kitabu cha Abdul Sykes nimeeleza matatizo yaliyotokea 1962 pale TANU kwa ushauri wa Mwalimu Kihere ilipoamua kuandika historia yake.
Katika mazungumzo haya alikuwapo Dossa Aziz na Nyerere.
Ikaamuliwa Abdul aandike historia hiyo na msaidizi wake akawa Dr. Wilbard Kleruu.
Abdul akatumia nyaraka alizokuwanazo toka 1929 baba yake alipokuwa mmoja wa waasisi wa African Association kama Secretary na nyingine yeye alipochukua uongozi wa TAA 1950 kama Secretary na Dr. Vedasto Kyaruzi akiwa President.
Ikawa historia hii anaiandika kutoka yale ambayo yeye kapokea kutoka kwa baba yake ambayo yalikuwa katika mswada wa kitabu na yake mwenyewe akiwa Burma Vita Kuu ya Pili (1939 - 1945) walipoamua kuunda TANU kupigania uhuru wa Tanganyika.
Inaelekea historia hii haikuweza kukubalika kama ndiyo historia ya TANU na harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Pakawa na sintofahamu Abdul akajitoa akabakia Dr. Kleruu katika uandishi ule wa historia ya chama cha TANU.
Mswada huu haukuchapwa ukabakia ofisi ya TANU hadi ulipoibiwa na kuchapwa kitabu mwaka wa 1971 jina la mwandishi likiwa Abubakar Ulotu.
Hili neno ''kuibiwa,'' alilikataa mhariri wa kitabu cha Abdul Sykes alinitahadharisha kuwa tunaweza kuingia matatani.
TANU ikaja juu kuhusu kitabu hiki kakini walilalamika kimya kimya.
Mwaka wa 1977 ndipo Chuo Cha CCM Kivukoni kikaandika historia nyingine ya TANU.
Ukivisoma vitabu hivi utasema vyote vimeandikwa na mtu mmoja.
Vitabu vyote hivi viwili Abdul Sykes hayumo na wazalendo wengine wengi pia.
Matokeo ya haya ni kuwa pakawa hakuna historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika hadi kilipotoka kitabu cha Abdul Sykes 1998.
Kitabu hiki kiliwashtua watu wengi mmojawapo Prof. Haroub Othman.
Vyuo Vikuu Marekani na Ulaya wakakipenda kwani kilikuwa kitabu kilichokuja na elimu mpya.
Prof. Haroub akaenda kwa Mwalimu kutaka kusadikisha historia ya Nyerere na Abdul Sykes kama vile nilivyoandika ndivyo kweli ilivyokuwa.
Lakini Prof. Haroub kabla hajakwenda kwa Mwalimu alizungumza na rafiki yake Abdul Sykes Ahmed Rashaad Ali kutafuta ithibati ya kile nilichoandika ambayo aliipata.
Prof. alikuwa na hoja kuwa Mwalimu na yeye aandike ili upande wake wa historia hii ufahamike vinginevyo historia yake itaingia doa.
Kulikuwa na mambo makubwa mawili ambayo Prof. Haroub alitaka Mwalimu ayaweke wazi.
Kwanza mchango wa Ukoo wa Sykes katika kupigania uhuru wa Tanganyika na pili uhusiano wa Nyerere na Waislam kabla na baada ya uhuru.
Bahati mbaya Mwalimu alikuwa mgonjwa hana nguvu tena za kunyanyua kalamu kuandika.
Yapo mengi lakini nakuomba utosheke na haya.
Nakala ya toleo la kwanza la kitabu kilichochapwa na Minerva Press, London 1998
Mwalimu Kihere
Kushoto Prof. Haroub Othman, Ahmed Rashaad Ali na Sheikh Ahmed Islam picha hii niliwapiga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tulikuwa tunakwenda Jeddah na Air Tanzania Corporation (ATC) kwa ajili ya Umra 1997