Ukweli kuwa Mama Maria Nyerere aliuza mafuta ya taa tu au na vitu vingine unaweza kupatikana kwa kumuuliza muhusika mwenyewe.Na wewe vile vile unaniwekea maneno kinywani. Hakuna mahali nilipopinga historia ya Abdul Sykes au Sykes mwingine yeyote kupewa uzito. Ninachopinga ni wewe kufanya hao ndio nzima ya mapambano yetu ya uhuru. Hawakuwa peke yao kama vile Nyerere hakuwa peke yake.
Historia ipi hiyo ya Mama Maria inayosema marafiki zake walikuwa ni hao wakina mama wa kiislamu peke yake. Kwa akili za kawaida tu zingesema kuwa huyu mama ni lazima alikuwa na marafiki zake ambao walikuwa ni wakristo wenzake na sio waislamu peke yao.
Sikupingi kuwa Nyerere alikaa katika nyumba ya wakina Sykes. Lakini kwa vile haujasema alikaa kwa muda gani, kuna uwezekano kuwa baada ya hapo alihamia kwenye mojawapo ya nyumba za John Rupia.
Hilo la wakina Issa Shivji, Dr. Salim Ahmed na Hashim Mbita ni la kwako. Lakini kwa vile najua Mwalimu mwenyewe alikuwa na vitabu mpaka nyumba yake ilikuwa haitoshi nasita kuamini kuwa ulikuwa na kumbukumbu za historia yake kuliko yeye mwenyewe.
Kwa vile wewe binafsi haujawahi kusikia kuwa mama Maria alikuwa anauza soda pamoja na mafuta ya taa hakumfanyi aliyesema hivyo kuwa muongo. Picha uliyoweka inaonyesha kuwa kuna uwezekano kuwa ni kweli. Kwa vile haujaweka chanzo ya hayo madai, ni vigumu kujua kama mwandishi aliambiwa hivyo na mama Maria mwenyewe.
Amandla...
Huyu mama bado yupo hai, na anafikika kwa njia yoyote ambayo mtaona ni sawia kwenu na yeye.