Fundi...
Nimepokea taarifa kuwa Mama Maria pamoja na mafuta ya taa alikuwa akiuza Coca-Cola:
"SALESMAN ALIEKUWA ANAMPELEKEA SODA ZA COCA-COLA NI MAREHEMU AMAL BAFADHIL. NI SHEMEJI YAO KINA MOHAMED BAHADORY WA MKUNGUNI STREET."
Ukoo wa Bahadory ni maarufu Dar es Salaam ya miaka ile.
Hapana sababu ya sisi kuvutana na historia ya Abdul Sykes kama unaikubali au la.
Kuwa kulikuwa na wengine ni kweli lakini hawakutajwa popote hadi pale mimi nilipowataja ndani ya kitabu cha Abdul Sykes.
Watu hushangaa ninaandika TANU kadi no. 5 ni ya Denis Phombeah Mnyasa wa Nyasaland, no. 6 Dome Okochi Budohi Mluya kutoka Kenya kisha nikaweka na picha nimepiga na yeye Nairobi 1972 nikiwa na umri wa miaka 20.
Naona hukupenda mimi kujumuishwa na Dr. Salim Ahmed Salim na Brig. Hashim Mbita kuwa ni wenye maktaba kubwa iliyosheheni taarifa za Mwalimu.
Mimi hili pia limenishtusha sana.
Unasema ni la kwangu.
Hapana hili si la kwangu hili ni la taifa lililopoteza historia yake sasa wanaikusanyq upya.
Prof. Shivji anatoka Kigoda Cha Mwalimu Nyerere.
CCM wameniomba niwapatie baadhi ya Nyaraka za Sykes.
Mwakilishi wa Ford Foundation aliwasilana na mimi ili nitoe msaada kwa Nyerere Foundation.
Kuna mambo hujuzuia kusema.
Nina nyaraka za Mwalimu yeye hana na alipata miaka mingi iliyopita kuziomba kwa Ally Sykes.
Baadhi ya nyaraka hizi nimewapa watafiti waliozihitaji na baadhi zipo Library of Congress, Washington DC na vyuo vingi Marekani.
Unajua katika miaka ya 1980 Mwakilishi wa Library of Congress Tanzania alikuwa Ahmed Rashaad Ali.
Mimi huyu ni baba yangu.
Nadhani umenielewa.
Mimi sina kawaida ya kumuita mtu muongo wala kumtukana mtu au kumkejeli mtu katika mnakasha.
Humchukulia kuwa hajui na wajibu wangu ni kumfunza na ikiwa hataki hapana ugomvi.
Nakuwekea picha ya mmoja wa watoto wa Mzee Bahdoury - Ismail ''Gigi'' Bahdoury.
Hili jina la Gigi ni kwa ajili alikuwa na kipaji kikubwa sana cha kucheza mpira katika vijana wa Dar es Salaam.
Gigi lilikuwa jina la mchezaji wa Italy Luigi ''Gigi' Riva katika miaka ya 1960s.
View attachment 2465812
Ismail ''Gigi' Bahdoury Muscat 1999.
View attachment 2465820
Kushoto: Ahmed Rashaad Ali, Dr. Harith Ghassany na Mwandishi
View attachment 2465823
Library of Congress, Washington DC