Fundi...
Unaghadhibika.
Hakuna sababu ya kutumia lugha kali za "mazuzu."
Mimi nimeeleza safari ya Mwalimu ilivyokuwa.
Ikiwa hutaki basi hatuna sababu ya kugombana.
Mipango yote ya safari ilikuwa ikipangwa nyumbani kwa Abdul Sykes ambako Nyerere alikuwa akitoka Pugu kuja mjini anafikia.
Mwalimu hakuchanja "vaccination" kwa hofu ya hujuma za Waingereza.
Kazi hii Abdul alimkabidhi mdogo wake Abbas.
Kweli unaweza kufananisha historia hii na...
Ipo tofauti kubwa.
Kulia Haruna Taratibu, Saadan Abdu Kandoro, Julius Nyerere, Sheikh Mohamed Ramia na Iddi Faiz Mafungo, Dodoma Train Station 1950s
View attachment 2468827
Kushoto: Rashid Sisso, Robert Makange, Zuberi Mtemvu, Iddi Faiz Mafungo, Julius Nyerere, John Rupia, Titi Mohamed wanamsindikiza Nyerere uwanja wa ndege safari ya kwanza UNO 1955
View attachment 2468830
Kulia: Chiku bint Said Kikusa, Titi Mohamed na Kulia ni Tatu bint Mzee na kati ni wanamsindikiza Julius Nyerere safari ya kwanza UNO 1955