Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #141
Mama...Kimsingi uliamua tu kukosoa uonekane wewe ndo unajua kuliko hao waandishi wengine kwa bahati nzuri ukafeli vibaya kusudio lako. Siku nyingine kosoa ukiwa na uhakika.
Hapana sijafeli popote.
Nimeshaeleza mara kadhaa kuwa biashara ya Mama Maria iliyokuwa inafahamika duka liko Mtaa wa Mchikichi kisha duka liko nyumbani kwa Ali Msham ilikuwa ni kuuza mafuta ya taa.
Hata kitabu cha Nyerere (2020) kinaeleza hivyo.
Haya ya kuwa alikuwa anauza na Coca-Cola tumeyajua hivi tuko katika mjadala huu.
Unakusudia niwe na uhakika upi zaidi ya huo hapo juu?
Wewe ulikuwa unaijua historia hii ya Mama Maria niliyokuwekeeni hapa?