Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #101
Fundi...Kujisifu na kusifiwa ni vitu viwili tofauti. Kuulizwa maswali na mtafiti ni jambo la kawaida. Wewe ukitembelewa na msomi basi unaamini mara moja kuwa ni kwa sababu wewe ni authority pekee katika field yako. Watafiti makini huwa wanakuwa na sources nyingi na sio kila source wanaitumia au kuikubali.
Mimi ungesema umetafiti sana kuhusu mgogoro wa tawi la EAMWS lililokuwa Tanzania ningekuelewa ingawa nisingekubaliana nawe.
Ytafiti wowote unaegemea upande mmoja ndio maana unakuwa kama si utafiti bali ni simulizi. Ndio maana una kawaida ya kucherry pick na ku insinuate mambo bila kutoa ushahidi kamili ili tu kujenga hoja yako ya kupigania dini yako. Mfano ni duka la Mama Nyerere. Mtafiti makini yeyote angehoji uwezekano mama Maria kutegemea uuzaji wa mafuta ya taa peke yake. Wewe badala ya kuangalia ile picha kama mtafiti uliiangalia Kama ushahidi wa simulizi za wazee wako. Huo sio utafiti.
Ukibanwa unasema ulisoma nyaraka zilizoandikwa na hao unaowaita ndugu zako. Hauwezi kuzungumzia historia ya EAMWS bila kuwazungumzia mabohora, makhoja na maahmaddiya hata kama haukubaliani na imani yao.
Amandla....
Ahsante sana.