Mnachihangu
JF-Expert Member
- Oct 22, 2022
- 890
- 1,022
Huyu anachuki sana na nyerere na ukristo kwa ujumlaKwanini unadhani kuwa hata angeifahamu historia ya Nyerere kuwekewa sumu asingeiandika?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyu anachuki sana na nyerere na ukristo kwa ujumlaKwanini unadhani kuwa hata angeifahamu historia ya Nyerere kuwekewa sumu asingeiandika?
Champ...Mzee Mohamed Said ulikuwa na miaka 10 mwaka 1962. Kila kitu unachoandika ni kwa kusimuliwa. Katika muktadha huo wewe sio source ya kuaminika kwasababu kwanza uko biased kwenye dini yako lakini pili maelezo yako asilimia kubwa umeyatoa kwa waislamu wenzio ambao mwalimu aliwaweka kando kwasababu walikuwa weupe kichwani.
Kila mahali hutaki kutambua kwamba John Rupia alikuwa na mchango mkubwa sana unalazimisha masimulizi ya Sykes ndio yawe standard. Mimi namuona Sykes ni mtu mwenye wivu baada ya kuwekwa pembeni na mwalimu wakati anaijenga nchi.
Nyerere alifanya akili sana kuwakataa hao wazee wa kiislamu maana nia yao ilikuwa kuleta utawala wa dola ya kiislamu. Kinachowauma nyie ni kwamba mlimpa misaada Nyerere lakini yeye akaamua kuweka utaifa mbele badala ya maslahi yenu ya kidini. Pole sana maana ishatoka hiyo na historia inatambua mwalimu ndiye aliongoza kupigania uhuru mwanzo mwisho.
Wekezeni katika elimu acheni hii ajenda yenu ya kuzaliana muwe wengi mkiamini mtaitawala Tanzania. Hilo sahauni. Juzi hapa watoto wenu mliowazaa bila mpangilio wameuwawa kama panya road huko temeke. Narudia tena jikiteni kwenye elimu ili tujenge taifa lenye maendeleo.
Lakini nani mwingine historia yake iliandikwa pamoja na ya Nyerere? Sidhani kama waliachwa wakina Sykes peke yao.Fundi...
Kwangu mimi faraja yangu ni kuwa angalau kitabu cha Abdul Sykes kimefungua mjadala leo tunayazungumza haya hadharani.
Makala yangu ya kwanza iliyochapwa na Africa Events kueleza historia ya kweli ya TANU na uhuru wa Tanganyika gazeti lote toleo zima lilikusanywa na kutolewa kwenye mzunguko.
Makala ile iliwataja Abdul na Ally Sykes na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika katika historia ya kupambana na ukoloni.
Mwandishi akatukanwa na kutishwa asithubutu kutia mambo ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika katika TANU.
Aliyenitisha mwaka ule wa 1988 ni yule kiongozi wa jopo la Chuo Cha CCM Kivukoni waliokuwa mwaka wa 1981 wanaandika historia ya TANU aliyehakikisha kuwa historia ya Sykes haiandikwi kwenye kitabu cha TANU.
Iko siku In Shaa Allah nitamweleza Prof. Malima.
Mimi jina pagan silipendi kwa sababu lilitumika kubeza imani za mababu zetu. Wageni walipotuletea dini zao kitu cha kwanza walichofanya ni kuzipa jina baya imani zetu.1. 32% + 30% + 37% = 99%. What about the 1%?
2. Wahindu hawakuhesabiwa? Au nao ni pagans/local belief? Au ndiyo hiyo 1%?
Mohammed unafananisha machungwa na mananasi. Wewe uliandika historia ya wakina Sykes, hukuandika historia ya TANU au Tanganyika. Ndio maana uliweza kwenda ndani sana kuchambua mchango wa wakina Sykes na wenzao katika historia yetu. Hukujali kilichoendelea Songea, Namtumbo, Iringa au Mbeya kama havikuhusu wakina Sykes na waislamu wenzao. Judith Listowel aliandika " The Makings of Tanganyika" na hivyo wigo wake ulikuwa maana. Alianza na uvamizi wa wajerumani, akazungumzia wale waliowapinga katika pwani ya Tanganyika (1888-9), wahehe (1891-8) na Maji Maji (1905-1907). Wewe hapa ukajikita kwenye ushiriki wa baba yake Kleist Sykes, kwengine hukujisumbua sana zaidi ya kudai kuwa waislamu ndio walioongoza mapambano hayo.Champ...
Tuchunge lugha na heshima zetu tufanye mjadala wa kupendeza.
Iko siku miaka mingi sisi hatupo watakaokuja kutusoma waseme, "Hakika walipita watu."
Hii si taarifa ya mimi kupewa.
Mimi nimeishi nyakati hizo lau nilikuwa mtoto, baba na babu yangu wameishi nyakati hizo na nimewadiriki wengi ninaowataja hapa.
Wengine nimejuananao kwa karibu sana.
Kitabu cha Abdul Sykes hakina mfano wake katika vitabu vilivyoandikwa kuhusu TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika.
Kamsome Listowel (1963) Kimambo na Temu (1969), Uloto (1971), Kivukoni (1981) na Shivji at al (2020) utaona tofauti.
Ndugu yangu si kama najisifu nataka nikuzindue utoke ujingani.
Unatuambia Waislamu twende shule wewe una elimu ya kutosha kufanya mjadala wa mada hiyo?
Ushamsoma Ishumi? (sikumbuki mwaka).
Fungua uzi nitakuja kutoa darsa.
Nisome kwa utulivu na njoo kwangu kwa mjadala kwa adabu na heshima.
Mjadala huu si mahali pa lugha "longolongo."
Hapa nipo kwa kuamini pana heshima.
Fundi...Mohammed unafananisha machungwa na mananasi. Wewe uliandika historia ya wakina Sykes, hukuandika historia ya TANU au Tanganyika. Ndio maana uliweza kwenda ndani sana kuchambua mchango wa wakina Sykes na wenzao katika historia yetu. Hukujali kilichoendelea Songea, Namtumbo, Iringa au Mbeya kama havikuhusu wakina Sykes na waislamu wenzao. Judith Listowel aliandika " The Makings of Tanganyika" na hivyo wigo wake ulikuwa maana. Alianza na uvamizi wa wajerumani, akazungumzia wale waliowapinga katika pwani ya Tanganyika (1888-9), wahehe (1891-8) na Maji Maji (1905-1907). Wewe hapa ukajikita kwenye ushiriki wa baba yake Kleist Sykes, kwengine hukujisumbua sana zaidi ya kudai kuwa waislamu ndio walioongoza mapambano hayo.
Ikafuata utawala wa wajerumani na waingereza kati ya 1906 hadi 1945. Ya tatu akazungumzia watu maarufu walioshiriki lakini akajikita zaidi kwenye ushiriki wa Nyerere. Listobel alikuwa mzungu na aliangalia historia kupitia macho ya kizungu. Hakuwa historian na hivyo kitabu chake kimekosolewa sana na wengine. Lakini cha msingi ni kuwa alitaka kuandika historia ya Tanganyika na sio ya Nyerere au Sykes. Ndio maana ingawa katika historia yake ya TANU aliwataja wakina Sykes hakwenda ndani kama ulivyofanya wewe. Kitu ambacho wakina Ilife walimkosoa ni yeye kutothamini mchango wa watu wa kawaida katika mpambano huo. Wewe umejitahidi kuwaingiza lakini bahati mbaya umepanua wigo kuwatambua waislamu wenzako waliokuwa wakiishi Dar es Salaam na Tabora. Wale waliokuwa wanaishi sehemu nyingine na hawakuwa waislamu haukuwatambua.
Kwa sababu hizi hauna ujuzi wowote wa kutoa darasa la comprehensive history ya TANU na Tanganyika. Utakachokifanya ni ku regurgitate grievances zako za siku zote kuhusu ndugu zako na kuweka picha za cover za vitabu vyako na za ndugu zako. Hiyo haitakuwa kutoa darasa bali kujaribu ku indoctrinate.
Amandla...
Fundi...Lakini nani mwingine historia yake iliandikwa pamoja na ya Nyerere? Sidhani kama waliachwa wakina Sykes peke yao.
Amandla...
Usinilazimishe ninunue kitabu chako Mohammed. Title ya kitabu inamhusu Abdulwahid Sykes na sio Tanganyika wala TANU. Hii ina maana focus ni yeye na sio watu wengine. Hao wengine ni bit players katika historia yake. Na mtu ukisoma heading za chapter zako zinaonyesha wazi focus yako ni wakina Sykes na waislamu. Haukukiandika kwa nia ya kutafuta ukweli bali kuzungumzia maonevu ambayo uliamini ndugu zako walifanyiwa. Hivyo sivyo inavyoandikwa historia ya nchi.Fundi...
Nimekuambia kama unacho kitabu fungua nenda sura baada ya sura uangalie.
Hili hukufanya unarudi hapa na hoja zile zile.
The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924-1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika Mohamed Said
Table of Contents
Dedication Acknowledgements Table of Contents Introduction
Part One
Abdulwahid Sykes 1924-1968
Chapter 1. The Sykes: Origins 1894-1929 The Old Town of Dar es Salaam and its Elites Kleist Sykes, Pioneer and Man of Ideas: 1894-1949 World War One 1914-1918 The Founding of the African Association and Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Muslim Association of Tanganyika), 1929-1933 Chapter 2.The Second World War and Tanganyika’s Political Foundation, 1939-1945
The Burma Infantry, 1942 Chapter 3. Dar es SalaamDockworkers Movement 1947-1950 Dar es Salaam Port, 1947 Erika Fiah The Dockworkers’ Union, 1948
Chapter 4. The Genesis of Open Politics in Tanganyika 1950 -1954The Tanganyika African Association, 1950 TAA Political Subcommittee, 1951 Tanganyika as a Mandate Territory Kenyan Nationalists in the Struggle of Tanganyika,1950 TAA and KAU: Attempts at Linkage and Solidarity, 1950 The Meru Land Evictions, 1950 Chapter 5. Julius Kambarage Nyerere The Story of Julius Nyerere, 1952 Tanganyika African National Union (TANU)-The Party of Independence, 1954 Chapter 6. The Pan African Congress of Northern Rhodesia, 1953 Ally Kleist Sykes Part Two
Mass Mobilisation and Independence 1954-1961
Chapter 7. Mass Mobilisation 1954 The Elders’ Council and Nyerere’s Visit to the United Nations, New York, 1954 Idd Faiz Mafongo The African Press-Ramadhani Mashado Plantan, 1950 Ahmed Rashad Ali-Radio Free Africa (Radio ya Afrika Huru), 1952 Propagandists-The Bantu Group,1955 Incorporation of Swahili Women’s Societies into the Struggle, 1955 Football As a Political Weapon Chapter 8. The Formation of the Party in the Provinces Central Province, 1955 Southern Province, 1955 Western Province, 1955 Tanga Province, 1956 TANU in Mombasa, Kenya, 1957 Chapter 9. The Tabora Conference-The Road to Independence, 1958 The Tanga Strategy, 1958 The Debate for Tripartite Voting Pan-African Movement of East and Central Africa (PAFMECA), 1958 Independence, 1961 Part Three
Conspiracy Against Islam 1961-1970
Chapter 10. The Muslim Factor in Post-Independence Tanzania 1961-1970 Islam: The Ideology of Colonial Resistance The First Muslim Congress, 1962 Resistance to Change The Second Muslim Congress, 1963 Proposal for an Islamic University, 1964 The Politics of Islam, Church, State and the African Christian Chapter 11. The East African Muslim Welfare Society (EAMWS) ‘Crisis’ Fomentation of the BAKWATA ‘Crisis’ Nyerere, Tewa, Bibi Titi Encounter, 1968 The Islamic National Conference, 1968 Omissions Analysed Betrayal of Ideals Conspiracy Theory Epilogue Bibliography
Fundi...Usinilazimishe ninunue kitau chako Mohammed. Title ya kitabu inamhusu Abdulwahid Sykes na sio Tanganyika wala TANU. Hii ina maana focus ni yeye na sio watu wengine. Hao wengine ni bit players katika historia yake. Na mtu ukisoma heading za chapter zako zinaonyesha wazi focus yako ni wakina Sykes na waislamu. Haukukiandika kwa nia ya kutafuta ukweli bali kuzungumzia maonevu ambayo uliamini ndugu zako walifanyiwa. Hivyo sivyo inavyoandikwa historia ya nchi.
Amandla...
Sio lazima wawe na historia ya wakina Sykes kama vile sio lazima historia ya wakina Sykes iwe sawa na ya Nyerere. Naamini kabisa kuwa tungejifunza mengi kama historia za watu kama John Rupia, Kassanga Tumbo, Oscar Kambona, Bibi Titi, Rashid Kawawa, Mwakangale, Eliufoo, Tibandebage na wengine wengi zingeandikwa kama ulivyoandika historia za ndugu zako. Bahati mbaya haikufanywa hivyo ndio maana unaweza kuwatanguliza ndugu zako kuliko wao.Fundi...
Katika hao walioachwa yupo mwenye historia inayokaribia historia ya akina Sykes?
Nitakisomaje bila kukinunua? Na nikinunua wewe si utafaidika? Ukweli ni kuwa majadiliano yetu na ujengaji wako wa hoja, maandishi yako mengine hayanisukumi ninunue kitabu chako.Fundi...
Mimi siuzi vitabu kwa hiyo siwezi kukulazimisha wewe au yeyote awae yule kununua moja ya vitabu vyangu.
Oxford University Press wana idara nzima ya masoko.
Ahsante Mkuu fundimchundo nimefuatilia mjadala huu muda mrefu Mzee Mohamed Said ameshindwa pasipo shaka kutetea kitabu chake ambacho amekibandika historia ya Tanu kumbe ni historia ya Wazee wake na WaIslam wa Tanganyika.Nitakisomaje bila kukinunua? Na nikinunua wewe si utafaidika? Ukweli ni kuwa majadiliano yetu na ujengaji wako wa hoja, maandishi yako mengine hayanisukumi ninunue kitabu chako.
Amandla...
Watu hawawezi kupoteza muda kutunga kitabu ili kupinga kitabu chako kama wewe ulivyofanya kwenye huu uzi. Au wewe ulitunga kitabu ili upingwe? Maandishi yako ni historia tu ya baba zako na wazee wengine wa kiislamu. Maandishi yako hayana manufaa yoyote kwa taifa la Tanzania zaidi ya manufaa kwako binafsi na waislamu ambao pia umewabagua na kuwaongelea hao wa Kariakoo tuMama...
Nizidiwe.
Nizidiwe nini na nani na anizidi kwa yeye kuandika nini katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika?
Fanya utafiti tufahamiane.
Haya ya adabu yanategemea malezi.
Baadhi yetu tunazaliwa mama zetu wanatufunza adabu ya kula ya kuamkia nk.
Tunapelekwa kumbi na chuoni tunafunzwa adabu.
Adabu inakuwa sehemu ya maisha yetu.
Ikiwa huwezi kutofautisha samahani kwa neno hili ''ushenzi,'' uungwana siwezi kukulaumu kwani huenda hukuleleka.
Nadhani umepata kusikia wanafunzi wanawapiga walimu wao.
Wengi wanauliza nini kimetokea katika jamii yetu?
Kuwa napigania dini sawa siwezi kubadili uaminicho sana nitakuuliza kwani ni vibaya kupigania dini yako iwapo pana dhulma?
Kuhusu kupotosha hii ni fursa yako na wewe kuandika historia ambayo haikupotoshwa.
Kitabu kimetimiza miaka 25 na kinakimbilia chapa ya 5 hakijapatikana kitabu kupinga kitabu cha Abdul Sykes.
Mama...Watu hawawezi kupoteza muda kutunga kitabu ili kupinga kitabu chako kama wewe ulivyofanya kwenye huu uzi. Au wewe ulitunga kitabu ili upingwe? Maandishi yako ni historia tu ya baba zako na wazee wengine wa kiislamu. Maandishi yako hayana manufaa yoyote kwa taifa la Tanzania zaidi ya manufaa kwako binafsi na waislamu ambao pia umewabagua na kuwaongelea hao wa Kariakoo tu
Fundi,Sio lazima wawe na historia ya wakina Sykes kama vile sio lazima historia ya wakina Sykes iwe sawa na ya Nyerere. Naamini kabisa kuwa tungejifunza mengi kama historia za watu kama John Rupia, Kassanga Tumbo, Oscar Kambona, Bibi Titi, Rashid Kawawa, Mwakangale, Eliufoo, Tibandebage na wengine wengi zingeandikwa kama ulivyoandika historia za ndugu zako. Bahati mbaya haikufanywa hivyo ndio maana unaweza kuwatanguliza ndugu zako kuliko wao.
Amandla...
Mohammed, ninarudia pale pale kwa sababu siku zote mada yako, ushahidi wako ni ule ule. Ni hadithi zile zile, picha zile zile. Nasema siku zote kuwa kitabu chako ni historia ya Abdulwahid Sykes na sio historia ya Tanganyika au TANU. Kuna wakati ulitaka kumfunika Kassanga Tumbo na kumuinua babu yako tukakusahihisha.Fundi,
Nitarudia kukueleza yale yale mpaka lini?
John Rupia, Titi Mohamed na Rashid Kawawa wako katika kitabu cha Abdul Sykes.
Kassanga Tumbo na babu yangu Salum Abdallah ndiyo walikuwa viongozi wa TRAU kuanzia 1955 hadi walipowekwa kizuizini 1964.
Nitakuwekea hapa historia yao.
Rashid Kawawa utamsoma na babu yangu na Tumbo In Shaa Allah nitakuwekea hapa.
Eliufoo, Mwakangale na Tibandebage...
Kidogo nacheka.
Eliufoo yumo katika mswada huu: "Under the Shadow of British Colonialism The Life of Ally Kleist Sykes. "
Ndiyo nikacheka.
Hujui historia ya uhuru.
Kuna kwengine hapakuwa na chochote.
Nilipokuwa mdogo bibi yangu Mwatum bint Mgeni akinihadithia historia ya babu yangu Sheikh Muhammad Mvamila jinsi alivyokuwa kakaa mbele ya darsa anasomesha.