Mohammed,
Si kitu cha kushangaza. Wangapi katika hawa vijana wetu wanawajua wakina John Rupia, Erica Fiah, Vedasto Kyaruzi, Mwapachu, John Mwakangale Dennis Pombeah, Steven Mhando Kassanga Tumbo na hata Oscar Kambona. Huo ni udhaifu wa jamii yetu na unaendelea mpaka sasa hivi. Mapambio yote yanaimbwa kuwasifia viongozi wa juu wakisahau kuwa kuna wengi tu wanaochangia mafanikio yao. Angalau wakina Abdul walitunukiwa medali. Oscar Kambona hata kaburi lake ni la kutafuta.
Amandla...
Fundi...
Erica Fiah...
Kwa mara yangu ya kwanza nimemsoma Erika Fiah kupitia kalamu ya Daisy Sykes Buruku, ‘The Townsman: Kleist Sykes’, in Iliffe (ed)
Modern Tanzanians, Nairobi, 1973, pp. 95-114.
Nilikuwa Arusha ndani ya Maktaba ya Taifa ambako nilikikuta kitabu hicho hapo juu alichohariri John Iliffe.
Nilivutiwa sana na mtu huyu khasa jinsi walivyokuwa anagombana na Kleist Sykes katika African Association.
Lakini kalamu ya kwanza kumweleza Erika Fiah haikuwa imeshikwa na mkono wa Daisy.
Erika Fiah kaelezwa katika mswada alioacha Kleist Sykes kabla hajafariki 1949 na Daisy akatumia chanzo hiki cha babu yake kumwandika babu yake na pia Erika Fiah.
Lakini mimi katika utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes nilizungumza na Mzee Islam Barakat mtu aliyewajua wote wawili kwa karibu sana.
Mzee Barakat akimjua Kleist na vilevile Erika Fiah.
Kutoka kwa Mzee Barakat nikamwandika Erika Fiah kwa staili yangu.
Mzee Barakat alinieleza historia ya Dockworker's Union of Dar es Salaam chama cha makuli ambacho General Secretary wake alikuwa Abdul Sykes akiwa kijana mdogo wa miaka 24.
Kama Erika Fiah alivyopambana na Kleist Sykes katika African Association katika miaka ya 1930, Erika Fiah akapambana na mtoto wa Kleist, Abdul miaka ya meishoni 1940s.
Bahati mbaya hujakisoma kitabu cha Abdul Sykes ka hiyo haya huyajui.
Wakati huo Barakat alikuwa Mwafrika wa kwanza kuwa Labour Inspector na alikuwa katika KAR pamoja Abdul Sykes wakati wa Vita Vya Pili Vya Dunia (1939 - 1945).
Vedasto Kyaruzi...
Ninao mswada wa kitabu chake, ''The Muhaya Doctor.''
Dr. Kyaruzi aliingia katika uongozi wa TAA akiwa President na Abdul Sykes Secretary kwa juhudi kubwa ya Schneider Abdillah Plantan.
Bahati mbaya katika mswada wake hakumtaja popote ila Schneider na wenzake waliowatia hawa vijana madarakani amejumiuishwa katika kundi la ''wazee'' hawana majina.
Hivi ndivyo Nyerere na yeye anavyopenda kuwaeleza wale waliomuunga mkono kuchukua uongozi wa TANU kawatambulisha kama ''wazee'' hawana majina.
Mwapachu...
Mkutano wa kuamua kumuingiza Nyerere ndani ya ''circle'' achukue uongozi wa TAA 1953 kisha mwaka wa 1954 waunde TANU ulifanyika nyumbani kwa Hamza Mwapachu Nansio Ukerewe.
Mazungumzo haya walikuwapo Hamza Mwapachu kama mwenyeji, Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe.
Ali Mwinyi alikuwa Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.
Hii ilikuwa miezi ya mwanzo ya mwaka wa 1953.
Steven Mhando...
''Mkomunisti,'' hivi ndivyo Waingereza walivyokuwa wanamuona.
Alikuwa mjumbe wa TAA Political Subcommittee wajumbe wengine wakiwa Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Sheikh Hassan bin Ameir Mufti wa Tanganyika, Sheikh Said Chaurembo na John Rupia.
Kassanga Tumbo...
Nishamweleza.
Oscar Kambona...
Kuna kitabu chake kinaandikwa.
Tusubiri.
John Rupia na Dr. Vedasto Kyaruzi
Hamza Mwapachu na Abdul Sykes
Kassanga Tumbo
Denis Phombeah