Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #201
Fundi...Mohammed, ninarudia pale pale kwa sababu siku zote mada yako, ushahidi wako ni ule ule. Ni hadithi zile zile, picha zile zile. Nasema siku zote kuwa kitabu chako ni historia ya Abdulwahid Sykes na sio historia ya Tanganyika au TANU. Kuna wakati ulitaka kumfunika Kassanga Tumbo na kumuinua babu yako tukakusahihisha.
Unasema kuwa John Rupia yumo katika kitabu chako lakini hapa unapata kigugumizi kukiri kuwa alikuwa mfadhili mkubwa TANU na ndie aliyelipia sehemu kubwa ya gharama ya safari ya Nyerere kwenda UN 1955. Unasema umemtaja lakini unashindwa kusema ndie aliyelipa fine ya shilingi 3000 aliyotozwa Nyerere katika kesi yake ya 1958. Hauwezi kuwatendea haki watu kama Solomon Eliufoo kwa kuwapachika ndani ya mswada wako unaomzungumzia Ally Kleist Sykes wakati yeye alikuwa mshauri mkubwa wa Julius Nyerere. Mimi sijui kama umemzungumzia Joan Wickens aliyekuwa anaenda kwa baiskeli Ikulu kila siku kutoka kwenye makazi yake Salvation Army.
Mimi siku utakapojitoa katika mipaka uliyokiwekea ndio nitakusoma. Siku utaweza kuwachambua wakina Sykes na waislamu kama unavyomchambua Julius Nyerere na wakristu.
Amandla....
Utanisoma kila siku na utaona haya haya kwa kuwa historia haibadiliki ni ile ile na kila siku napata wanafunzi wapya na narejea somo lile lile na picha zile zile.
Mwaka wa 25 toka kitabu cha Abdul Sykes kichapwe na kila siku kiko midomoni mwa watu.
Kitabu cha Ulotu na Kivukoni chapa mara moja vyote vimekufa.
Ushapata hata kusikia mtu anaviuliza?
Kitabu changu bado kinaishi na kila uchao nahojiwa na FM Stations na TV Stations kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyika.
Nimesimama Northwestern University, Evanston, Chicago Illinois na nimezungumza vipi kitabu changu kilivyobadili historia iliyokuwapo na kuweka historia mpya.
Leo mnaisoma upya historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika na mnaisoma upya historia ya Julius Nyerere.
Zilipoanza kejeli baada ya uhuru kuhusu TAA kuitwa ati "chama cha starehe," Ahmed Rashaad Ali akiumia roho yake na akimtaka Abdul ajibu kejeli zile.
Abdul alikataa na hakufungua kinywa chake akabakia kimya hadi anaingia kaburini mwaka wa 1968.
Katika kifo chake magazeti ya TANU Uhuru na Nationalist hawakuchapa hata taazia.
Taazia iliandikwa na kuchapwa na Brendon Grimshow Mhariri wa Tanganyika Standard.
Katika sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika Abdul Sykes na mdogo wake Ally wakapewa Medali ya Mwenge wa Uhuru na Rais Kikwete kwa mchango wao katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.
Huu ndiyo mwaka ambao baba yao Kleist Sykes maisha yake yaliyotokea katika Dictionary of African Biography (DAB).
Kleist Sykes mwanae Abdul Sykes ndugu na rafiki yangu toka udogoni alifunga safari akaja Tanga kunishukuru.
Kleist akiamini kuwa ni kitabu nilichoandika ndicho kilichosababisha baba zake watambulike.
Kleist alilia machozi kama mtoto mdogo.
Kwetu sisi huu ni ushindi mkubwa.
Mwenyezi Mungu amesema yeye kajiharamishia dhulma.
Kitabu cha Abdul Sykes na yake mengi aliyofanya kupigania uhuru wa Tanganyika ndiyo haya maneno yale yale na picha zile zile zinajirudia kila siku na watu hawachoki kunisikiliza na kunisoma.
Tazama mnavyojazana hapa.
Kitu gani kinawaleteni kwangu?
Kila mnapokuja na maswali hata kama ni ya kejeli najibu.
Niko katika shinikizo kubwa kuwa niandike maisha yangu.
Alhamdulilah Rabilalamin.
Tanganyika Standard (Sunday News) 20 October 1968
Kulia wa kwanza Mohamed Said na wa tatu ni Kleist Sykes picha hii tulipiga miezi michache baada ya kifo cha Abdul Sykes
Kushoto ni Kleist Sykes, Miski Sykes, Mohamed Said nimeshika Medali ya Mwenge wa Uhuru ya Abdul Sykes, Aisha ''Daisy'' Sykes na Ilyaas Sykes picha hii tulipiga nuyumbani kwa Kleist 2017