Makosa ndani ya Makala ya Mama Maria Nyerere Kutimiza Miaka 93

MAKALA YA MAMA MARIA NYERERE KUTIMIZA MIAKA 93 NA MAKOSA NDANI YA MAKALA

Kuna makala imewekwa mtandaoni kuhusu Mama Maria Nyerere kutimiza miaka 93 hii leo.

Makala hii imesheheni mengi katika maisha ya Mama Maria.

Nimeisoma na imenifurahisha na kunielimisha katika mengi ambayo sikuwa nayajua vyema.

Juu ya hayo yote makala hii imeruka sehemu muhimu sana katika maisha yake na kwa kweli si yake tu bali na ya mumewe Mwalimu Nyerere na historia ya TANU na pia kuandika mengine ambayo si ya kweli.

Makala hii inazungumza duka alilofungua Mama Maria Magomeni.

Mwandishi anaeleza duka hili kuwa duka lililokuwa linauza bidha kadhaa.

Hii si kweli Mama Maria alikuwa na duka dogo la kuuza mafuta ya taa.

Yako makosa mengi lakini hapa sitayazungumza tutizame hili hapo chini:

‘’In the mid 1950s, Mwalimu & his family were living at Magomeni Mapipa where they rented a small house.

This was after they had stayed in John Rupia's house at Mission Quarter, Kariakoo for one year.

This followed Mwalimu Nyerere's abrupt resignation as a teacher at St. Francis Pugu on March 22, 1955.

Mama Maria, to make ends meet, opened a small shop in their small house at Magomeni to sell sugar, soaps, salt, cooking oil etc.

She believed in living within her means and working hard for everything.

She was a rock to Mwalimu Nyerere's family.’’

Nimerekebisha machache katika historia ya Mama Maria Nyerere kwa kueleza historia yake kwa kutumia maelezo ya wale waliompokea Mwalimu alipofika Dar es Salaam mwaka wa 1952 ili historia muhimu ifahamike vizuri kwa faida ya kizazi hiki na kizazi kijacho:

"Napenda kueleza kitu kidogo katika historia ya Mama Maria Nyerere.

Katika akina mama wa mwanzo kufahamiana na Mama Maria Nyerere alikuwa Bi. Mwamvua bint Mrisho maarufu kwa jina la Mama Daisy.

Walifahamiana kwa kuwa Mama Daisy alikuwa mke wa Abdul Sykes na kama tujuavyo Mwalimu Nyerere baada ya kuacha kazi ya ualimu alikwenda kuishi nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu.

Hapa ndipo Mama Maria na Mama Daisy walipounga udugu.

Hii ilikuwa mwaka wa 1955.

Mama Daisy amenihadithia anasema baada ya miaka mingi kupita alikutana na Mama Maria Ukumbi wa Diamond Jubilee Mwalimu alipotoa hotuba kuwaaga Wazee wa Dar es Salaam.

Mama Maria alichukua fursa hii kuonana na kuzungumza na akina mama wa Dar-es-Salaam.

Mama Maria na Mama Daisy walikumbatiana kwa mapenzi Mama Maria akaieleza hadhira ile kuwa Mama Daisy na mumewe ndiyo waliowapokea yeye na mumewe Dar es Salaam.

Duka la mafuta ya taa la Mama Maria alilifungua Mtaa wa Mchikichi na Livingstone wakati wanaishi nyumbani kwa Abdul Sykes.

Akina mama ambao walikuwa jirani na duka hili walikuwa Bi. Chiku bint Said Kisusa ambae alikuwa anaishi mtaa huo wa Mchikichi kona na New Street (sasa Lumumba Avenue).

Duka la mafuta ya taa la Magomeni Mapipa Mama Maria alilifungua nyumbani kwa Ali Msham Mtaa wa Jaribu.

Ali Msham alikuwa amefungua tawi la TANU nyumbani kwake na Mwalimu alipohamia Maduka Sita Magomeni ikabidi Mama Maria awe anakwenda Kariakoo kila siku.

Ali Msham ndipo alipotoa nafasi nyumbani kwake duka lihamishiwe hapo ili kumpumzisha Mama Maria na shida ya kuparamia mabasi na watoto asubuhi kwenda Kariakoo.

Duka la mafuta ya taa la Mama Maria la hapo Maduka Sita lilikuja baadae.

Tunamtakia Mama Maria umri tawil na afya njema."

Picha hiyo hapo chini ni nyumba ya Mwalimu Maduka Sita Magomeni na huyo anaeingia ndani ya nyumba hiyo ni yeye mwenyewe.

Angalia bango juu ya nyumba linalotangaza duka la mafuta ya taa.

323194726_553729993036637_5201274679647759998_n.jpg
dingi na uwongo mligombana ,hongera sana
 
Hivi unadhani kila kitu lazima kiandikwe? Unajua Nyerere aliolea kwa nani akiwa anafundisha Tabora? Huyo Sykes wako unamtukuza hadi unaboa
Kolola,
Usikasirike na kutumia lugha zisizofaa.

Kama uko "bored," unajitoa katika huu mjadala.
"Sykes wako."

Wangu mimi au mzalendo aliyepigania uhuru wa Tanganyika na rafiki wa Nyerere?

Historia yake ipo kwenye kitabu atakae anasoma.

Nimealikwa kumzungumza University of Iowa, Northwestern University Marekani na Zentrum Moderner Orient (ZMO), Ujerumani.

Nani anaemtukuza Abdul Sykes?
Ni mimi au vyuo hivyo?

Nani anaemtukuza Abdul Sykes ni mimi au ni wasomaji wa kitabu chake kinachokwenda sasa chapa ya 5?

Nani anaemtukuza Abdul Sykes ni mimi au nyinyi mnaojadili historia hii ambayo yeye alihusika?
 
Kwa vile wewe ni mtu mzima, nadhani umenielewa kuhusu huyo Sykes wako
 
Tulia.
Ondoa hamaki huu ni mjadala tu.
Tunapambanisha hoja.

Jiepushe na hiyo lugha, "Sykes wako."

Mimi sijakuelewa.
Nifafanulie.
 
Sijui kwanini sikuzaliwa zamani hizo za uhuru inaonekana maisha yalikuwa na mvuto wake hata wakati wadogo maisha yalikuwa na mvuto wake tofauti na sasa
 
Mzee Mohamed Said heshima sana kwako ! Unatupa madini sana !!
Kwa hiyo kipindi hicho mama maria anauza mafuta ya taa ! Umeme haukuepo kabisa ?
Chry...
Nyumba chache sana Kariakoo zilikuwa na umeme.

Mimi nimezaliwa mwaka wa 1952 kwenye nyumba ambayo haikuwa na umeme Mtaa wa Kipata nyuma ya Mtaa wa Uhuru (zamani Kitchwele).

Wala hapakuwa na maji ndani.

Maji yakitekwa kwenye bomba la mtaani kwa kutumbukiza senti moja unapata debe moja.
 
Tumetoka mbali sana ! Mungu awaweke tujifunze ya nyuma kidogo !
 
Uzuri umeweka picha ambayo ina bango la kuwa ni mawakala wa mafuta ya taa ya Shell Crown. Lakini pia kuna bango la Cocacola na pembeni kuna lingine ambalo bidhaa zake hazionekani vizuri. Kwa picha hiyo ni dhahiri kuwa alikuwa anauza bidhaa zaidi ya mafuta ya taa. Sasa kama kwenye hili unasema uongo kwa nini tukuamini kwenye mengine?

Amandla.....
Nguruvi3 JokaKuu
We akili huna,
 
MAKALA YA MAMA MARIA NYERERE KUTIMIZA MIAKA 93 NA MAKOSA NDANI YA MAKALA

Kuna makala imewekwa mtandaoni kuhusu Mama Maria Nyerere kutimiza miaka 93 hii leo.

Makala hii imesheheni mengi katika maisha ya Mama Maria.

Nimeisoma na imenifurahisha na kunielimisha katika mengi ambayo sikuwa nayajua vyema.

Juu ya hayo yote makala hii imeruka sehemu muhimu sana katika maisha yake na kwa kweli si yake tu bali na ya mumewe Mwalimu Nyerere na historia ya TANU na pia kuandika mengine ambayo si ya kweli.

Makala hii inazungumza duka alilofungua Mama Maria Magomeni.

Mwandishi anaeleza duka hili kuwa duka lililokuwa linauza bidha kadhaa.

Hii si kweli Mama Maria alikuwa na duka dogo la kuuza mafuta ya taa.

Yako makosa mengi lakini hapa sitayazungumza tutizame hili hapo chini:

‘’In the mid 1950s, Mwalimu & his family were living at Magomeni Mapipa where they rented a small house.

This was after they had stayed in John Rupia's house at Mission Quarter, Kariakoo for one year.

This followed Mwalimu Nyerere's abrupt resignation as a teacher at St. Francis Pugu on March 22, 1955.

Mama Maria, to make ends meet, opened a small shop in their small house at Magomeni to sell sugar, soaps, salt, cooking oil etc.

She believed in living within her means and working hard for everything.

She was a rock to Mwalimu Nyerere's family.’’

Nimerekebisha machache katika historia ya Mama Maria Nyerere kwa kueleza historia yake kwa kutumia maelezo ya wale waliompokea Mwalimu alipofika Dar es Salaam mwaka wa 1952 ili historia muhimu ifahamike vizuri kwa faida ya kizazi hiki na kizazi kijacho:

"Napenda kueleza kitu kidogo katika historia ya Mama Maria Nyerere.

Katika akina mama wa mwanzo kufahamiana na Mama Maria Nyerere alikuwa Bi. Mwamvua bint Mrisho maarufu kwa jina la Mama Daisy.

Walifahamiana kwa kuwa Mama Daisy alikuwa mke wa Abdul Sykes na kama tujuavyo Mwalimu Nyerere baada ya kuacha kazi ya ualimu alikwenda kuishi nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu.

Hapa ndipo Mama Maria na Mama Daisy walipounga udugu.

Hii ilikuwa mwaka wa 1955.

Mama Daisy amenihadithia anasema baada ya miaka mingi kupita alikutana na Mama Maria Ukumbi wa Diamond Jubilee Mwalimu alipotoa hotuba kuwaaga Wazee wa Dar es Salaam.

Mama Maria alichukua fursa hii kuonana na kuzungumza na akina mama wa Dar-es-Salaam.

Mama Maria na Mama Daisy walikumbatiana kwa mapenzi Mama Maria akaieleza hadhira ile kuwa Mama Daisy na mumewe ndiyo waliowapokea yeye na mumewe Dar es Salaam.

Duka la mafuta ya taa la Mama Maria alilifungua Mtaa wa Mchikichi na Livingstone wakati wanaishi nyumbani kwa Abdul Sykes.

Akina mama ambao walikuwa jirani na duka hili walikuwa Bi. Chiku bint Said Kisusa ambae alikuwa anaishi mtaa huo wa Mchikichi kona na New Street (sasa Lumumba Avenue).

Duka la mafuta ya taa la Magomeni Mapipa Mama Maria alilifungua nyumbani kwa Ali Msham Mtaa wa Jaribu.

Ali Msham alikuwa amefungua tawi la TANU nyumbani kwake na Mwalimu alipohamia Maduka Sita Magomeni ikabidi Mama Maria awe anakwenda Kariakoo kila siku.

Ali Msham ndipo alipotoa nafasi nyumbani kwake duka lihamishiwe hapo ili kumpumzisha Mama Maria na shida ya kuparamia mabasi na watoto asubuhi kwenda Kariakoo.

Duka la mafuta ya taa la Mama Maria la hapo Maduka Sita lilikuja baadae.

Tunamtakia Mama Maria umri tawil na afya njema."

Picha hiyo hapo chini ni nyumba ya Mwalimu Maduka Sita Magomeni na huyo anaeingia ndani ya nyumba hiyo ni yeye mwenyewe.

Angalia bango juu ya nyumba linalotangaza duka la mafuta ya taa.

323194726_553729993036637_5201274679647759998_n.jpg
Hiyo makala unayodai ina makosa. mwandishi aliongea na mama Maria mwenyewe na mwanaye Madaraka. Nadhani hao wanaaminika zaidi kuliko third party
 
Chry...
Hakika maisha yamebadilika sana.
Mzee...
Vijana wako wanashangaa eti kwanini nyerer hakitaja ukweli wa historia yake.

Hivi mwenye dhamira unajiuliza kwnini anadhamiri tena?

Mzee una kipaji na elimu ya kuwavumilia Waefeso hawa, ila sisi tunawaona wasumbufu kama Walawi wa Musa
 
Back
Top Bottom