Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Ufahamu wa mtoto tangu akiwa mdogo anaanza kuongea ni kama bank account, unachohifadhi ndicho unachovuna. Watoto wakianza kuongea wanakua na maswali mengi, hii ni asili yao ya kutaka kufahamu dunia.
Usichoke kumfahamisha mazingira anayo ishi. Ukiamka asubuhi akikuuliza unakwenda wapi mueleze kwa ufasaha kwa kiwango cha uelewa wake kuwa ni lazima uwende unakokwenda ili upate pesa. Mueleze faida ya kazi unayofanya na jinsi inavyosaidia jumuia. Hata kama unapika maandazi, mueleze umuhimu wa unachofanya.
Watoto wanaopata maarifa mapema inawasaidia kuwa wasadadisi zaidi na huelewa mambo mengi. Kuongea na kuwafahamisha watoto pia kunawajengea ujasiri wa maisha.
Mtoto akiharibu simu, ipad au remote control, usimpige. Mueleze umuhimu wa kifaa na shida mtakayo pata kikiharibika. Vitu vyako vya muhimu jaribu kuviweka mbali lakini akikukuta unanyoa ndevu mueleweshe kifaa unachotumia na umuhimu wake. Sisi wakina mama make up zetu tuweke mbali na ukipaka akikuona na akitaka kufahamu mueleweshe.
Kuzaa si kazi kazi kulea.