Makosa tunayo fanya wazazi kwa watoto wetu ni kutowapa ufahamu wa kutosha tangu wakiwa wadogo

Na wale tusio na wake wala watoto tuna-comment wapi na nini? Japo kwa ufupi watoto wa leo wako entitled sana. Yani aakishapata ufahamu anaona anastahili kuwa na simu kali, mavazi makali, maisha makali ili awaonyeshee wenzake mitandaoni. Wakike wanaishia kudanga ktk umri mdogo na KUPIGWA MIMBA TU OVYO na wa kiume wanaanza madeals deals nk ktk umri mdogo
 
Mtoto huwa anaanza kufahamu mavazi mazuri umri miaka mitano kuendelea. Kama unamuona anapenda muonekano unaweza kutumia nguo anazopenda kwa reward of good behaviour.

Ukiwa kama mzazi ni muhimu kufahamu alichonancho mtoto wako na kama hujamnunulia wewe ujue kimetoka wapi.

Kama huna mtoto weka akiba ya maneno.
 
Sina mtoto lakini napenda kujifunza kwa walio na watoto. Ndio nimewaona siku hizi wengi wamekuwa hivyo. Wadada wadogo ambao hawako shuleni ni kudanga tu. Vijana wadogo wanahangaika mtaani lakini hawataki kazi ngumu. Mimi naona katika post yako kitu ungeongezea ni UMUHIMU wa kumfunza mtoto kufanya kazi kwa bidii na kutochagua kazi tokea akiwa mdogo na pia kumfunza asiwe na peer pressure manake ajifunze kutoiga wenzake wenye vitu vizuri au manake ajifunze KURIDHIKA na alicho nacho WAKATI ANAPAMBANA KUPATA CHAKE KIZURI. Kuchagua kazi, uvivu hata wa kujisomea wakiwa shuleni, na kutaka kuiga maisha na mwenendo wa marafiki ni mambo yanayopoteza watoto wengi sana
 
Sasa huku mjini atacheza na nani kila MTU kwake dear?? Nitafutie MTU nizae nae basi
Hio ndio effect ya nyumba za mageti kwenye malezi. Hamna namna kwenda na nyakati japo zinatujengea tabia nyingine mpya kabisaa.
 
House girl anajua matatizo ya mume na mtoto kuliko mke wa ndoa,

House girl anakaa mda mwingi na mtoto mpaka anajua ndo mama yake,

Sasa upendo utatoka wapi hapo lazima yotokee tunayoyasikia tu.
 
Sasa
Sasa sisi wa kishua koko unatuambiaje, wazazi wa kina Prince? Wale mtoto akiona mgeni ndo kwanza anataka kuangalia mikatuni yake Disney , mara kachukua mgari wake mtoy mkubwaa wa formula one. Anazunguka nalo sebulen.

Mama ana kaujauzito katumbo kamechomoka , yupo na kigauni kifupi,Prince akichoka anakimbilia chini ya miguu ya mama. Utasikia wewe P, acha ujinga! Baba P unamuona mwanao?!Baba akiwa na kinjunga yupo anacheki gemu ya Man U kwa tablet, Samsung ikiwa kwenye chaji ,utasikia wewe Prince nenda kachukue πŸ” kwenye friji.

Ila sisi tunajua kuigiza life jamani
 
Aisee!!!?
 
Rafiki yangu aliwafundisha watoto wake, akija mgeni wanamsalimia na kupotea vyumbani kwao, wakibaki sebuleni labda mgeni amekuja na mtoto wa umri wao. Wanaitwa kama chakula tayari na mgeni atakula na familia.
 
Rafiki yangu aliwafundisha watoto wake, akija mgeni wanamsalimia na kupotea vyumbani kwao, wakibaki sebuleni labda mgeni amekuja na mtoto wa umri wao. Wanaitwa kama chakula tayari na mgeni atakula na familia

Rafiki yangu aliwafundisha watoto wake, akija mgeni wanamsalimia na kupotea vyumbani kwao, wakibaki sebuleni labda mgeni amekuja na mtoto wa umri wao. Wanaitwa kama chakula tayari na mgeni atakula na familia.
Mh! Hii nayo si nzuri aisee. Lini sasa watoto watajifunza kujamiiana na wanajamii? Waweze kuchanganyika kwa kuzingatia maadili
 
Nimeshuudia mtoto kwa umri ulioutaja anakataa kulala nyumba ya udongo kwa bibi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…