Makosa ya kimkakati kuhusu covid 19, yataigharimu Tanzania kiuchumi

Makosa ya kimkakati kuhusu covid 19, yataigharimu Tanzania kiuchumi

KISHADA

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
2,226
Reaction score
3,293
Kwa kadiri siku zinavyosogea, tutashuhudia mengi kuhusu namna viongozi wetu wanavyoshughulikia Corona.

Mimi nielekee eneo la uchumi unaotokana na mahusiano au ushirikiano na mataifa mengine.

Tuanzie na utalii ambao nao unachangia fedha nyingi za kigeni na ajira kwa Watanzania.

Watalii wa nje ni watu kutoka mataifa mengine. Hawa wenzetu wako makini kusikiliza mataifa yao yanasemaje kuhusu usalama wao. Serikali yetu inapokuwa haiaminiki au haiko wazi kwenye taarifa za covid huo utalii tutausikia tu. Huwezi kushawishi wazungu na watalii kwa kufungua anga tu lakini kukawa na ukakasi kuhusu usalama wa watalii.

Taarifa za Corona, mtazamo wa mapambano na hatua za mapambano zinahitaji kuwa smart na zisizotiliwa mashaka.

Kwenye hili Tanzania tumeshafeli mapema. Ikumbukwe taasisi kama WHO na balozi mbali mbali kauli zao kuhusu Tanzania na njia za kupambana na Corona ni muhinu Sana kwa kujenga imani ya watalii kuja Tanzania. Kwa mpaka sasa Tanzania imeamua kutumia njia za kienyeji na taarifa zake nyingi zinapingana au zinaleta shida katika ulimwengu wa sayansi.

Kwa mfano kauli za Rais kuhusu njia za kutibu Corona kwa kutumia kujifukiza hakujapata ithibati ya kitaalamu kutoka mamlaka za kiafya za kidunia. Suala la vipimo vya maabara na hatua za kufichwa taarifa za maambukuzi Hadi Sasa kunashusha imani ya serikali. Katika Hali hio tusitegemee kupata watalii Hadi jitihada kubwa ifanywe kuwaaminisha usalama wao.

Hata mgogoro na majirani zetu kuhusu namna tunavyoshughulikia corona, kumejengeka picha kwamba Tanzania Haina mashirikiano mazuri ya kikanda kuhusu kupambana na Corona. Hii yote inashusha imani.

Sitoshangaa mataifa mengine kuwaondoa raia wao Tanzania Kama ilivyofanya Uingereza na kutolewa kauli za tahadhari zaidi ambazo zitafifisha utalii wetu na biashara nyengine.

Tatizo ni kutopima kauli kwa viongozi wetu pia na kubeza, kukosa uwazi wa taarifa, kukosa mashirikiano na kuchukuliwa hatua muafaka za makubaliano ya Pamoja. Katika hali hio tunaweza kukuta sekta ya utalii na uchumi wetu kuchelewa kuimarika.

Tanzania siyo kisiwa inapaswa ijifungue kutoka kwenye madhaifu ya utawala uliopo na tuendane na uhalisia kwa kuimarisha mahusiano, mashirikiano ya kikanda na kimataifa na kuchunga miiko ya kidiplomasia Ili kurejesha imani na mashirika, wadau wa maendeleo na uchumi na mataifa mengine.

Janga la Corona athari zake sio ndogo. Viongozi wetu waiweke Tanzania pahali pake na ifike mahali taswira hasi ya Tanzania kwenye Kila jambo kimataifa liondolewe.


Kishada
 
Ni kweli kabisa, wangetakiwa wawe na mkakati dhabiti kuonyesha jinsi wanavyoshughulikia tatizo la C-19 otherwise tutatengwa kwa muda refu sana hasa kwenye sector ya utalii na biashara ya mwingiliano .Kutokuwa consistency na matamshi yetu wenyewe ni shughuli.
 
Ndiyo hivyo sasa, ndege zimeshajaa watalii wa kuja kufanya utalii. Bila shaka kuna Watalii wengi sana watapenda kuja kubadili upepo na hali ya hewa nchini mwetu baada ya kupambana na Corona huko kwao. Muhimu Serikali iwe tu makini zaidi na hao wageni maana ndiyo hao hao waliotuletea hiyo Corona hapo awali.
 
Tanzania sio kisiwa inapaswa ijifungue kutoka kwenye madhaifu ya utawala uliopo na tuendane na uhalisia kwa kuimarisha mahusiano, mashirikiano ya kikanda na kimataifa na kuchunga miiko ya kidiplomasia Ili kurejesha imani na mashirika, wadau wa maendeleo na uchumi na mataifa mengine.


Jr[emoji769]
 
[emoji15][emoji15][emoji15]
masoudkipanya_CAb4xueDkna.jpg
 
Back
Top Bottom