Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,316
- 871,876
Mshikwa na kidhibiti ndio mwenye kesiMtumaji au mchoraji? Kwako Mshana Jr
Jr[emoji769]
Mshikwa na kidhibiti ndio mwenye kesiMtumaji au mchoraji? Kwako Mshana Jr
Siyo wote mkuu?Mshikwa na kidhibiti ndio mwenye kesi
Jr[emoji769]
Dunia haiendi hivyo. Diplomasia ni muhimu Sana. Sio Kila kitu lazima upinge ilimradi tu uoneshe madhaifu yako. Hili la covid ushirikiano ni muhimu Sana kwa sababu tunahitaji kuaminika ili mambo mengine yaende.Kuacha kufuata mkumbo wa lockdown ndo hatupambani na #covid19? Hizo njia za kisayansi zimewasaidia nn hadi sasa hao wanaozifuata.
Acha parojo Rais Magufuli kasema ndege zimejaa wanataka kuka kutalii wewe unaleta maneno ya uoga
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kadiri siku zinavyosogea, tutashuhudia mengi kuhusu namna viongozi wetu wanavyoshughulikia Corona.
Mimi nielekee eneo la uchumi unaotokana na mahusiano au ushirikiano na mataifa mengine.
Tuanzie na utalii ambao nao unachangia fedha nyingi za kigeni na ajira kwa Watanzania.
Watalii wa nje ni watu kutoka mataifa mengine. Hawa wenzetu wako makini kusikiliza mataifa yao yanasemaje kuhusu usalama wao. Serikali yetu inapokuwa haiaminiki au haiko wazi kwenye taarifa za covid huo utalii tutausikia tu. Huwezi kushawishi wazungu na watalii kwa kufungua anga tu lakini kukawa na ukakasi kuhusu usalama wa watalii.
Taarifa za Corona, mtazamo wa mapambano na hatua za mapambano zinahitaji kuwa smart na zisizotiliwa mashaka.
Kwenye hili Tanzania tumeshafeli mapema. Ikumbukwe taasisi kama WHO na balozi mbali mbali kauli zao kuhusu Tanzania na njia za kupambana na Corona ni muhinu Sana kwa kujenga imani ya watalii kuja Tanzania. Kwa mpaka sasa Tanzania imeamua kutumia njia za kienyeji na taarifa zake nyingi zinapingana au zinaleta shida katika ulimwengu wa sayansi.
Kwa mfano kauli za Rais kuhusu njia za kutibu Corona kwa kutumia kujifukiza hakujapata ithibati ya kitaalamu kutoka mamlaka za kiafya za kidunia. Suala la vipimo vya maabara na hatua za kufichwa taarifa za maambukuzi Hadi Sasa kunashusha imani ya serikali. Katika Hali hio tusitegemee kupata watalii Hadi jitihada kubwa ifanywe kuwaaminisha usalama wao.
Hata mgogoro na majirani zetu kuhusu namna tunavyoshughulikia corona, kumejengeka picha kwamba Tanzania Haina mashirikiano mazuri ya kikanda kuhusu kupambana na Corona. Hii yote inashusha imani.
Sitoshangaa mataifa mengine kuwaondoa raia wao Tanzania Kama ilivyofanya Uingereza na kutolewa kauli za tahadhari zaidi ambazo zitafifisha utalii wetu na biashara nyengine.
Tatizo ni kutopima kauli kwa viongozi wetu pia na kubeza, kukosa uwazi wa taarifa, kukosa mashirikiano na kuchukuliwa hatua muafaka za makubaliano ya Pamoja. Katika hali hio tunaweza kukuta sekta ya utalii na uchumi wetu kuchelewa kuimarika.
Tanzania siyo kisiwa inapaswa ijifungue kutoka kwenye madhaifu ya utawala uliopo na tuendane na uhalisia kwa kuimarisha mahusiano, mashirikiano ya kikanda na kimataifa na kuchunga miiko ya kidiplomasia Ili kurejesha imani na mashirika, wadau wa maendeleo na uchumi na mataifa mengine.
Janga la Corona athari zake sio ndogo. Viongozi wetu waiweke Tanzania pahali pake na ifike mahali taswira hasi ya Tanzania kwenye Kila jambo kimataifa liondolewe.
Kishada
Acheni nyinyi.
Dunia Ina formula zake katika kuyaendea mambo na kuleta ushawishi.
Hivi unadhani wanaofuata miongozo hiyo ni wajinga. Utashawishi vipi watu kuwa Corona imeisha kama mambo haya yako hivi
1. Unasindwa kuchukua hatua za kuchukuwa za ushauri wa kitaalamu was awali
2. Unahamasisha mikusanyiko pasi hadhari za kutosha
3. Unaambiwa umechelewa kuchukuwa hatua elekezi na WHO unajimazia bila hatua.
4. Hatua elekezi ya lockdown hata walau ya maeneo maalumu unasema uchumi utayumba utafikiri ni Tanzania pekee ndio itayumba.
5. Majirani wanataka makubaliano ya mkakati unasusa.
6. Unapinga vipimo vya maabara unaaanza kuwahusisha mabeberu, kibaya zaidi unaongea public.
7. Unakataa mashirikiano ya wadau wa ndani na unakataa mawazo yao kwa kuwaita mawakala wa mabeberu.(wapinzani).
8. Unajiamulia kivyako kuanza kuondowa walau zile hatua chache za kuzuia maambukuzi bila kuomba kupata ushauri wa kikanda na mamlaka za kiafya za dunia.
Katika Hali hio, unategemea Nini happy baadae usiposhirikushwa kwenye mikakati mengine yenye maslahi kimataifa kwa kuitwa mkorofi usiye mashirikiano?
Tuitendee Haki Tanzania katika Kila eneo. Diplomasia tumepwaya sana
Hata huko kwenye madini umefuatilia kuona hali ipoje kwa sasa? Na zile >400tr shs tumelipwa ngapi?Wakati tunaanza harakati za makinikia wengi walikuja na uoga kama huu!
Bobu jaribu kutembelea platforms za kimataifa usiishie tu jf humu halafu unaconclude....huko ndo utajua nchi yako inazungumziwa vipi..,katoe tongotongo fikra zako zifunguke.Dunia haiendi hivyo. Diplomasia ni muhimu Sana. Sio Kila kitu lazima upinge ilimradi tu uoneshe madhaifu yako. Hili la covid ushirikiano ni muhimu Sana kwa sababu tunahitaji kuaminika ili mambo mengine yaende.
Nakwambia hili la covid inavyoshughulikiwa Tanzania, limeongeza value ya kwenye uhasi wa watawala wetu na sio value kwenye chanya. Yumkini Tanzania ndio inaaibika.
Kwanza hawa viongozi walitakiwa kuhakikisha usalama wa wananchi kwa kuhimiza wote tuvae barakoa na kwa njia hii maambukizi yangepungua ,lakini sasa naona wanataka huu ugonjwa uchukue mkondo wake kwaniwabaki wale waliopona na dhaifu waondoke,kwa kufanya hivyo wale vibabu wa Ulaya ambao ndio wenye hela ykuja kutalii hawatakuja kwani wanaamini bado hapa kwetu patakuwa kitovu cha ugonjwa kutokana na staili ya uendeshwaji wa huu ugonjwa.Inashangaza pale tunaposema tusivae barakoa,ywende kwenye madansi sijui lengo ni nini.Mungu utunusuru ndio kilichobaki,kwani peke yako ukijikinga na mwingine hajajikinga basi nafasi ya kuambukizwa itabaki palepale.Kwa kadiri siku zinavyosogea, tutashuhudia mengi kuhusu namna viongozi wetu wanavyoshughulikia Corona.
Mimi nielekee eneo la uchumi unaotokana na mahusiano au ushirikiano na mataifa mengine.
Tuanzie na utalii ambao nao unachangia fedha nyingi za kigeni na ajira kwa Watanzania.
Watalii wa nje ni watu kutoka mataifa mengine. Hawa wenzetu wako makini kusikiliza mataifa yao yanasemaje kuhusu usalama wao. Serikali yetu inapokuwa haiaminiki au haiko wazi kwenye taarifa za covid huo utalii tutausikia tu. Huwezi kushawishi wazungu na watalii kwa kufungua anga tu lakini kukawa na ukakasi kuhusu usalama wa watalii.
Taarifa za Corona, mtazamo wa mapambano na hatua za mapambano zinahitaji kuwa smart na zisizotiliwa mashaka.
Kwenye hili Tanzania tumeshafeli mapema. Ikumbukwe taasisi kama WHO na balozi mbali mbali kauli zao kuhusu Tanzania na njia za kupambana na Corona ni muhinu Sana kwa kujenga imani ya watalii kuja Tanzania. Kwa mpaka sasa Tanzania imeamua kutumia njia za kienyeji na taarifa zake nyingi zinapingana au zinaleta shida katika ulimwengu wa sayansi.
Kwa mfano kauli za Rais kuhusu njia za kutibu Corona kwa kutumia kujifukiza hakujapata ithibati ya kitaalamu kutoka mamlaka za kiafya za kidunia. Suala la vipimo vya maabara na hatua za kufichwa taarifa za maambukuzi Hadi Sasa kunashusha imani ya serikali. Katika Hali hio tusitegemee kupata watalii Hadi jitihada kubwa ifanywe kuwaaminisha usalama wao.
Hata mgogoro na majirani zetu kuhusu namna tunavyoshughulikia corona, kumejengeka picha kwamba Tanzania Haina mashirikiano mazuri ya kikanda kuhusu kupambana na Corona. Hii yote inashusha imani.
Sitoshangaa mataifa mengine kuwaondoa raia wao Tanzania Kama ilivyofanya Uingereza na kutolewa kauli za tahadhari zaidi ambazo zitafifisha utalii wetu na biashara nyengine.
Tatizo ni kutopima kauli kwa viongozi wetu pia na kubeza, kukosa uwazi wa taarifa, kukosa mashirikiano na kuchukuliwa hatua muafaka za makubaliano ya Pamoja. Katika hali hio tunaweza kukuta sekta ya utalii na uchumi wetu kuchelewa kuimarika.
Tanzania siyo kisiwa inapaswa ijifungue kutoka kwenye madhaifu ya utawala uliopo na tuendane na uhalisia kwa kuimarisha mahusiano, mashirikiano ya kikanda na kimataifa na kuchunga miiko ya kidiplomasia Ili kurejesha imani na mashirika, wadau wa maendeleo na uchumi na mataifa mengine.
Janga la Corona athari zake sio ndogo. Viongozi wetu waiweke Tanzania pahali pake na ifike mahali taswira hasi ya Tanzania kwenye Kila jambo kimataifa liondolewe.
Kishada
Rudia Tena mada
Umeona. Kuna mambo ya muhimu ya kimkakati yameachwa Hadi sasaKwanza hawa viongozi walitakiwa kuhakikisha usalama wa wananchi kwa kuhimiza wote tuvae barakoa na kwa njia hii maambukizi yangepungua ,lakini sasa naona wanataka huu ugonjwa uchukue mkondo wake kwaniwabaki wale waliopona na dhaifu waondoke,kwa kufanya hivyo wale vibabu wa Ulaya ambao ndio wenye hela ykuja kutalii hawatakuja kwani wanaamini bado hapa kwetu patakuwa kitovu cha ugonjwa kutokana na staili ya uendeshwaji wa huu ugonjwa.Inashangaza pale tunaposema tusivae barakoa,ywende kwenye madansi sijui lengo ni nini.Mungu utunusuru ndio kilichobaki,kwani peke yako ukijikinga na mwingine hajajikinga basi nafasi ya kuambukizwa itabaki palepale.
Tanzania isifananishwe na Superpower MarekaniHao WHO wanaodharauliwa na marekani au?
Kwani hao WHO wanajua kuwa ninyi waafrika huwa mnatibiwa kwa waganaga na mnapona, na kama mnaheshim hizo sheria za WHO kwa nini mnatumia dawa za kienyeji wakati mnajua ni makosa?
Hao WHO hawajitambui achana nao.