Makosa ya kuepuka katika uvaaji wako wa suti

Makosa ya kuepuka katika uvaaji wako wa suti

Zurie

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2014
Posts
2,012
Reaction score
5,571
Suti ni vazi la heshima sana na linamfanya mtu kuonekana maridadi sana lakini ukikosea kuvaa suti waweza kuwa kituko. A traditional suit ya mwanaume inajumuisha shati, koti, tai na suruali.

Zifuatazo ni tip za ku-coordinate vitu hvyo vema kabisa ili kupata muonekano maridhawa.

IMG-20161004-WA0004.jpg


Hii tip hata jirani yangu hapa ofisini inamhusu. Msivae vest za kukaba koo jamani. Haivutii vest kuchomoza kwa nje ya shati lako.

IMG-20161004-WA0001.jpg


Tai isiwe ndefu sana kupita mkanda au fupi sana. Ikiwa iishie usawa wa mkanda wako. Rangi za tai pia jamani muwe mnaangalia, ingawa najua wengi wenu ni color blind!

IMG-20161004-WA0002.jpg



Kuonesha brand sio issue. Nguo quality utaijua tu kwa material yake.

IMG-20161004-WA0003.jpg


Hapa wale ndugu zetu mashabiki wa 'Waaaasaaaafiiiiii' au wale wazee wa Sigda usoni hawawezi kuelewa ila kuonesha vijiguu vyako chini ya trouser sio kabisa. Pia kuvaa msulupwete unalegea huku chini ndo worse. Vaa length nzuri isiyoburuza chini na wala isiexpose soksi zako.

Nawatakia Alhamisi njema, Nawapenda woote!
 
Picha ya kwanza ya kuonesha Vest inamuhusu kiongozi mkubwa sana nchi hii. Nimemuona mara mbili vest yake imechomoza kwa juu!

Sijui ni Bullet Proof. Labda
 
Asante sana kwa thread nzuri sana. Hakika watu wengi tumekuwa tukikosea bila kujua. Hii itasaidia sana, Ubarikiwe Zurie
 
Hiyo namba 3 kuhusu urefu wa surual kiukwel inategemeana na fashion na mamb yanabadilika

Sahv mtu kuvaa suru fupi na tai ni kawaida coz ndo fashion
 
Hiyo ya kuvaa koti la label sijui kama wabongo wataweza kuiacha maana ni tatizo sugu. Mafundi washona suti wana label kabisa za kuweka kwenye mkono wa koti. Ukisema ni sivyo inavyovaliwa wewe ndio unaonekana mshamba. Asante kwa maelekezo, wababa funguo macho na kufuata sio kusoma na kuacha hapa ni somo muhimu sana hili
 
Hiyo ya kuvaa koti la label sijui kama wabongo wataweza kuiacha maana ni tatizo sugu. Mafundi washona suti wana label kabisa za kuweka kwenye mkono wa koti. Ukisema ni sivyo inavyovaliwa wewe ndio unaonekana mshamba. Asante kwa maelekezo, wababa funguo macho na kufuata sio kusoma na kuacha hapa ni somo muhimu sana hili

img-20161004-wa0002-jpg.432137


Hapo ndio huwa najiuliza au kuna watu wanaazima hizo nguo wanatakiwa wazirudishe baadae dukani?
Inakuwaje unatembea na label? Kuna ingine ameisahau kidogo hizi suti zinakuja hazijafumuliwa mifuko ya koti, wengine wanaicha hivyo hivyo....
 
Back
Top Bottom