Makosa ya Upinzani


Hatuna akina Raila na tunaweza tusipate. Lakini tunashindwa kumpata Svangirai? mtu ambaye maisha yake, hamu yake, historia yake ni kupigania haki za wanyonge kikweli kweli bila woga? come on guys! Robert Mugabe alikuwa anaungwa mkono na waZimbabwe kuliko Kikwete, jamaa ni mbabe kuliko yeyote yule Tanzania. ZANU-PF ilikuwa inaungwa mkono kuliko CCM inavyoungwa mkono.

Lakini tumeshuhudia wananchi wa Zimbabwe wakichagua wabunge wa upinzani na Svangirai akipata zaidi ya 47% licha ya Mugabe kuiba na kutishia maafisa wa kura. Mkuu wa majeshi wa Zimbabwe alishasema hawezi kumpigia saluti kiongozi wa upinzani hata akishinda Urais. Lakini wananchi bado walimchagua Svangirai. Wananchi walipiteswa na wengine wakauawa lakini bado tu.

Upinzani wa Tz umejifunza nini toka MDC?

Mkuu Zitto, muda huu ndo ulikuwa wa kujenga chama na kuhamasisha wananchi kwa ajili ya uchaguzi. Lakini kimyaaaa hakuna operation sangara wala zinduka. Viongozi wetu mnasubiri muda wa kampeni. Hakuna ushindi hapo. Ninawasiwasi sana na ninyi viongozi wetu, kama kweli mnania thabiti ya kushika dola.
 
Mwanakijiji,

Thanks for this thread, nilikuwa na raise swali hili hili earlier today.

Katika attachment yako Professor Solinger amesema


Sasa mimi naona kama sisi ndio kwanza tunaelekea katika hiyo "critical boost" aliyoisema ya "split in the ruling party".

Sasa opposition yetu inaweza kuitumia hii nafasi vizuri au kui squander.

Mimi naamini sana katika voter education, hivi opposition wana mkakati gani na voter education?

Kuna mkuu kaja hapa over the weekend na report za kutoka vijijini huko watu wanafikiri J.S Malecela bado ni Prime Minister (mpaka nikawa siamini nikamuuliza kama anatania) utawaeleza vipi watu hawa wasipigie kura CCM?

Mimi naamini watu wakijulishwa hali vyama vya upinzani vinaweza kupata si tu wanachama wengi wapya, bali hata na viongozi wengi wenye talent na kuweza kutupa chama mbadala tunachokitaka.

Lakini upinzani priority zao ziko wapi? Program zao za voter education ziko wapi? Network zao ziko extensive kiasi gani? Policies zao ziko intuitive kiasi gani? Wanaonyeshaje tofauti za dhahiri kati yao na CCM? Wanaonyeshaje kwamba wamekomaa na wanaweza kuendesha nchi vyema zaidi ya CCM? Watatuhakikishiaje kwamba CCM hawawezi kutumia machinery ya dola kuiba kura hata kama tukiwapigia upinzani, tume ya uchaguzi ni ya CCM!

Samahani kwa kuuliza maswali mengi kuliko majibu kwa sababu na mimi sijaona majibu ya maswali haya, majibu ambayo yanaweza kuwafanya watu waweke imani katika upinzani na kuamua kuwatoa CCM.
 

CCM wanayo yote hayo uliyoyauliza?
 
CCM wanayo yote hayo uliyoyauliza?

Forget about CCM, CCM ndiyo tatizo, na CCM ndiyo incumbent, na CCM ndiyo ina electorate ya watu wanaofikiri Malecela ni PM mpaka leo. Kwa hiyo CCM wao wanachotaka ni ku maintain the status quo, kwa hiyo hawana haja ya kuleta voter education kwa sababu voter education is to their disadvantage.they would rather have an uneducated electorate in order to stay inpower.Chiligati kasema wazi juzi kwamba priority ya CCM ni ku stay in power, kwishne.

On top of that CCM wana a nationwide network, kwa hiyo at least in the network aspect jibu la swali lako ni Yes, CCM wana extensive network, je upinzani una a matching network? Tunajua upinzani ni mchanga ukilinganishwa na CCM, lakini huu ndio wakati wa kuonyesha ukomavu na kujitutumua kushindana nao, after all miaka 17 si midogo hivyo.

Ni kazi ya wapinzani na wataka mabadiliko kuleta haya mambo.Huwezi kutegemea CCM ilete voter education itakayo wa expose kwamba wao wako incompetent, it will be counterproductive to them.

Ndiyo maana nauliza ili kuwafunga magoli CCM, wapinzani wana mikakati gani kuhusu haya mambo.

Wengi tunajua historia ya upinzani Tanzania, na mheshimiwa Zitto katika post yake ya mwanzo anakuwa overly defensive unnecessarily to an extent (preaching to the choir as some would say).Yaani tunavyowasema wapinzani hapa si kwa sababu hatuwapendi, ni kwa sababu tunapenda mabadiliko, ila, pamoja na yote waliyofanya obviously it is not enough na ndiyo maana bado wao ni wapinzani.

Ndiyo maana nauliza, ili kuelevate upinzani hawa watu wana mikakati gani mipya? What are they doing differently? maana tunaweza kuwa tunazunguka katika merry go round kila miaka mitano hapa, tunapiga kelele CCM hivi, CCM vile kwa sababu tunarudia vitu vilevile kwa jinsi ile ile tukitegemea matokeo tofauti.
 

kama ambavyo wewe mheshimiwa zito ambavyo umekuwa ukitungiwa uongo,fitna na majungu na wapambe wa mbowe wanaohisi amani ya wao kutawala inahatarishwa na wewe.

Nimesikitika sana kusikia kuwa mbowe bado ana bifu la uchaguzi.umemuachia nafasi na kashinda kwa asilimia 96 bado analia kuwa anawafukuza wanachama wengine. Kweli tuna safari ndefu sana.kwenye demokrasia ya vyama mimi naona cuf wako juu kuliko utumbo anaoufanya mbowe na wenzake.
 
Upinzani Tanzania uko hivi:-
a) Sehemu ya kutokea kama ni vijana..yaani kupata vyeo, jina na hatimaye kwenda kusoma au kurudi CCM mifano mnayo wenyewe
b) Kwa watu wazima kutengeneza network na kufanya biashara na CCM kila baada ya uchaguzi (simply) kuhadaa wananchi..
c) NGO za kuchota pesa kutoka kwa wafadhili na namna nzuri ya kuongea na Rais wa Tanzania siku ya uhuru na mialiko Ikulu.
Tufanyaje??..movement within (CCM) and outside CCM iandaliwe, movement ndani ya serikali
Kivipi?...(Ndani ya CCM wapo vijana waliochoka wanaweza kuanzisha movement
Nje....(wapo vijana hususan hapa JF, Chadema and CUF ambao wananweza kuanzisha movements vuguvugu
Vijana wengi wako serikalini (walimu, civil servants, jeshini wameshachoka na haya mambo) wanaweza kuanzisha movement..
results: Not very soon it can also be painfull...
When and who: Nani aanze. mtafuteni AbdulSykes knows how to start succesfully movements..
 

Umezisikia wapi hizi habari?
 
WildCard,
Zingatia maneno ya Zitto Udikteta wa Nyerere chini ya chama Kimoja.
Kilikuepo chama cha Wafanyakazi NUTA kilikuwa na nguvu na kilikuwa tishio kwa serskali na Waajiri. Nyerere akakigeuza kuwa Bawa la TANU/CCM na kukiita JUWATA. Nao wakaanza kuhubiri Fikra za Mwenyekiti.Kuhusu Wanavyuo tumeona humu Walidiriki kuchapwa Viboko hadharani.
Vyama vya Upinzani kosa lao kubwa ambalo Mzee Mwanakijiji hakulitaja ni ukosefu wa PESA za kujiendesha na kuendeshea Kampeni za Uchaguzi wakati Unapowada. Hivyo ni sahihi pengine kwa Watanzania kujaribu kuokoa Merrikebu yenye Vinoo vya Dhahabu, na kuuacha Mtumbwi uliobeba Makopa na Unga wa Muhogo.
 
Sidhani kama hii issue ni vema tuwashushie wapinzani pekee. Hata sisi watanzania tunahusika kwa njia moja au nyingine. Kama sisi watanzania wenyewe tunaona ubabaishaji wa serikali na watendaji wake kwa nini tuendelee kuwapa dhamana ya kutuongoza??????? Silaha yetu KURA TU.

Kuna wabunge wengi wanajua uchafu wa serikali lakini wametulia tu badala ya kuiwajibisha. Na hii si wabunge wa upinzani tu bali hata CCM lakini sisi wananchi tunashindwa kuelewa kuwa hao wabunge wako pale kwa niaba ya nani. Mfano, Mh. Mwakyembe na wengineo ambao walikuwa kwenye ile kamati yake wakidai kuwa kama wabunge pamoja na Lowassa watajaribu kujitetea bungeni na kuiponda kamati ya Mwakyembe, basi Mwakyembe na wenzake wataeleza yote ambayo hawakueleza au kuweka ndani ya ripoti. Kwa misingi au sababu hiyo utaona kuwa ile ripoti haikukamilika kwa sababu kuna maneno au ukweli mwingine ulifichwa. Sasa huo ukweli ulifichwa kwa manufaa ya nani?

Mh. Zitto naye amejaribu ku-relate mabadiliko katika demokrasia pamoja na historia ya nchi. Ninakubaliana na hoja yake lakini linapokuja suala la kuwatumikia wananchi kwa uadilifu halina suala la historia ya nchi. MPs need to be responsible to the people and not their parties. Kuna thread moja Mh. Zitto aligusia mambo ya double posho kwa wabunge na vilevile alisema kuwa kuna wabunge wengine wanachukuwa pesa nyingi zilizotengwa kwa ajili ya Transportation na matengenezo ya magari yao lakini wanasafiri kwa mabasi wakiacha magari yao bila kutumia. Alisema kuwa anawafahamu hao wabunge, sasa kama unawafahamu kwa nini aendelee kukaa kimya wakati watanzania wanapoteza kodi zao kulipia HUDUMA HEWA? Suala ni uwajibikaji, it doesn't matter unawakilisha jimbo gani. Hii pesa inayochukuliwa kwa huduma hewa ingeweza kutengeneza madawati au kununua vitabu kwa ajili ya watoto wetu mashuleni.

Nimegusia pande zote, chama tawala na upinzani. Utaona kuwa kuna siri nyingi za maovu ya serikali wabunge wetu hawataki kuiwajibisha serikali. Ninaamini mtu kama Mh. Zitto atakuwa anajua kashfa nyingi kuhusu nishati na madini. Lakini anaweza kuuchubuwa na asiseme chochote akiwa na moja yake kichwani. Wabunge kazi yenu mojawapo ni kuisimamia serikali, inapokosea lazima iwajibishwe. Say all what you know, na serikali lazima tu itakuja na majibu.
 
Umezisikia wapi hizi habari?
You are the living proof,kama sample wamekuchukua wewe, median,standard variation n.k zimeangukia kwenye point inayoitwa Mwafrika.

Hakuna asiyejua jinsi unavyomchukia Zitto na upande uliokuwa kwenye uchaguzi, ulionywa hapa na watu kibao kuwa usichukue upande, nyie ndio mmenilazimisha kutuma post humu kwa lengo la kutovumilia tena upumbavu wenu, mnajuana mko wangapi humu

ila wenye kutaka facts na truth wanaongalia mstakabali wa taifa hili, wanaojadili ideas, wewe haumo humo, kama msafara wewe ni mjusi kaitika msafara wa Kenge

huu ni ukweli kataa kubali, pinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…