Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,526
- 34,057
Yoda,Natumaini wazee wako wamewakiliswa ipasavyo katika hicho kitabu
Huyo sasa ndiye mwandishi tunataka siyo wewe uandishi wako wote unatetea familia ya Kleist Sykes na wanae. Wenyewe hawajawahi kulalamika kwa kuwa JKN aliwapa fursa. Ila wewe 24/7 kupotosha historia yetu nzuri.MAKTABA IMEPOKEA: MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE PHOTOGRAPHIC JOURNEY
Rafiki yangu ndugu Ali Sultan mmoja wa watayarishaji wa kitabu hiki kikubwa cha Mwalimu jana alikuwa Ikulu Dodoma kwa uzinduzi wa kitabu hiki.
Leo kafika Maktaba kunikabidhi kitabu.
Kiswahili hakina msamiati wa kueleza shukurani zangu kwake.
"Nayajua mapenzi yako kwa Mwalimu," kaniambia akinikabidhi hazina hii.
Kitabu hiki kina historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika katika picha na maelezo.
Yapo mengine mengi katika maisha ya Mwalimu.
Maneno hayatoshi kueleza yaliyomo ila uwe na kitabu hiki wewe mwenyewe mkononi unafungua ukurasa baada ya ukurasa.
Hakika kazi kubwa imepitika.
Tuna deni kubwa kwa waandishi wa kitabu hiki ambalo si rahisi kulilipa.
View attachment 3317692
Muuliza swali alitaka kujua kama jina Sykes limo cc YodaYoda,
Wazee wangu ni kitu kingine kabisa katika historia ya Mwalimu.
Endapo nitakuwekea picha nilizonazo kwenye Maktaba na nikakuwekea maelezo nina hakika utashangaa kupita kiasi.
Kuna picha ya Mwalimu Nyerere Maktaba ambayo nimepewa na marehemu Maulidi "Chubby," Tosiri inamuonyesha Mwalimu aneshika mkuki na ngao.
Nadhani hii ni katika picha za mwanzo sana za Nyerere baada ya kuundwa TANU 1954.
Maulidi ni mtoto wa Iddi Tosiri ambae kadi yake ya TANU ni no. 25 na alihudhuria mkutano wa kwanza wa TANU August 1954 Arnautoglo Hall.
Katika Photographic Journey ipo picha ambayo Iddi Tosiri yupo na Mwalimu na wanachama wengine wa TANU, New Street.
Picha hii ipo Maktaba na nilipewa pia na marehemu Maulid Tosiri.
Picha nyingine ya zamani sana ya Mwalimu katika TANU nilipewa na Faiz Mafungo, mtoto wa Iddi Faiz Mafungo.
Huyu Iddi Faiz Mafungo na Iddi Tosiri ni ndugu na kadi yake ya TANU ni No. 24 na alihudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Arnautoglo.
Iddi Faiz Mafungo ni Mweka Hazina wa kwanza wa TANU na pia alikuwa Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).
Picha hii niloyopewa na Faiz Mafungo imepigwa Dodoma mwaka wa 1955 au 1956.
Inamwonyesha Mwalimu, Iddi Faiz Mafongo, Sheikh Mohamed Ramiyya, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Iddi Taratibu.
Iddi Tosiri, Iddi Faiz Mafongo na Sheikh Mohamed Ramiyya hawa watatu ni ndugu na Iddi Tosiri na Iddi Faiz Mafongo ndiyo waliompeleka Nyerere Bagamoyo mguu kwa mguu kumjulisha kwa Sheikh Mohamed Ramiyya.
Picha nyingine ya zamani mwanzoni inaundwa TANU niliipata kwa Jim Bailey ilipigwa mwaka wa 1955 uwanja wa ndege safari ya kwanza ya Nyerere UNO.
Hizi ni picha mbili.
Nyingine yuko Nyerere na Iddi Faiz Mafungo hapo uwanja wa ndege.
Iddi Faiz Mafongo ndiye alikuwa mkusanyaji wa fedha za safari ya UNO.
Picha hii yuko Mwalimu, Bi. Chiku bint Said Kisusa (mke wa Shariff Abdallah Attas, Tatu bint Mzee, Bibi Titi Mohamed na Lucy Lameck.
Nina picha ya 1955 nilipewa na Bilal Rehani Waikela Nyerere yuko Tabora pamoja na Titi Mohamed, Bilal Rehani Waikela na wanachama wa New Young Strong Team katika juhudi ya kuunda TANU.
Yapo mengi.
Top Gear,Bookshop kinapatikana?
Stuxnet,Huyo sasa ndiye mwandishi tunataka siyo wewe uandishi wako wote unatetea familia ya Kleist Sykes na wanae. Wenyewe hawajawahi kulalamika kwa kuwa JKN aliwapa fursa. Ila wewe 24/7 kupotosha historia yetu nzuri.
Najuwa machungu na husda uliyonayo moyoni japo umekipokea
Asante sana Mkuu.Top Gear,
Nasikia kipo Mkuki na Nyota.
Njinjo,Muuliza swali alitaka kujua kama jina Sykes limo cc Yoda
Tunasubiri Lissu anyongwe na Samia, ili wajukuu zako waje kuandika mchango wa wazee wako kwenye mageuzi ya mfumo wa uchahuzi na vita dhidi ya ubaguzi, ufisadi, dhulma na mauajiYoda,
Wazee wangu ni kitu kingine kabisa katika historia ya Mwalimu.
Endapo nitakuwekea picha nilizonazo kwenye Maktaba na nikakuwekea maelezo nina hakika utashangaa kupita kiasi.
Kuna picha ya Mwalimu Nyerere Maktaba ambayo nimepewa na marehemu Maulidi "Chubby," Tosiri inamuonyesha Mwalimu aneshika mkuki na ngao.
Nadhani hii ni katika picha za mwanzo sana za Nyerere baada ya kuundwa TANU 1954.
Maulidi ni mtoto wa Iddi Tosiri ambae kadi yake ya TANU ni no. 25 na alihudhuria mkutano wa kwanza wa TANU August 1954 Arnautoglo Hall.
Katika Photographic Journey ipo picha ambayo Iddi Tosiri yupo na Mwalimu na wanachama wengine wa TANU, New Street.
Picha hii ipo Maktaba na nilipewa pia na marehemu Maulid Tosiri.
Picha nyingine ya zamani sana ya Mwalimu katika TANU nilipewa na Faiz Mafungo, mtoto wa Iddi Faiz Mafungo.
Huyu Iddi Faiz Mafungo na Iddi Tosiri ni ndugu na kadi yake ya TANU ni No. 24 na alihudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Arnautoglo.
Iddi Faiz Mafungo ni Mweka Hazina wa kwanza wa TANU na pia alikuwa Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).
Picha hii niloyopewa na Faiz Mafungo imepigwa Dodoma mwaka wa 1955 au 1956.
Inamwonyesha Mwalimu, Iddi Faiz Mafongo, Sheikh Mohamed Ramiyya, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Iddi Taratibu.
Iddi Tosiri, Iddi Faiz Mafongo na Sheikh Mohamed Ramiyya hawa watatu ni ndugu na Iddi Tosiri na Iddi Faiz Mafongo ndiyo waliompeleka Nyerere Bagamoyo mguu kwa mguu kumjulisha kwa Sheikh Mohamed Ramiyya.
Picha nyingine ya zamani mwanzoni inaundwa TANU niliipata kwa Jim Bailey ilipigwa mwaka wa 1955 uwanja wa ndege safari ya kwanza ya Nyerere UNO.
Hizi ni picha mbili.
Nyingine yuko Nyerere na Iddi Faiz Mafungo hapo uwanja wa ndege.
Iddi Faiz Mafongo ndiye alikuwa mkusanyaji wa fedha za safari ya UNO.
Picha hii yuko Mwalimu, Bi. Chiku bint Said Kisusa (mke wa Shariff Abdallah Attas, Tatu bint Mzee, Bibi Titi Mohamed na Lucy Lameck.
Nina picha ya 1955 nilipewa na Bilal Rehani Waikela Nyerere yuko Tabora pamoja na Titi Mohamed, Bilal Rehani Waikela na wanachama wa New Young Strong Team katika juhudi ya kuunda TANU.
Picha nyingine ni ya 1956 safari ya pili ya Mwalimu UNO imepigwa Arnautoglo Hall dhifa ya kumuaga Mwalimu yuko Abdulwahid Sykes, Nyerere, Dossa Aziz na Nangwanda Lawi Sijaona.
Picha hii alinipa mtoto wa Abdul Sykes, Kleist Sykes.
Nyingine Mwalimu yuko Shambani kwa Chaurembo, Mtoni 1956 kwenye dua ya kuomba salama kwa harakati za kudai uhuru.
Dua hii ilifanyika baada ya watu kutoka Hijja na ilihudhuriwa na masheikh wengi na watu maarufu wa mji wa Dar-es-Salaam.
Picha hii alinipa Mohamed Chaurembo sasa yapata miaka 40 lakini maelezo ya picha nilipata kwa Sheikh Iddi Chaurembo mtoto wa Sheikh Abdallah Iddi Chaurembo.
Yapo mengi.
Kijakazi,nina swali nje ya mada kidogo, kwa nini waislamu wanapenda sana communism? i mean, hata walioleta communism tanzagiza ni waislamu, je, kuna uhusiano wowote kati ya uislamu na communism? kwa maana ukiangalia karibia nchi zote zenye waislamu wengi kuna commumism …
Huo sasa ni uchuro. Unatoka nje ya biti kizembeTunasubiri Lissu anyongwe na Samia, ili wajukuu zako waje kuandika mchango wa wazee wako kwenye mageuzi ya mfumo wa uchahuzi na vita dhidi ya ubaguzi, ufisadi, dhulma na mauaji
Nmaanisha hawa wahuni baada ya mwaka 1961 waliona wamemaliza.Huo sasa ni uchuro. Unatoka nje ya biti kizembe
Hongera mwanahistoria naamini kuna mchango wako kwenye hicho kitabu.MAKTABA IMEPOKEA: MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE PHOTOGRAPHIC JOURNEY