Mwaki...
Kitabu hicho hapo chini kina kurasa 30.
Nimekisoma chote kwa muda mfupi sana.
Kinaeleza maisha ya Songea Mbano.
Unaweza ukajiuliza huyu Songea Mbano ndiye huyu aliyeandika barua kwa Sheikh Sultan Mataka bin Hamin Massaninga?
Huu ulikuwa wakati wa vita na barua hii aliandika kutafuta msaada wa kupigana na Wajerumani.
Katika barua hii anamtaja Chinyalanyala ambae jina lake la kwanza ni Omar.
Halikadhalika anamtaja pia Hassan bin Ismail na Kazembe.
Kazembe (51) alikuwa Nduna ila Hassan Ismail (53) alikuwa raia wa kawaida.
Hizo ni namba zao katika mnara wa majina ya walionyongwa na Wajerumani.
Kitabu hiki kimeniongezea taarifa muhimu katika historia ya Nduna Abdulrauf Songea Mbano.