Maktaba kuu ya Arusha

Maktaba kuu ya Arusha

lulu za uru

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2015
Posts
2,557
Reaction score
3,221
Kazi iendelee...

Maktaba kuu ya Arusha, kisima cha maarifa uliyebeba mengi...

Safari za ushindi za watu machozi yao na furaha, historia ya tangu kuumbwa kwa dunia hata leo kaskazini kusini mashariki na magharibi jamani wahusika ipakeni rangi hii maktaba kwa nje rangi imechoka mno maktaba inaonyesha haijafanyiwa renovation miaka na miaka ni aibu kwa Arusha.
 
Naunga mkono ushauri huu. Ya Kilimanjaro hivi majuzi wameipaka rangi imependeza sasa.

Nafikiri KNCU ndio ilikuwa inailea Maktaba ya Moshi na ARCU ndio ilikuwa inailea ya Arusha.

Serikali au Manispaa ya Arusha washughulikie hili.
 
Ni aibu sana sidhani kama rangi itamaliza million 30 kwa serikali hiyo ni pesa ndogo sana..duhhh fedheha hii pigeni hata rangi tu...kwanza...
 
Kwenye miaka ya 1980s maktaba ya mkoa wa Kilimanjaro ilikua kimbilio la wenye kupenda kujisomea. Ilikua imesheheni vitabu vya taaluma mbalimbali, vitau vya kiada na ziada, vitabu vya hadithi na maarifa lukuki

Watu wazima na wanafunzi walifika kujisomea pale pale na pia kwa wale waliokua wanachama waliruhusiwa kuazima na kwenda kujisomea nyumbani

Haya ni mambo ambayo hlitakiwa yatiliwe mkazo na Serikali kuu au hata Halmashauri zetu kwa kujenga na kusimamia Maktaba za kujisomea vitabu angalau kwa kila Wilaya nchini. Kwa namna hiyo tutarejesha utamaduni wa watu hasa watoto na vijana kujisomea na kujiongezea maarifa
 
Watu wa kaskazini wanapenda sana kusoma, ndiyo maana nyerere aliwaona kama threat kwenye uongozi wake, labda aliona wangeleta mabadiliko makubwa nchini na legacy yake ingepotea
 
Ile maktba imechoka. Kwa nje haina hata mvuto sijui kwa ndani itakuwaje
 
Enzi hizo nimen'goa sana mamanzi pale. Nikiwazogeza tuu pale Pizza Hut basi inakuwa imeisha hiyo.
 
Mimi nimeitumia sana nikiwa form four Arusha secondary miaka ya 2004, pale kwa utulivu ni sehemu sahihi ila kwa maswala ya usalama hapafai
Kwa eneo kama eneo si pabaya, pametulia na kuhusu usalama unafikiri majambazi wataenda kuiba nini mle ndani? Isitoshe yale maeneo hayapo mbali na Central Police ya Arusha, ndio mana hata benki nyingi zipo kwenye line ile.
 
Back
Top Bottom