Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,526
- 34,057
MAKTABA: MUHIDIN ISSA MICHUZI NA PICHA ALIZOPIGA MAREHEMU MOHAMED SHEBE
Leo Maktaba imewapokea wapiga picha maarufu na wakubwa katika nayakati zao Muhid ''Ankal'' Issa Michuzi na Mohamed Shebe.
Muhidin Issa Michuzi amefika mwenyewe wakati Mohamed Shebe zilizokuwapo ni mkusanyiko wa picha alizopiga katika uhai wake kuanzia miaka ya 1950.
Historia ya picha za Mohamed Shebe zinaanza na historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika kumfanya yeye kuwa mtu wa kwanza kurekodi katika picha harakati za TANU na tunathubutu kusema kuwa kazi hii imemfanya yeye Mohamed Shebe kuwa mtu wa kwanza kumpiga picha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipoanza harakati za kuongoza mapambano dhidi ya ukoloni wa Muingereza.
Jina la Mohamed Shebe nimelisikia kwa mara ya kwanza katika miaka ya 1980 nilikuwa nimekwenda Kinondoni Mtaa wa Sekenke nyumbani kwa mama yangu Bi. Mwanaisha bint Mohamed.
Baada ya kumwamkia akaniambia, ''Baba Mzee Mohamed hebu panda hapo juu tungua hizo picha.''
Katika picha hizo kulikuwa na picha nikiipenda sana.
Niko tumbo wazi nimekaa nina umri wa kiasi cha mwaka mmoja hivi.
''Chukua picha zako hizo.''
Mama yangu alikuwa mgonjwa.
Alikuwa anajua kuwa hana muda mrefu wa kuishi.
''Chukua picha zako nimekuwekea kaa nazo mwenyewe.''
''Picha hii kanipiga nani?''
Nilikuwa nimeishika mkononi picha ile yangu ambayo ilipigwa mwaka wa 1953.
''Picha hiyo kakupiga rafiki yako Shebe. Studio yake ilikuwa pale Livingstone na KIpata ikitazamana na nyumba tuliyokuwa tukikaa.''
Kisa kirefu.
Hivi ndivyo nilivyokuja kumuuliza Mbaraka Shebe mfayakazi mwenzangu Bandarini kama anauhusiano na Mohamed Shebe aliyekuwa na studio Mtaa wa Livingstone na Kipata.
''Huyo ni baba yangu mzazi.''
Mohamed Shebe alikuwa keshafariki.
Mbaraka Shebe akanifanyia nakala ya picha katika Maktaba ya Picha alizopiga baba yake akanipa.
Huu ni mkusanyiko wa picha ambazo sasa zinafikisha umri wa zaidi ya miaka 70.
Sikufanya khiyana picha hizo nimezitumia katika makala zangu nyingi na nikieleza chanzo chake.
Baada ya miaka mingi kupita juzi Mbarak Shebe kaja nyumbani kwangu na picha halisi akanambia kuwa nafsi yake inampa shida kukaa na picha zile ambazo kwa hakika ni hazina na kumbukumbu ya historia ya Tanganyika.
Anaona picha zile zinastahili kuwa katika Maktaba yangu.
Sikuwa na maneno ya kusema.
Kinywa kilinijaa mate.
Unamshukuru vipi mtu wa namna hii?
Nilirudi nyuma miaka mingi nikijaribu kuleta picha siku Mzee Mohamed Shebe somo na rafiki yangu alipokuja nyumbani kunipeleka kwenye studio yake kunipiga picha.
Mama anasema alinibeba mwenyewe hadi kwenye studio yake.
Mwaka wa 1953 baada ya mwaka mmoja TANU inaundwa na Mzee Shebe anapiga picha za mikutano ya TANU Mnazi Mmoja.
Katika picha hizo kuna picha inaonyesha uwanja wa Mnazi Mmoja na huo Mnazi Mmoja wenyewe.
Kuna pia sehemu ambayo ilitengwa makhususi walikuwa wanakaa akina mama watupu.
Sehemu hii katika picha iko mkono wa kushoto utaona rangi nyeusi imetanda kote.
Hayo ni mabaibui waliyokuwa wakivaa mama zetu wamekuja kumsikiliza Julius Nyerere nakuitia shime mikutano ya TANU.
Picha hizi nikaiambia nafsi yangu mimi sina ujuzi wa kuzihifadhi kama inavyostahili.
Lazima nimwite ndugu yangu Muhidin Issa Michuzi nimkabidhi yeye.
Lakini nimemwambia Ankal.
Hivi nchi hii itamlipa nini marehemu Mohamed Shebe kwa kuhifadhi historia ya Mwalimu Nyerere na harakati za uhuru?
Hivi nchi hii itawalipa nini wanae kwa kutufanyia hisani hii ya kutupa maktaba ya mkusanyiko wa picha alizopiga baba yao?
Subiri uzione picha hizi.