Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Lord...Mzee Mohamed Said napata wapi kitabu cha 'Maisha na Nyakati za Abdulwaheed Sykes'? Kuna mtu huko Dar nataka nimwagize aninunulie. Mimi niko mikoani.
Njiwa,Mwalimu Mohamed Said unaacha alama kubwa sana .. mchango wako watakuja kuutambua pindi ukiondoka.. usisikitike na kukataa tamaa binaadamu ndivyo alivyo endelea kutuelimisha .. mitandao inahafadhi kamwe haitasahau
Joka....
Asante sana Mkuu.Lord...
Kitabu kinapatikana Ibn Hazm Media Centre katika maduka yake ya kuuza vitabu Msikiti wa Mtoro, Manyema Mtambani na Kichangani.
Kipo kwa Kiswahili na Kiingereza bei shs: 10,000.00.
Joka....
Kitabu cha Sivalon cha nini hapa?
JK,..nimesikia wanazuoni mbalimbali wakikitaja kitabu cha John Sivalon na hali hiyo imenifanya nitamani kukisoma.
..pia vitabu vya Aboud Jumbe,Ally Hassan Mwinyi, Ben Mkapa, Edwin Mtei, Andy Chande, Al-Nuur Kassum, ...vyote natamani kuvisoma ili kuifahamu zaidi Tanzania yetu.
JK,
Wanazuoni hao wanasema nini kuhusu kitabu cha Sivalon?