Maktaba ya Mohamed Said na Maswali ya Wasomaji

Maktaba ya Mohamed Said na Maswali ya Wasomaji

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Wana JF Jukwaa la Historia,
Nimekuwa nikifanya majadiliano hapa sasa huu ni mwaka wa 11.

Nimegundua kuwa kuna wafuatiliaji wengi wa mijadala hii yetu ambayo wanauliza maswali ambayo kwa hakika nishayajibu mara nyingi sana.

Kwa nia ya kuondoa tatizo hili na kwa nia ya kusambaza elimu kwa wote bila khiyana naweka link hapo chini ya YouTube yangu ambayo nimezungumza mengi.

Ikiwa mathalan msomaji anataka kujua historia ya TANU, AMNUT, UTP au historia ya Zuberi Mtemvu, John Rupia, Bibi Titi Mohamed anachotakiwa kufanya ni kuingia kwenye link na kuandika jina kutafuta:

1714453422914.jpeg

Kambi ya Kipumbwi, Tanga 2003

www.youtube.com/@samitungo
 
Mwalimu Mohamed Said unaacha alama kubwa sana .. mchango wako watakuja kuutambua pindi ukiondoka.. usisikitike na kukataa tamaa binaadamu ndivyo alivyo endelea kutuelimisha .. mitandao inahafadhi kamwe haitasahau
 
Mzee Mohamed Said napata wapi kitabu cha 'Maisha na Nyakati za Abdulwaheed Sykes'? Kuna mtu huko Dar nataka nimwagize aninunulie. Mimi niko mikoani.
Lord...
Kitabu kinapatikana Ibn Hazm Media Centre katika maduka yake ya kuuza vitabu Msikiti wa Mtoro, Manyema Mtambani na Kichangani.

Kipo kwa Kiswahili na Kiingereza bei shs: 10,000.00.
 
Mwalimu Mohamed Said unaacha alama kubwa sana .. mchango wako watakuja kuutambua pindi ukiondoka.. usisikitike na kukataa tamaa binaadamu ndivyo alivyo endelea kutuelimisha .. mitandao inahafadhi kamwe haitasahau
Njiwa,
Ahsante sana.
 
Joka....
Kitabu cha Sivalon cha nini hapa?

..nimesikia wanazuoni mbalimbali wakikitaja kitabu cha John Sivalon na hali hiyo imenifanya nitamani kukisoma.

..pia vitabu vya Aboud Jumbe,Ally Hassan Mwinyi, Ben Mkapa, Edwin Mtei, Andy Chande, Al-Nuur Kassum, ...vyote natamani kuvisoma ili kuifahamu zaidi Tanzania yetu.
 
JK,
Wanazuoni hao wanasema nini kuhusu kitabu cha Sivalon?
 
Back
Top Bottom