Tetesi: Makubaliano CHADEMA/ACT Wazalendo: Membe kumsapoti Lissu kisha kuteuliwa kuwa Waziri wa Nje

Tetesi: Makubaliano CHADEMA/ACT Wazalendo: Membe kumsapoti Lissu kisha kuteuliwa kuwa Waziri wa Nje

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
40,455
Reaction score
73,145
Kumekucha. Habari zilizovuja ni kuwa kuna makubaliano yamefanyika kati ya ACT na Chadema kuwa upande wa Zanzibar CHADEMA itaingiza nguvu zake kumsapoti Maalim Seif katika pambano la Urais nao ACT Wazalendo watawaunga mkono CHADEMA katika Urais huku bara kwa maana ya Serikali ijayo ambayo kimahesabu itaundwa na Lissu iwe ya ushirikiano na Membe ambaye hatagombea tena abaki kama mshauri wa Lissu kwa sasa na baadae kuja kupewa Wizara ya Mambo ya Nje kwani huko amebobea.

Hakika mambo ni mengi muda mchache. Ila yako Bambam. Naiona Tanzania ya furaha kwa mbaaaali inakuja.
 
Kwahiyo Chadema wamesamehe majimbo 50 ya Zanzibar? Na bara majimbo 65 hawajasimamisha wagombea, bado act kaweka wagombea nchi nzima. Bado watakaonyanganywa kura kama kafulila, hii Ni technical nockout
 
Mwaka 2015 wanajeshi walivamia ofisi za ZEC mchana kweupe na "kumteka" Jecha na wote mnajua kilichofuata

Mpinzani hawezi kupewa urais kwenye plate Africa hii. Kenya hapo karibu tu ni mfano. Hata Malawi watu waliandamana zaidi ya miezi minne na kuuawa sana tu mpaka tume huru ikaundwa.
 
Mkuu Chakaza Banaa Naona Kweli Mambo Ya Kurusha Roho Watu Yameshika Kasi

Watie Hofu TU😁😁
 
Back
Top Bottom