Makubaliano kati ya Serikali na kampuni ya madini ya Barrick, yametekelezwa kwa kiwango gani mpaka sasa?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Naomba kujua hawa wanaume wa kampuni ya Madini ya Barrick wametekeleza makubaliano gani mpaka sasa maana tuliahidiwa mengi na makubwa ila kwa sasa ukimya umetawala tofauti na kilichokuwa kinahubiriwa majukwaani.

Kwa mfano, ujenzi wa smelter umeshaanza? Na kama umeanza, umefika asilimia ngapi ya utekelezaji?

Vipi kuhusu ile economic benefit ya 50 kwa 50?

Yako mengi tu ila kwa sasa siyasikii tena na sijui hata katika hili Bunge lililoisha majuzi kuna lolote lilijadiliwa kuhusu makubaliano haya

Mwenye majibu tafadhali.

Waandishi wa Habari wa nchi wa siku hizi wanafeli vibaya sana na wameacha wanasiasa ndio wawasetie agenda za kuandika na kuripoti.

Pathetic!
 
Mkuu, wewe ndio uliwaahidi Kijijini kwenu kwamba utarudi na Noah za makinikia? JPM alikuchota akili, nenda Kijijini kasalimie ndugu na jamaa, Kisha waeleze, watakuelewa
 
Nilisoma sehemu kwamba makinikia yalizuiliwa kimakosa.
Ndio imeisha hiyo. Nguvu kubwa na rasilimali fedha iliyotumika kwenye hili swala vimeishia kuwa ni hasara kwa nchi na wananchi wake.

Huu ni sawa na uhujumu uchumi tu hasa nikifikiri vile vikao vya majadilioni na tija iliyopatikana naona ni sawa tu na kuhujumu nchi.
 
Usicheze na beberu aisee
Beberu katupiga na kitu kizito licha ya kukaa nae kwenye mazungumzo kwa karibu miezi mitatu huku wahusika wa majadilioni wakiwa wamejifugia pasipo kuruhusu watu wasiohusika kuwasogelea.

Mpaka sasa sioni tija ya ile nguvu ya iliyotumika pamoja na vile vikao vilivyochukua karibu miezi mitatu kama sikosei.
 
Twiga mining corporation inasimamia mambo uliyotaja ikiwemo 50/50 nimeona kwenye mgodi BARRICK
NORTH MARA.
 
Miezi 8, aiyo 3.
 
Twiga mining corporation inasimamia mambo uliyotaja ikiwemo 50/50 nimeona kwenye mgodi BARRICK
NORTH MARA.
Ni nini ulichokiona? Ilikuwa awamu ya usanii mwingi, sawa na tulivyoaminishwa kuwa ni donor country. Wajinga waliamini, wenye akili walijua ni hadithi sawa na zile za wti hapo zamani za kale wanyama wote walikubaliana kufanya mkutano. Mwenyekiti wao, Simba, akawaambia, ...
 
Naomba kujua hawa wanaume wa kampuni ya Madini ya Barrick wametekeleza makubaliano gani mpaka sasa maana tuliahidiwa mengi na makubwa ila kwa sasa ukimya umetawala tofauti na kilichokuwa kinahubiriwa majukwaan
Kwa hiyo kwako Barrick ndiyo unawaita wanaume. Wewe ni mwanamke!!! Unapenda sana kuwalamba wazungu makalio yao. Kila siku unasifia wazungu.
 
Panya mabaka alijifanya muongeaji mkuu katika mkutano wa Panya kumbe paka alikuwa juu alipo ruka moja kwa moja akamshika panya mabaka panya wote walitawanyika kwa mbali alisika mfalme akisema "mkutano umehailishwa mpaka siku Nyingine"

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
K

Kwa hiyo kwako Barrick ndiyo unawaita wanaume. Wewe ni mwanamke!!! Unapenda sana kuwalamba wazungu makalio yao. Kila siku unasifia wazungu.
Kumbe hujui hata ni nani aliwaita hao Barrick wanaume. Unajichora tu unaonekana hujui vizuri hii issue.

Acha kuropoka wakati huna unalojua.
 
Naomba kujua hawa wanaume wa kampuni ya Madini ya Barrick wametekeleza makubaliano gani mpaka sasa maana tuliahidiwa mengi na makubwa ila kwa sasa ukimya umetawala tofauti na kilichokuwa kinahubiriwa majukwaani...
Kuongezea walìpo peleka yale makinikia mbona hatukuelezwa ni kiasi gani cha madini kilikutwa huko au ilikuwa kweli ni professorial rubbish?
 
Naomba kujua hawa wanaume wa kampuni ya Madini ya Barrick wametekeleza makubaliano gani mpaka sasa maana tuliahidiwa mengi na makubwa ila kwa sasa ukimya umetawala tofauti na kilichokuwa kinahubiriwa majukwaani...
Wakikujibu unistue. Kwani kile kishika uchumba walipata?
 
Naomba kujua hawa wanaume wa kampuni ya Madini ya Barrick wametekeleza makubaliano gani mpaka sasa maana tuliahidiwa mengi na makubwa ila kwa sasa ukimya umetawala tofauti na kilichokuwa kinahubiriwa majukwaani.

Kwa mfano, ujenzi wa smelter umeshaanza? Na kama umeanza, umefika asilimia ngapi ya utekelezaji?

Vipi kuhusu ile economic benefit ya 50 kwa 50?

Yako mengi tu ila kwa sasa siyasikii tena na sijui hata katika hili Bunge lililoisha majuzi kuna lolote lilijadiliwa kuhusu makubaliano haya

Mwenye majibu tafadhali.

Waandishi wa Habari wa nchi wa siku hizi wanafeli vibaya sana na wameacha wanasiasa ndio wawasetie agenda za kuandika na kuripoti.

Pathetic!
Usiwalaumu waandishi ndugu,hawana vyombo vyao wenyewe
 
Back
Top Bottom