Strong ladg
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 1,357
- 3,114
Makumbusho yaliyojengwa kwa ajili ya kumbukumbu ya Kapteni Thomas Sankara na wenzake 12 waliouwawa pamoja hatimaye yamezinduliwa rasmi.
Makumbusho hayo yamezinduliwa mnamo tarehe 17 Mei 2025 katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi wa Burkina Faso na wale waliotoka nchi jirani kama vile Senegal na Chad.
Makumbusho hayo yamejengwa mahali ambapo mauaji ya Thomas Sankara na wenzake yalitokea mnamo mwezi Oktoba mwaka 1987.
Licha ya umuhimu wa Thomas Sankara katika historia ya Burkina Faso, makumbusho haya ya kumuenzi yamejengwa miaka zaidi ya 30 baada ya kifo chake kwa sababu kwa muda mrefu nchi ya Burkina Faso ilikuwa chini ya uongozi wa Blaise Compaoré ambaye alihusika na kifo cha Thomas Sankara.