Makundi 7 ya watu wanaoheshimiana sana Tanzania. Nini siri yake?

Makundi 7 ya watu wanaoheshimiana sana Tanzania. Nini siri yake?

Kila jamaa ktk jamii wanaheshimiana as long as wanakinywea kikombe kimoja.

Maskini anamkubali maskini mwenzake,simple tu maskini hampendi tajiri utasikia yule ni freemason sijui anachukua misukule alimradi aonyeshe kutokubaliana nae.
 
Kuna makundi ya watu wakikutana mahali wanaheshimiana sana. Mimi nimeona makundi yafuatayo, je kuna siri gani?
1. Wachawi
2. Washirikina
3. Wanasiasa
4. Wanajeshi
5. Polisi
6. Wafanyabiashara wakubwa
7. Viongozi wa dini
8. Mateja
9. Madalali
10. Matapeli
11. Mafundi
Ongeza na wana Yanga...
Huwa wananchi tukikutana tunaheshimiana sana
 
Great thinkers, no time to prove our worth 😎
20230411_195719.jpg
 
Mtoto wa kike na baba yake, wana bond special sana
20230411_200241.jpg
 
Kuna makundi ya watu wakikutana mahali wanaheshimiana sana. Mimi nimeona makundi yafuatayo, je kuna siri gani?
1. Wachawi
2. Washirikina
3. Wanasiasa
4. Wanajeshi
5. Polisi
6. Wafanyabiashara wakubwa
7. Viongozi wa dini
8. Mateja
9. Madalali
10. Matapeli
11. Mafundi

Madaktari usiwasahau
Ukisikia wanaitana chief kaa mbali
 
Hapo kwenye 3,4,5,7 nadhani hauk sawa.

Kwanza lazima ujengewe uwezo wa kutofautisha kati ya kuheshimiana na kuogopana( nidhamu ya woga).

Kuheshimiana hakufundishwi ama kulazimishwa bali kunatoka ndani ya moyo wa mtu.

Heshima lazima iambatane na upendo, kuchukuliana na kuvumiliana kutoka moyoni bila kushurutishwa na sheria za kada husika.

Sasa nije katika hayo makundi.

3. Wanasiasa, hawa hawaheshimiani hata kidogo na wala hawapendani labda kama hukumaanisha wanasiasa wa dunia hii(fuatilia maana mifano ni mingi ya kurogana,kutoleana lugha chafu,kusingiziana,kuumbuana,kudhalilishana nk.

4 na 5
Askari wote hawaheshimiani bali wanaogopana. Jeshini unashurutishwa ukiwa mdogo kwa cheo umtii mkubwa kwa cheo, hapa umri wako ama nafasi ya mtu katika jamii haina mahali pake. Mf. Askari mwenye cheo cha juu anaweza kumpigisha deki au kumrusha kichurachura askari mwenzake wa cheo cha chini mbele ya kadambasi ama mkewe hata kama hakuna ulazima wa kufanya hivyo, ama mdogo ukawekwa mahabusu mpaka akili ikukae.

Majeshini kuna nidhamu ya kuogopana, mkubwa dhidi ya mdogo. Amri inatoka juu kwenda chini bila kuhoji ama kujadili.(rejea Kigwangala anawarusha kichura chura askari wanyamapori mbele ya kadamnasi kwa kutaka misifa na ujiko tu kwenye kamera) na hawatakiwi kuhoji wala kulalamika hadharani.

Kwenye mess hakuna kuchanganyika kati ya maofisa na askari wa chini.

7.Viongozi wa dini, Heshima ipo endapo wote ni dhehebu moja.Yakiwa madhaehebu tofauti ama dini tofauti hakuna kuheshimiana zaidi ya kuchambana.

Hawa hawaheshimiani na ndio maana hawaaminiani. Hawa kila mmoja anamwita mwenzake tapeli.

Abiria wa usafiri wa bajaji.
Hawa huheshimiana kiasi fulani, 1.Kwanza ukiingia kwenye bajaji akaja mwenzako unasogea bila kusogezwa na mtu

2. Mara nyingi anapoingia abiria mpya husalimia abiria wenzake aliowakuta ndani.

3.Subira na kuvumiliana.
Wanavuta subira kuwasubiri wenzao ili safari ianze, hawatoi lugha chafu. Hatanunaposhuka taratibu hawanung'uniki

4.Upendo
Wakati mwingine ukipanda bajaji na mzigo, abiria waliotangulia kupanda kabla yako hutokea wakakupokea mzigo na kuupachika nyuma ya chombo wakati huo wakisogea kukuachia nafasi ili ukae vizuri.

Tofauti na abiria wa daladala ambao wakishapanda daladala hawataki kusogea ili mwenzao apate nafasi, hata konda akiwaomba wasogee kutoa nafasi huishia kutoa lugha ya matusi. Yaani abiria akishapanda yeye tu hataki mwingine apate nafasi, akisha panda yeye anataka hapohapo gari liondoke limpeleke yeye tu hao wengine wajibebe!

Kundi jingine linaloheshimiana kwa dhati ni walevi ama watu wa mvinyo.
Hapa siongei sana. Takwimu ziko wazi.
 
Kuna makundi ya watu wakikutana mahali wanaheshimiana sana. Mimi nimeona makundi yafuatayo, je kuna siri gani?
1. Wachawi
2. Washirikina
3. Wanasiasa
4. Wanajeshi
5. Polisi
6. Wafanyabiashara wakubwa
7. Viongozi wa dini
8. Mateja
9. Madalali
10. Matapeli
11. Mafundi

12. Watu wasiojulikana
 
Back
Top Bottom