Makundi 9 ya wapiganaji yaungana dhidi serikali ya Ethiopia

Makundi 9 ya wapiganaji yaungana dhidi serikali ya Ethiopia

S
SPONSOR NI USA NA UK .

Ethiopia ilikuwa inakua kwa speed ya hatar , so ili kustop , suluhisho ni vurugu ka hizo.
Sidhani kama utapata suluhu kwa kuwatupia wengine shutuma kwa matokeo ya matendo yako.Kaa chini ujiulize kwanza,weye umechangia au ni sababu kiasi gani kwa kinachoendelea au kilichotokea.Tuache visingizio.Mchawi unaye kiunoni mwako.
 
Ukiona marekani anaondoa watu wake ujue utawala huo wa sehemu husika umeanguka
 
Aliyemloga mwafrika ni mwafrika mwenzake .....

[emoji654]WATIGRAY WANASAPOTI KUBWA SANA NYUMA YAO.....

[emoji654]FALL OF ETHIOPIA AND RISE OF TIGRAY SOCIETY ....mda utaongea
Hawana saport yeyote hawa WaTigray. Ila walizaliwa kuwa wapambanaji toka enzi na enzi kuna Menelik ushamsikia alikuwa balaa. Wanafaham sana guerilla warfare
 
Ana maana iwapo waasi watashinda basi wawe waungwana,wasimfanyie dhalili abiy.Ndo maana ya kufanya Uislam kwa lugha ya mtaani.
Sasa wewe ndugu yetu unahamanika na kuwaambia watu akili kisoda ilhali ni ugeni wako tu wa mji.
Ukiangalia kwa yanayotokea huko Pakistan, Afghanistan, Somalia etc ambako ndio nyumbani kwa Uislam utagundua hata hiyo maana ya mtaani ina walakini.
 
Alichojaribu kukufanya Abiey Nyerere alikiweza miaka 60 iliyopita, Afrika ukabila unatuharibia sana...

kilichoivunja Somalia ni Ukabila na mambo ya koo, vita ya sasa ya Ethiopia ni Ukabila, kilichoivunja Sudan ni ukabila...

Rwanda, Burundi, Kenya haya ni mabomu ambayo inabidi tuwe nayo makini sana. muda wowote Yanalipuka
 
Abiy Ahmed ni mtu imara sana,hao vibaka watanyoosha mikono sio mda
 
SPONSOR NI USA NA UK .

Ethiopia ilikuwa inakua kwa speed ya hatar , so ili kustop , suluhisho ni vurugu ka hizo.
Ethiopia ilibugi tu kuanza bifu na misri, kuhusu maji,, sasa watamtoa na hiyo nchi inaweza kumeguka vipande vipande
 
Ethiopia ilibugi tu kuanza bifu na misri, kuhusu maji,, sasa watamtoa na hiyo nchi inaweza kumeguka vipande vipande
Ethiopia na bwawa lake inaenda kuwa Historia Kama ilivyokuwa Historia ya DRC. Mnamo miaka ya 1970s nchi ya DRC ilianza mkakati wa ujenzi wa Mabwawa ya Umeme Maarufu Kama INGA DAMS Kwenye maporomoko ya Mto Congo (INGA FALLS). Edapo Mradi huo ungelikamilika kwa 100% Basi zingelizalishwa Jumla ya MEGAWATT 40,000. Hizi Zinatosha kutumika Barani Afrika Kote na shida ya Umeme ikaisha kabisa. Lakini ilianza misukosuko na Bwana likaishia njiani kuzalisha MEGAWATT 460 TU. Afrika bado tuna safari ndefu sana.
 
Makundi 9 yanayopiga vita serikali ya Ethiopia, yametangaza kuunda muungano hii leo ili kulazimisha mabadiliko ya kisiasa nchini humo.

Hatua hiyo inaongeza shinkizo dhidi ya Waziri mkuu Abiy Ahmed, wakati makundi ya wapiganaji yakiendelea kukaribia mji mkuu wa Addis Ababa.

Makundi kadhaa yamejihami kwa silaha japo haijabainika iwapo makundi yote yanayopinga serikali yana silaha.

Makundi ya wapiganaji wa Oromo na lile linalodai kupigania demokrasia la Agaw, yameambia shirika la habari la Reuters kwamba muungano huo unaojumulisha wapiganaji wa Tigray, ni halali.

Wapiganaji wa Tigray wamekuwa wakipigana na serikali kwa mwaka mmoja sasa katika vita ambavyo vimeua maelfu ya watu na kulazimisha zaidi ya milioni mbili kutotoka makwao.

Mataifa ya Afrika na ya magharibi yamekuwa yakitaka mapigano kusitishwa mara moja nchini Ethiopia, baada ya wapiganaji wa Tigray kusema kwamba wanaelekea kudhibithi mji mkuu wa Addis Ababa wiki hii.

Wapiganaji wametangaza kudhibithi mji wa Kemise, kilomita 325 kutoka Addis, lakini serikali imefutilia mbali madai hayo na kusema kwamba wapiganaji wanatoa habari za uongo kuhusu walipofikia.


VOA Swahili
Hakuna kitu ni porojo tu, wahuni wachache wa diaspora wameitisha press wakatangaza kuungana wakiwa Washington kisha wakapewa buku 7 kama za lumumba (joke). Kwa ukabila ulivyomkali Ethiopia hakuna namna vikundi hasimu vikashirikiana labda Oromo na somali kwa kupitia mgongo wa Dini.

Tigrayans, Amhara na Oromo ni paka na chui na wamekuwa wakichapana tokea utawala wa Mengistu. Leo hii waungane then nani awe kiongozi wa nchi?
 
Tusipende kila tunapofeli ktk mambo yetu kuanza kuwasingizia Wazungu.

Vita unaweza kuianzisha wewe mwenyewe ndani ya nchi yako na hao wazungu wakachangamkia tu fursa ya kuuza silaha zao zilizoko kwenye maghala. Vita Ni biashara pia ndani yake.

Jingine tawala nyingi za kiafrika Ni tawala zilizofeli, na hivyo zinachochea uasi au machafuko kutoka kwa raia. Maendeleo yamekuwa kisingizio Cha watawala wa kiafrika kuua kunyanyasa raia, uvunjivu was haki za kiraia nk. (Jiwe Ni case study kwa hili) Raia wanapoamka au wanapokataa matendo haya maovu tunaanza
kuwapakazia western countries.

Chukulia mfano hapa Tz , hili suala la kuandika katiba mpya linavyominywa na watawala. Siku Watz wakipata ujasiri na kusema liwalo na liwe Hali itakuwa mbaya sana . Na kwa mwanya huo wa nje watapata fursa ya kujineemesha kiuchumi kupitia hayo machafuko. Ila kwa ujinga watu hawataangalia tumefeli wapi badala yake watahangaika na matokeo ya kufeli kwetu badala ya chanzo cha tatizo.

Tanzania jinsi ilivyo hakuna Amani, Ni amani bandia inayohanikizwa na propaganda za watawala na vibaraka na chawa wao. Kilichobaki Tz ni utulivu tu. Amani ilishatoweka. Na utulivu una mwisho wake na tutashuhudia km hayo ya Ethiopia. Ni suala la muda kuamua. Woga,uzuzu,ujinga,elimu duni
inayozaa kutokujitambua kwa Watanzania ndiyo vitu watawala wanatafsiri km amani.

Ukiwasikiliza CCM na tambo zao utagundua kwamba bila mtutu wa bunduki hawawezi kuondoka. Kumbuka CCM kwa sasa si chama cha siasa bali ni genge la watu wachache wenye maslahi yanayofanana ktk kupora na kugawana rasilimali za nchi.Woga na uvumilivu kwa Wahabeshi umefika kikomo ndiyo unaona sasa wanapambana bila woga.
 
SPONSOR NI USA NA UK .

Ethiopia ilikuwa inakua kwa speed ya hatar , so ili kustop , suluhisho ni vurugu ka hizo.
inamaana hao us na uk ndio walimwambia walimwambia Abiy akataze jimbo la tigrey kufanya uchaguzi wao? muda mwingine tusisingizie wazungu kwa ujinga wetu wenyewe, huyo waziri mkuu wa ethiopia alitumia majeshi ya eritrea kupiga raia wa tigray na kujisifu kuwa amemaliza vita sasa acha na yeye yamkute, tokea mwanzo sikukubaliana huyo jamaa kupewa nobel peace prize ilikua mapema sana, sasa rangi yake ya ukweli imeonekana, alimuua yule mwanamuziki mwenye asili ya olomo kisa alikua hakubaliani na sera zake
 
Back
Top Bottom