Zacht
JF-Expert Member
- Jul 17, 2020
- 1,124
- 2,472
Hardtimes create tough men
Machafuko na vurugu za kisiasa, ukosefu wa elimu sahihi ya dini,elimu ya kiraia na mateso ya kijamii(uongozi) vilizalisha kizazi cha vijana wenye hasira waliokua kutokana na mazingira magumu vikapelekea makundi haya kuzaliwa si kwa misingi ya Qur’an.
Asili ya vikundi vingi hasa vya mashariki ya kati vilitokea kipindi cha vita baridi Mwaka 1979, pale Umoja wa Kisovieti (USSR) ulipovamia Afghanistan kueneza ukomonisti
Marekani, Saudi Arabia na Pakistan ziliamua kuunga mkono wapiganaji waliopinga uvamizi huo.
Marekani ilitumia nafasi hii kama silaha ya dhidi ya Urusi, kwa kufadhili wapiganaji hao na walitoa hamasa kwa Waislamu duniani kote kuisaidia Afghanistan akiwemo kijana kutoka Saudi Arabia Osama bin Laden,
Huo ndio mizizi wa kwanza wa makundi ya jihadi yalitokana na siasa za mataifa, si dini ilikuwa proxy war kati ya mataifa makubwa.
Baada ya Warusi kuondoka Afghanistan mwaka 1989
Wapiganaji wengi walirudi makwao wakiwa na uzoefu wa vita, silaha, na misimamo mikali.
Baadhi yao walihisi kuwa serikali za Kiislamu katika nchi zao (Misri, Algeria, Saudi Arabia n.k.) ni vibaraka wa Magharibi, hivyo wakaanzisha mapambano ya ndani ya kupindua serikali.
Osama bin Laden akaanzisha Al-Qaeda, ikidai inalinda Uislamu dhidi ya Wamagharibi na tawala za kifisadi za Kiislamu.
Lakini kimsingi, malengo yao yalikuwa ya kisiasa ni kumuondoa Marekani ambaye alianza kuweka mizizi yake Afghanistan baada ya kumuondoa soviet.
Makundi yaliyozaliwa miaka ya 2000 kwenye uvamizi wa Marekani Iraq
Baada ya kumuondoa Saddam Hussein, Marekani ilivunja jeshi la Iraq na chama cha Ba’ath.(Cha kisuni)
Watu wengi wa madhehebu ya Sunni waliondolewa kwenye serikali, hali iliyoleta mpasuko , chuki na machafuko.
Happ ndipo Abu Musab al-Zarqawi akaanzisha kikundi cha (Jama’at al-Tawhid wal-Jihad) kilianza kushambulia majeshi ya Marekani na raia wa Shia ambao walipewa inchi na Marekani
Baada ya kifo cha Zarqawi (2006), kikundi hiki kiliungana na Al-Qaeda na kuwa Al-Qaeda in Iraq (AQI).Baadae kilipanuka na miaka ya 2011–2013,
kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria, kiliibuka upya kikajiunga na wapiganaji wa Syria na kikajiita ISIS (Islamic State in Iraq and Syria).
Kutokana na machafuko haya ya muda mrefu raia wengi wengi wamepoteza matumaini ya kuishi ,nafasi ya kupata elimu ya dini na kiraia kumepelekea makundi haya kupata nguvu kwa watu waliopoteza matumaini.
Lakini kwenye mlengo wa kidini Makundi haya yapo mbali na muktadha wa Kiislamu kuhusu jihadi na muda mwingine wanatafsiri aya na hadith za Mtume nje ya muktadha wake kupata uungwaji mkono kwa Waislamu, kwa mfano kikundi kama HAMAS kipo kwasabbu za kisiasa Lakini wapo Waislamu kwa kutoelewa wanalikunga mkono kwa kuamini kinafanya jihadi kwa misingi ya Uislamu.
Kwanini tunasema vikundi hivi vipo kisiasa
Kwanza ileweke jihadi sio vita kwaajili ya kueneza Uislamu au kuua wasio Waislamu hicho ndio kitu cha kwanza na kikubwa kinachowatenganisha matendo yao na Uislamu, Jihad ni vita vya kujilinda na dhuluma ,kupigania haki (mkidhulumiwa) na sio kuvamia watu bila sababu (bila kushambuliwa)
Qur’an 2:190
“Piganeni katika njia ya Allah wale wanaokupigeni, lakini msivuke mipaka. Hakika Allah hawapendi wavukao mipaka.”
Hapa kuna masharti manne muhimu:
Vita iwe kujilinda, si kushambulia bila sababu.
Iwe kwa amri ya kiongozi halali wa Kiislamu, si kikundi binafsi.
Wanao pigwa ni wale wanaopiga Waislamu, si raia wasio na hatia.
Kuvuka mipaka (kuua wanawake, watoto, au kuharibu) ni haramu.
Pia Qur'an inaonyesha kuwa Waislamu hawaruhusiwi kuwadhuru wasiohusika kwenye vita.
Qur’an 60:8–9
“Allah hakukatazeni muwatendee wema na uadilifu wale wasiokupigeni kwa dini, wala hawakuwafukuza katika nyumba zenu...”
Hardtimes (vita, ukosefu wa elimu, udikteta) vimezalisha tough men waliokosa mwelekeo wa kiimani.
Ukosefu wa elimu sahihi ya dini
Vijana wengi katika maeneo haya hawana elimu ya fiqh, tafsiri, wala historia ya dini. Wanapewa tafsiri potofu ya Qur’an kama na viongozi wao mfano wanapewa aya inayosema
“Piganeni katika njia ya Allah…” (2:190)
Lakini wakaacha nusu yake:
“…msivuke mipaka. Hakika Allah hawapendi wavukao mipaka.”
Na siasa za kimataifa zilitumia maumivu yao kama silaha na matokeo yake ni makundi yanayobeba Qur’an mikononi, lakini mioyoni mwao kuna chuki na kisasi.