Kwa sera gani?Lissu ndio kipenzi cha Watanzania sasa hivi.
Watoto na familia nzima ya JK, hawawezi kumpa kura Mfalme JuhaEti wazee hawa ambao hawajalipwa pension?
Vijana wa wapi labda watoto wa Kikwete Mkapa na Mwinyi
Kundi lingine la kijamii litakaipa kura CCM ni la wasomi wametoa tamko lao kuwa kuna watu hawanadi sera wanatukana tu na kutishia amani tu
Kundi lingine la kijamii litakaloipa kura CCM ni walala hoi waliomba walimu bure kwa watoto wao,walioomba wajengewe miundo mbinu,walioomba miradi ya maji,umeme,vituo vya afya nk wakapewa
Lissu anaungwa mkono na wenye akaunti mia mia mitandaoni!Siasa ni Sayansi na uwekezaji kwa jamii.
Rais Magufuli na Chama Chake cha CCM wanaijua vyema Siasa na kwa uhakika waliweka mazingira tofautitofauti ya kuhakikisha makundi yote ya kijamii yanaiunga CCM.
Nitaanisha Makundi kadhaa ambayo CCM imeweza kuyapoka kutoka upinzani na Makundi iliyoendelea kuyashikilia.
1-Wazee(Kundi linaloipa heshima)
2-Wanawake(Bado ni kundi kindakindaki)
3-Vijana(Kundi hili limepokwa kutoka upinzani baada ya 2015.)
4-Wasanii(kundi hili limeongezewa wafuasi kulinganisha na 2015)
5-Wanampira(aliyekuwa mwenezi wa CCM amehamasisha sana kundi hili)
6-Wanafunzi vyuo vikuu (Kwa miaka mitano mgogoro wa kukosekana kwa boom haukuwepo,Tahliso wamuunfa mkono)
7-Wanafunzi wa Sekondari(High Schools),kundi hili limeguswa baada ya Shule kongwe zote nchini kupata fedha kiasi cha Tsh milioni 900+ kuboresha miundombinu
8-Wafanyakazi hasa walimu
madeni ya muda mrefu yamelipwa.Walimu wa sekondari wanapata responsibility allowance.
Madaktari wapya zaidi ya 1500 walipata fursa za ajira.
9-Wachimbaji wadogo wadogo
wamepata fursa ya kufanya biashara kimataifa.HONGERA LAIGWANANI LAIZER KWA KUPIGA MAWE YA KILO ZA KUTOSHA HUKO MERERANI.
10-Wamachinga,mama ntilie na bodaboda :Mgambo wa majiji na halmashauri hawawaletei bugudha tena.(Kundi hili limepokwa kutoka upinzani)
11-Wakulima na Wafugaji:
Yale mauaji na vurugu yaliyokuwa yakitokea mara kwa mara yamepungua hasa.Kangomba wamepigwa pin haswa.
12-Taasisi za dini:Hatimaye taasisi za dini zimetambua nia njema ya Mhe. Rais na sasa zi pamoja naye(Kundi hili limepokwa kutoka upinzani)
13-Walemavu:Wengi wamepata fursa zikiwemo za uongozi na mikopo bila riba.Mauaji ya Albino yameisha.
14-Viongozi wasomi wa vyuo vikuu:Unaposajili watu kama Kitila Mkumbo na Palamagamba Kabudi sekta ya Elimu ya juu inakuelewa unafanya nini.
15-Wapinzani wapenda maendeleo:Wengi walisema eti wamenunuliwa ila kiukweli wameona upinzani haujielewi.
16-Wafanyabiashara wa kati na wakubwa:hapa wafanyabiashara wakitanzania wamepewa fursa ya uwanja sawa wa kushindana na fursa za kuuza na kuagiza nje ya nchi.
17-Wakandarasi wenye mitaji midogo
sasa hivi zile curtail za kibiashara zimevunjwa
ORODHA ITAENDELEA
SAFARINI KALIUA!!!!!
CCM OYEE!
Hata hao wanaopiga propaganda wote ni CCM, saccos mwaka huu hamtausahau. Magufuli, tano tena.Scientific analysis!
Sasa hivi upinzani wamebaki na kakundi kadogo ka kupiga propaganda mitandaoni. Ukifungua JF thread za kuitukuza CHADEMA na kuibeza CCM zimeongozana, japokuwa zinaongea utumbo mtupu, lakini wao wamewekeza fedha zao kwenye kutuma thread nyingi za kupika, pamoja na picha za kupika.
Ila kiuhalisia ukienda kwenye makundi kama ambavyo umeelezea vizuri sana, kura zote ni Magufuli! Kweli siasa ni sayansi, watamkumbuka sana Dr Slaa!