Makundi ya wananchi Niger yaapa kupigania ulinzi wa nchi

Kuwa na bunduki au vifaa bora vya kijeshi hakuwezeshi kushinda vita. Hao ECOWAS na washirika wao wa USA na France wanaweza kuwatoa hao wanajeshi lakini wasiweze kabisa kuitawala Niger. Tujifunze Afghanistan na Vietnam ya Kusini. Marekani waliweka serikali walizozitaka lakini hazikudumu maana wananchi hawakutaka kutawaliwa na hao vibaraka
 
Unayosema ni kweli lakini eneo hili lina fyoko fyoko za muda mrefu za Boko Haram, ISIS na makundi mengine ya "kigaidi". Nigeria na juhudi zao zote wameshindwa kuwamaliza Boko Haram na mpaka leo wakiamua kukiwasha kule Nigeria ya Kaskazini wanakiwasha tu. Generali wa jeshi Buhari aliahidi kuwamaliza lakini mpaka amemaliza muda wake kawaacha.

Wasiwasi wangu ni kwamba, mapigano haya yanaweza kuvishwa koti la udini na eneo zima hili likawaka moto maana tayari linafukuta kwa harakati hizo. Na kama historia inavyotuonyesha hakuna cha ECOWAS wala nani atakayeweza kuwashinda wahafidhina wa kidini wakiamua maana wao hawaogopi kufa...na hakuna silaha hapa duniani inayoweza kumshinda mtu ambaye haogopi kufa. Hata Wamarekani wanalijua hili (rejea kilichowapata dhidi ya Mataliban!)

Busara itumike vinginevyo hii inaweza kugeuka "quagmire" nyingine ikawa mapigano ya muda mrefu ya kuviziana. Na waathirika wakubwa, kama kawaida, watakuwa ni wanawake na watoto.

Mungu Ibariki Afrika!
 
Ivi kwa nini wanaotumia profile picha ya uyo mzee wengi hawanaga akili 🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮
 
Jinga kabisa hili
 
Hayo ni maneno tu hata hao waliopindua ni wale wale tu hawana chochote watakacho ifanyia Niger sana sana ni ufisadi tu watafanya na kung'ang'ania madaraka, tuko hapa.

Kaburu P.W. Bother alishasema, "Hakuna kosa baya na lisilosameheka kama kumpatia mtu mweusi haki ya kutawala," leo hii sote tu mashahidi kwani kila mwafrika angekuwa na uwezo wa kulikimbia hili bara angekimbia lkn hatuna tu namna.
 
Unashabikia utapeli na uporaji wa mzungu mfaransa? Yawezekana pia unashabikia DP World kupora Tanganyika
 
Wananchi wa huko wanaonesha wanauzalendo sana.kwenye matatizo wameungana.cha ajabu sisi huku Tanzania nichi inauzwa lakini watu hatuungani kuwakabili wahalifu badala yake wanazidi kusifu upuuzi wa viongozi
 
Usiwapangie watu, wananchi wanachoka, uhuru wa kweli utaletwa na bunduki. Kama hao ufaransa na ECOWAS wanaweza basi waingie vitani, matamko ni mengi sana ni muda wa vitendo

Africa inaamka sasa, md wa ukombozi wa ukweli.
 
Maneno ya kanga hayo, watu wameamua na hauna kurudi nyuma, vibaraka wa west wote matumbo joto
 
Wewe utakuwa mwarabu ...idiot
 
Mrusi ndo Putin halafu huyo huyo Putin anatawala ki mabavu Urusi ukimpinga unalishwa sumu.
 
Hata kama ingekuwa Tz naamin nyomi ingejitokeza kwenda kuchukua mafunzo. Raia wamechoka na hizi tawala za sanaa, eti Democrasia wakati ni Wizi na ufisadi wa mali za umma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…