Makundi ya watu ambao wakifungua biashara lazima zife, fahamu kundi lako na Ubadilike

Makundi ya watu ambao wakifungua biashara lazima zife, fahamu kundi lako na Ubadilike

1.Kapata Pesa za Ghafla

Hapa kuna wale wenzangu wa michezo ya bahati na sibu au kuna mirathi,kuuza kitu flani nk nk,hawa watu mara nyingi biashara huiwaza angali ameshika pesa,alikua hana hata mpango wa biashara ila kwakua kapata pesa na watu waliomzunguka wengi marafki majiran n wafanyabiashara wanamshawishi,anafungua.. huyu mtu hatoboi.
Dah!? Umenifumbua macho💪💪💪💪💪🔥🔥🔥
 
Kwahiyo wenye Million 10 hatupaswi kufanya biashara Mkuu?
Mnaruhusiwa kufanya, Ukinipa mimi Mil. 10 kama nataka fungua duka la nguo

sitokodi frem,nitaificha 9m mahali,nitatoka na 1m nitaenda k.koo nitanunua nguo

nitakazotaka kuanzia,nitaanza kama machinga mahali nitafungua kakibanda changu (tuliii)

nitaanza kuuza huku nikisoma wateja wanataka nini,wanavaa nini,bei za nguo,nguo gan si nzuri,nk nk

halafu kakibanda changu nitaanza kukaongeza mdogo mdogo kulingana na mahitaji ya wateja wangu

kumbuka nina kale ka (9m) nimekaficha so nitakua nakadokoa kila nikiagzwa kitu na mteja,mkuu mpaka

ile 10m inakuja kuishia kwenye kibanda changu (kama bado nitakua hapo) nguo nitakazokua nazo,zote zinauzika sitokua na nguo yakumaliza mwezi haijanunuliwa.

ila leo hii wewe kafungue duka la 10m,nunua mzigo wa 10m nakuhakikishia utaingia chaka nguo nyingi sanaaaa na hutojua hilo kwasababu nguo ni mingi umenunua na hautojua kasoro zake ki ufupi una hatari ya kupoteza kuliko mimi.

Mkuu mimi nikitaka fungua biashara ya 20m naianza kimachinga,hutonielewa leo ila ukinitafuta baada ya mwaka kwenye biashara hyo hyo utaniita Mchawi,biashara si uchawi bro ni Calculations tu.
 
Nimepata kitu kwa kweli, ni kushukuru ndugu mleta mada. Kama ilivyo ada elimu haina mwisho kila leo ni kujifunza na elimu yoyote aipatayo mtu huwa haimuachi kama ilivyo mkuta.

Mimi japo sio mfanya biashara wala mjasiriamali lakini bandiko hili limenigusa katika engo yangu na nimepata mawili matatu ya kuni songesha mbele.
 
Mhh wee.kajamaa vinyuzi vyako ni vya maaanaa daah..unamawazo positive snaa..refer ile nyuz yako ya Tshs 50000
nafanya kwa ajli ya wana JF mkuu,naokoa watu wengi sana

PM ninazokutana nazo zinanifanya nisiache saidia watu maana

naletewa shuhuda nzito nzito jambo linalonifanya niseme YES i need more....
 
Nimepata kitu kwa kweli, ni kushukuru ndugu mleta mada. Kama ilivyo ada elimu haina mwisho kila leo ni kujifunza na elimu yoyote aipatayo mtu huwa haimuachi kama ilivyo mkuta.

Mimi japo sio mfanya biashara wala mjasiriamali lakini bandiko hili limenigusa katika engo yangu na nimepata mawili matatu ya kuni songesha mbele.
Ubarikiwe Pendaaa....
 
Mwamba kama mwamba....nipo katika harakat ya kuongeza goli lingne la biashara mpya though..sjawai ifanya ila nataka nijarib...duka la vyakula muhimu tuu na vinnywaji

Location nzur
Jijana wa golin anakuja week ijayo kutoma kijijin...etc etc

Ni expect nn from this biashara mkuu
 
Mr. Controller: aiseeeeh umebarikiwa sana kuwa cons mzuri sana hivi nikuombe jambo andika vitabu bas ili unachokifanya humu kije kisaidie na kizazi kinachokuja baada ya sisi wa leo kwani unamapin sana katika kumshauri binadamu muelewa na mwenye maono y a mbali
 
Back
Top Bottom