Kwahiyo wenye Million 10 hatupaswi kufanya biashara Mkuu?
Mnaruhusiwa kufanya, Ukinipa mimi Mil. 10 kama nataka fungua duka la nguo
sitokodi frem,nitaificha 9m mahali,nitatoka na 1m nitaenda k.koo nitanunua nguo
nitakazotaka kuanzia,nitaanza kama machinga mahali nitafungua kakibanda changu (tuliii)
nitaanza kuuza huku nikisoma wateja wanataka nini,wanavaa nini,bei za nguo,nguo gan si nzuri,nk nk
halafu kakibanda changu nitaanza kukaongeza mdogo mdogo kulingana na mahitaji ya wateja wangu
kumbuka nina kale ka (9m) nimekaficha so nitakua nakadokoa kila nikiagzwa kitu na mteja,mkuu mpaka
ile 10m inakuja kuishia kwenye kibanda changu (kama bado nitakua hapo) nguo nitakazokua nazo,zote zinauzika sitokua na nguo yakumaliza mwezi haijanunuliwa.
ila leo hii wewe kafungue duka la 10m,nunua mzigo wa 10m nakuhakikishia utaingia chaka nguo nyingi sanaaaa na hutojua hilo kwasababu nguo ni mingi umenunua na hautojua kasoro zake ki ufupi una hatari ya kupoteza kuliko mimi.
Mkuu mimi nikitaka fungua biashara ya 20m naianza kimachinga,hutonielewa leo ila ukinitafuta baada ya mwaka kwenye biashara hyo hyo utaniita Mchawi,biashara si uchawi bro ni Calculations tu.