Makundi ya watu ambao wakifungua biashara lazima zife, fahamu kundi lako na Ubadilike

Makundi ya watu ambao wakifungua biashara lazima zife, fahamu kundi lako na Ubadilike

Nakupenda kaka yangu CONTROLA yani una vitu kichwani hata kama huvifanyii kazi ila jua vinatusaidia sana. Unaweza ukawa siku hyo umekata tamaa kabisa ukija kusoma mada zako unasema kumbe niendelee kuvumilia tuu.
Your welcome love... Thanks 😍

Napenda tu ufahamu kaka ako sio Motivator, sio Mpasha watu vichwa wale tunawaita

motivational speaker,ukiona kitu nakiandika ujue nakifanya and mostly vyote ninavyoshauri

watu wafanye navifanya na kama sikifanyi,basi kipo njiani kinakuja "naibiaga watu siri za plan zangu"

japo hawajui,naandika kwa ajili ya wana JF naandika kwasababu najua naokoa wangapi,testimony ninazo PM

Sitochoka wala kuacha wala kusitisha kufanya ninachofanya,ukiniuliza my favourite game nitakujibu just easy "chasing money" its my favourite game..

Be inspired and take action,nawaambiaga watu walio around me hasa marafiki na watu walionizoea kuwa

Napenda kuwaona wakifanikiwa,napenda kuona nina marafiki wana pesa,napenda kuona nimezungukwa na watu wana mafanikio.

so sitoweza wapa pesa ila nimeshawambia nitawasaidia kwa lolote lililo ndani ya uwezo wangu,i had no one to push me forward before ila mimi nimejiapiza nitasaidia sana yeyote ataeniona naweza msaidia.

This is JF si miaka mingi Watu watanijua who is CONTROLA sibwabwaji tu,sitafuti fans,sitafuti anything nafanya kwa ajili yenu, ukiinuka ukasimama "huo ni ushindi kwangu"....
 
Kuna binti alianzisha uzi.

Alianza kwa kumuomba ushauri wa kibiashara mshkaji.

Baadaye wakawa na uhusiano wakaamua kuchanga pesa ili waanzishe biashara.

Mchizi akamuambia mdada ana shida akopeshwe pesa akakopeshwa 400K baada ya kudaiwa akavunja uhusiano na majibu shit ya kumwaga.

Mwisho akamtishia binti kwamba atamfanyia kitu kibaya yeye ana roho mbaya.

So this is just a confused con artist at work.
Walianzisha uhusiano wa kimapenzi au urafiki wa kawaida?
 
Your welcome love... Thanks 😍

Napenda tu ufahamu kaka ako sio Motivator, sio Mpasha watu vichwa wale tunawaita

motivational speaker,ukiona kitu nakiandika ujue nakifanya and mostly vyote ninavyoshauri

watu wafanye navifanya na kama sikifanyi,basi kipo njiani kinakuja "naibiaga watu siri za plan zangu"

japo hawajui,naandika kwa ajili ya wana JF naandika kwasababu najua naokoa wangapi,testimony ninazo PM

Sitochoka wala kuacha wala kusitisha kufanya ninachofanya,ukiniuliza my favourite game nitakujibu just easy "chasing money" its my favourite game..

Be inspired and take action,nawaambiaga watu walio around me hasa marafiki na watu walionizoea kuwa

Napenda kuwaona wakifanikiwa,napenda kuona nina marafiki wana pesa,napenda kuona nimezungukwa na watu wana mafanikio.

so sitoweza wapa pesa ila nimeshawambia nitawasaidia kwa lolote lililo ndani ya uwezo wangu,i had no one to push me forward before ila mimi nimejiapiza nitasaidia sana yeyote ataeniona naweza msaidia.

This is JF si miaka mingi Watu watanijua who is CONTROLA sibwabwaji tu,sitafuti fans,sitafuti anything nafanya kwa ajili yenu, ukiinuka ukasimama "huo ni ushindi kwangu"....
Appreciated
 
Kwangu hii ndo post Bora tokea nijiunge humu
Na mnavyomjaza sifa ndio maana anawapiga huko PM mnakuna kulia lia humu.
Huyu mwana alitapeli mdada humu, akamla bure na kisha akamkopa, finaly akamtengenezea matusi ya kumdhihaki kwamba ana kaswende akafie mbali, cha ajabu wana JF hawa hawa hawajawah kuona huyu jamaa ana appologize wala kusema kamlipa dada hela yake isipokuwa zile jeuri na dhalau alizoonesha kwenye msg alizokuwa anamtumia yule mdada ndo hizo hizo kazimaintain.

Na hii kujisifia kwamba ana madini sijui business ni eidha ana kopy toka kwa waandishi huko kwenye apps na magroup ana paste humu, maana yule dada aligusia kwamba huyu kijana hana kitu sana sana alifungua kibanda cha mpesa na kikamshinda.

Ninachotaka kusema

1. Hii ni njia anayotumia kuwalia hela watu humu na kuwala nyama zao pale inapobidi kama yule alieliwa hela na nyama.

2. Hawa ni wale wale motivational speakers, sio wafanyabiashara, basi kama anafanya ni theory nyingi

3. Wana JF tujifunze kuacha unafiki tunapoona mtu anaendekeza utapeli, ujeuri, ubedhui, n.k tunapasa kumshauri na kumfunza utu!

Ila kupiga piga makofi kwa tapeli inamaanisha mnaunga mkono tuhuma zake.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
1.Kapata Pesa za Ghafla

Hapa kuna wale wenzangu wa michezo ya bahati na sibu au kuna mirathi,kuuza kitu flani nk nk,hawa watu mara nyingi biashara huiwaza angali ameshika pesa,alikua hana hata mpango wa biashara ila kwakua kapata pesa na watu waliomzunguka wengi marafki majiran n wafanyabiashara wanamshawishi,anafungua.. huyu mtu hatoboi.

2.Nimechoka kuajiriwa nataka kufungua biashara yangu

Huyu nae ni wale wale yaniiii watu wa namna hii mimi nawaitaga ni wavivu,ukimuuliza kwann anasema amechoka kuajiriwa utamskia anakwambia kazi nyingi sanaa,naamka asubuhi sana narudi usiku,yani sina uhuru kila mahali kwenda hadi ruhusa, hana sababu ambayo ukiiskia unasema yes kweli huyu anahitaji kujiajiri, Hana Mawazo Hana kitu ni mweupe pee anachojua yeye ni afungue biashara yake.. Kamaliza. Asijue kuwa hamna adhabu kali kama kujiajiri.

3.Nina 2m hivi unanishauri nifungue biashara gani

Kuna watu nawasikitikiaga ila sina la kufanya nawajibu tu vile wanavyoniuliza,ila ki ukweli najua moyoni mwangu huyu na hii hela yake inaenda kupotea yoteee,ila ki ukweli watu wenye mitaji na hawajui waifanyie nini wapo kwenye risk sana.

4.Kuna biashara naskia ina hela sana,ngoja niifanye

Hawa ni wale watu ambao yeye anafanya hiyo biashara kwsabbu kasikia ina pesa,anaifungua hiyoo biashara kwasababu anamuona mtu inamlipa kama n mama ntilie na yeye anataka aige,hajui mwenzake faida anaipataje anachojua yeye ile biashaara ina pesa "naitaka namimi kuifanya".

5.Natafuta mtaji Mwakani hivi ntaanza Biashara yangu

Ukiona tu una mawazo ya hivi,jua huko mwakani kukifika utapata excuse ingine.. biashara hainaga cha kesho Ukiamua kuianza unaanza hapo hapo ulipo yani sasa hivi bila kujali una pesa au hauna hiyo ndio biashara na ujasiriamali,tunaaanzia na kile kilichopo hatusubiri kesho wala badae wala mwakani kwasababu mwakani kuna ratba zake zingine.

Hao ni watu watano ambao ktk wale ambao biashara zao nyingi zinakufa wengi hutokea kwenye 1 ya haya makundi matano,sasa unaweza ukajiuliza ni mtu gani akifungua biashara atafanikiwa,mbona kama makundi yote matano yamegusa kila mtu?

Hapana,kuna kundi 1 ambalo tunasema ni wale wenye "utayari" uthubutu na waliodhamiria kweli kufanya wanachokitaka bila kujali wana mtaji kiasi gani pale walipo.

Mfano kuna mtu ana lengo la kuja kufungua LIQUOR STORE ila amejiangalia akiba yake anajkuta ana sh.laki 1 au ana elfu hamsni tu,Mfanyabiashara wa kweli hutomsikia akikwambia ngoja nitafute mtaji halafu nitafungua mwakani au mwezi ujao...

mfanyabiashara OG huanza na alichonacho ana sh laki 1 mfukoni target yake si kuja kumiliki liquor store ya maana,anaweka target mbele ila kwasasa na hii laki yake ataenda nunua konyagi,valuer,double kick,na vinywaj vingine vya kupima pima ambavyo vitatoshea pesa yake...

Ataenda sehemu yenye mchanganyiko au atatafuta location yake atatega pale na mwamvuli wake atauza vyombo vyake, ataongezea na vocha,sigara nk..kumbuka anapoanza ataonekana kama jinga flani (watu hawajui target ya mwenzao ni ipi) ataanza kazi mdogo mdogo.

day 1 atauza kikonyagi kidogo,mara day 2 atamaliza konyagi kubwa ataenda akipanda mdogo mdogo hadi atakua akiuza Konyagi chupa zima,mtaji unakua alianza na mizinga miwili,ataenda akiongeza hadi atapoona inatosha,anahamia kinywaji kingine,hvyo hvyo.

Huyu mtu kufika mwakani atakua na kasehemu ambacho mtu kama hazard cfc akikatza tu pale lazima atafute kiti akae apashe koo,kwasababu huyu mtu ana malengo na anajua anapoelekea ukimtafuta baada ya miaka mi 5 Utamkuta na LIQUOR STORE yenye Wateja wa kutosha, ana channel za kutosha, anajua bei hadi za vizibo vya double kick humdanganyi kitu,anajua bei hadi za sticker za konyagi yani hamna asichojua kuhusu vinywaji vyake.

Huyu mtu biashara yake kufa ni Mumloge AFE ila sio mumloge mumuache hai,Mlogeni AFE ndio mtakua mmemuweza ila ukimloga akaumwa biashara ika drop Akipona akirudi uwanjani Hachukui round nyingi kufika alipokua, Kwanini unajua? Kwasababu hakutaka shortcut.

Mtaji wa biashara na ujasiriamali ni MUDA na wengi hili limewashindwa ndio mana anataka aanze biashara na mtaji wa mil.10 aanze biashara na mtaji wakupika kilo 6,aanze biashara na kununua bodaboda yake mwenyewe,aaanzie juuu Hamna anaetaka anzia huku sakafuni, na kama unajijua unafanya biashara hujui unachouza kinapatikana wapi Dear huna round wewe.

kuna mtu anauza majiko ya mkaa ila hajui majiko ya mkaa yanatengenezewa wapi,anachojua yeye majiko ya mkaa yakikarbia kuisha anapga simu analetewa,hadi alipo.

kuna mtu anauza mkaaa ila muulize mkaa una uza unautoa wapi,atakujibu easy tu "naletewaga na kaka mmoja yupo ruvu anamkaa mzuri bei nzuri kweli" muulize kawahi fika huko ruvu? ana uhakika na bei anayouziwa n nzuri kama anavyoipamba? watu ni wavivu watu wanapenda shortcut ndio mana wanafungua biashara mwaka tu zinakufa.

ila wapo ambao wataonekana wachawi,wameaga,wana bahati,nk kwasababu biashara zao hazifi,,biashara haina uchawi biashara inahtaji kufata utaratbu hatua kwa hatua usiruke hatua hata 1,ukijifanya unataka kukimbia tu ukaruka hatua tano mbele "siku 1 itaku cost" biashara hailazimishwi inajiendesha yenyewe taratbu mdogo mdogo.

Kuna watu wanataka nenepesha ng'ombe siku za minada,hatonenepa ila atavimbiwa,makundi ma 5 pale juu ni aina ya watu wapenda shortcut,akili yao inawaza pesa kuliko Biashara yenyewe.

Biashara si pesa tu,unapofanya biashara unahitaji faida mbili 1.wateja 2.pesa Faida namba 1 n wateja, sasa wewe unataka kuanza na mtaji wa mil.10 ili ukunje faida LAKI kwa siku, Hao wateja wakukupa laki per day unao? au unataka ukapge ramli?

Acheni shortcut,kubali kwamba biashara si pesa tu kuna siku watu wanarudi majumbani mwao hawana hata senti 5 faida yote kala mchana usiku na matumizi mengine,hajaweka akiba hata sent ila Ana amani ana furaha,kwanini unajua? hajapata pesa ya kuweka kwenye Kibubu ila kapata Faida ya Wateja,amepata wateja ambao siku 1 watakuja kumpa pesa mara mbili au tatu ya ambazo angezipata leo.

Badilika kama ulikua upo ktk kundi mojawapo pale juu, Biashara ina hela kweli (hata sio uongo) lakini ili uone pesa kimaukweliiiiii yakupasa ukubali kutoa sadaka muda wako na kila ulichonacho,nikisema muda siongelei masaa ua siku kadhaa naongelea ishu za miaka kadhaaa, Hakuna kirahisi wakuu anaewambia ni rahisi anawapotosha.

Asante kwa kusoma,naamini umepata kitu.
Umesema kweli Ila kumbuka pia dunia haiko kulingana na mtizamo wako mkuu
Once upon time said that "" we don't see things as they really are but how we're""
Nina milioni 600 nimefisadi samowea naagiza Kosta zangu 10 napata usimamizi mzuri na motisha plus morale kwa madereva.
Kuwa dereva atakayekuwa anatunza gari yake isiharibike mwisho wa mwaka nampiga kiwanja hapa kazi haiendi kweli.
Najenga nyumba za kupangisha so hapa sitoboi.

Huwa inategemeana na Aina ya biashara.binafsi napenda Sana biashara ya daladala Mana Haina kubembeleza mteja.
 
Jamaa namkubali sana kwa kanuni anayoitumia...anajibu vipi shutuma zinazotolewa na watu watatu tuu kati ya wanna jf zaidi ya 6000 waliosoma hii thread na mtu ambae haweki ushahidi ili watu wengine wathibitishe.......ni uhakika ukiwa na tabia ya kujibu kila ambacho binadamu anakutuhumu nacho Basi na utambue maisha yako yoote yatakuwa kwenye kujibu nakuomba misamaha

Tupo nae na kumpongeza kwa bandiko hili kwa sababu linatufundisha na kutuongezea nyama katika harakati tulizozichagua na hatuwezi kuwa upande wa kumshutumu kwa kitu ambacho hatujahakikishiwa na alietendewa wala na alieileta kwetu hiyo shutuma
Ndo maana mimi niliamua kuchagua madini yake na sio personal issues zake

Na ikiwezekana aendelee kutufundisha kila siku asichoke

CONTROLA Mungu akupe moyo kuyashinda haya hizi attacks zisizo na maana
 
Kama ni tuhuma why mnaendelea kumattack wakati hakuna uthibitisho?
Ukiichunguza sana utagundua ni wivu walionao kwa mwana kuwa kwanini anawafuasi na watu wengi wanasifia mabandiko yake kuliko wao .,..kwa maelezo yao wanafikia mpaka kuwakosea heshima waanzilishi na wafanyakazi wa jf kwa kusema kuwa wanamlinda mwana kwa kufuta huo uzi na kumpiga ban huyo dada kwa manufaa ya kumlinda tapeli controller
 
Kuna binti alianzisha uzi.

Alianza kwa kumuomba ushauri wa kibiashara mshkaji.

Baadaye wakawa na uhusiano wakaamua kuchanga pesa ili waanzishe biashara.

Mchizi akamuambia mdada ana shida akopeshwe pesa akakopeshwa 400K baada ya kudaiwa akavunja uhusiano na majibu shit ya kumwaga.

Mwisho akamtishia binti kwamba atamfanyia kitu kibaya yeye ana roho mbaya.

So this is just a confused con artist at work.
Hebu upandishe huo uzi usijekua unamchafua jamaa

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
 
Bro najifunza mengi sana kupitia posts zako
Siku nami nikifanikiwa nitakuja kupost
 
Motivation speaker
Aisee hawa jamaa ukiwasiliza unaweza kujiona dunian mjinga n wee tuuu
 
Back
Top Bottom