Makundi ya watu ambao wakifungua biashara lazima zife, fahamu kundi lako na Ubadilike

Kuna tofauti gani kwenye hili andiko na wale motivesheni spikas walioanzisha restaurant kwa mchele mmoja??
Tofauti yake ipo akilini mwako, ukiliweka hili andiko kichwani na kulitafakari vizuri, basi kama una akili timamu lazima ujifunze kitu!

Ila kama ubongo wako hauna uwezo wa kuelewa basi hautaona tofauti kati ya uzi huu na ule wa kula tunda kimasihara.
 
[emoji3][emoji3] unanunua ukwaju halaf unaubandika jikoni na maji mengi ya kutosha unauacha uchemke hadi ulegee yaan zile mbegu zake zionekane unaipua halaf unakoroga koroga kuhakikisha ukwaju unalainika zaid baada ya hapo unachuja utenganishe mbegu na juice na unautia maji ili kuondoa uchachu kwa kiwango ambacho utaona hapa unanyweka halaf unaweka sukari unaweka kwenye chupa tayar kwa kuuza usisahau kuhakikisha unauweka kwenye frij kidogo upoe
Oho basi sawa mkuu ..shukurani
 
Asante... nilikua mtaani kwa muda sana napiga mishe zangu naingiza hela natumia kifala tu... nw nimerudisha mpira kwa kipa(nimeajiriwa) ila yanashinda maisha haya...

Nawekeza huku kwenye kuajiriwa for one year nipate discpline kwanza ndo nirudi mtaani... kitaa bila discpline bila bila hutoboi yani
Ni vyema umeonja pande zote umejua uchungu na utamu wake, ki ukweli ajira huwa inatulinda sana panaotokea economic crisis kidunia ingawa sio sana ila sio mbaya kulinganisha na waliojiajiri, hela ya kujikimi ipo inakuwepo sio mbaya, ila ukijiajiri kuna wakati utatumia hela kwaajili ya gharama ya uendeshaji biashara muda wote huo wote na sio kutemgeneza faida
 
Kuna binti alianzisha uzi.

Alianza kwa kumuomba ushauri wa kibiashara mshkaji.

Baadaye wakawa na uhusiano wakaamua kuchanga pesa ili waanzishe biashara.

Mchizi akamuambia mdada ana shida akopeshwe pesa akakopeshwa 400K baada ya kudaiwa akavunja uhusiano na majibu shit ya kumwaga.

Mwisho akamtishia binti kwamba atamfanyia kitu kibaya yeye ana roho mbaya.

So this is just a confused con artist at work.
Duh ngoja aje atatolea ufafanuzi kwa hili
 
Sidhani kama atakuja, hizi allegations zipo toka mwanzoni mwa hii thread

Nigga anazipita tu....

Ugumu wa maisha na kukosa uelewa wa mambo unafanya watu wawe conned kirahisi mitandaoni humu

Amekaa kimya hadi sasa, most probably kijana ni con artist mwenye kiburi pro max
 
Ebhana mkuu huo Uzi sijawahi kuuona mkuu em Fanya kama unanitag chap ..

Mkuu CONTROLA hizi shutuma ni za kweli ..Yani unaanzisha mahusaiano na mamsi halafu unampiga asee!!? Kwa hiyo mbususu akupe na bado umtapeli sasa tunakuaminije boss na umekuwa ukitupa elimu jf na kukuona wewe kama kioo cha jamii kwa madini unayotupa.

Au nyie ndio wale majamaa wa global alliance nini ..wale wazee wa good morning millionaire hata kama ni usiku..

Sema hii itakuwa ni kashfa mbaya sana bro. Na Mimi sitokuamini tena hata kwenye hizi nyuzi zako.
Mdada alipost screenshots za vitisho kutoka kwa mshkaji.

Maajabu yake mdada akala ban.
 
1.Kapata Pesa za Ghafla

Hapa kuna wale wenzangu wa michezo ya bahati na sibu au kuna mirathi,kuuza kitu flani nk nk,hawa watu mara nyingi biashara huiwaza angali ameshika pesa,alikua hana hata mpango wa biashara ila kwakua kapata pesa na watu waliomzunguka wengi marafki majiran n wafanyabiashara wanamshawishi,anafungua.. huyu mtu hatoboi.

2.Nimechoka kuajiriwa nataka kufungua biashara yangu

Huyu nae ni wale wale yaniiii watu wa namna hii mimi nawaitaga ni wavivu,ukimuuliza kwann anasema amechoka kuajiriwa utamskia anakwambia kazi nyingi sanaa,naamka asubuhi sana narudi usiku,yani sina uhuru kila mahali kwenda hadi ruhusa, hana sababu ambayo ukiiskia unasema yes kweli huyu anahitaji kujiajiri, Hana Mawazo Hana kitu ni mweupe pee anachojua yeye ni afungue biashara yake.. Kamaliza. Asijue kuwa hamna adhabu kali kama kujiajiri.

3.Nina 2m hivi unanishauri nifungue biashara gani

Kuna watu nawasikitikiaga ila sina la kufanya nawajibu tu vile wanavyoniuliza,ila ki ukweli najua moyoni mwangu huyu na hii hela yake inaenda kupotea yoteee,ila ki ukweli watu wenye mitaji na hawajui waifanyie nini wapo kwenye risk sana.

4.Kuna biashara naskia ina hela sana,ngoja niifanye

Hawa ni wale watu ambao yeye anafanya hiyo biashara kwsabbu kasikia ina pesa,anaifungua hiyoo biashara kwasababu anamuona mtu inamlipa kama n mama ntilie na yeye anataka aige,hajui mwenzake faida anaipataje anachojua yeye ile biashaara ina pesa "naitaka namimi kuifanya".

5.Natafuta mtaji Mwakani hivi ntaanza Biashara yangu

Ukiona tu una mawazo ya hivi,jua huko mwakani kukifika utapata excuse ingine.. biashara hainaga cha kesho Ukiamua kuianza unaanza hapo hapo ulipo yani sasa hivi bila kujali una pesa au hauna hiyo ndio biashara na ujasiriamali,tunaaanzia na kile kilichopo hatusubiri kesho wala badae wala mwakani kwasababu mwakani kuna ratba zake zingine.

Hao ni watu watano ambao ktk wale ambao biashara zao nyingi zinakufa wengi hutokea kwenye 1 ya haya makundi matano,sasa unaweza ukajiuliza ni mtu gani akifungua biashara atafanikiwa,mbona kama makundi yote matano yamegusa kila mtu?

Hapana,kuna kundi 1 ambalo tunasema ni wale wenye "utayari" uthubutu na waliodhamiria kweli kufanya wanachokitaka bila kujali wana mtaji kiasi gani pale walipo.

Mfano kuna mtu ana lengo la kuja kufungua LIQUOR STORE ila amejiangalia akiba yake anajkuta ana sh.laki 1 au ana elfu hamsni tu,Mfanyabiashara wa kweli hutomsikia akikwambia ngoja nitafute mtaji halafu nitafungua mwakani au mwezi ujao...

mfanyabiashara OG huanza na alichonacho ana sh laki 1 mfukoni target yake si kuja kumiliki liquor store ya maana,anaweka target mbele ila kwasasa na hii laki yake ataenda nunua konyagi,valuer,double kick,na vinywaj vingine vya kupima pima ambavyo vitatoshea pesa yake...

Ataenda sehemu yenye mchanganyiko au atatafuta location yake atatega pale na mwamvuli wake atauza vyombo vyake, ataongezea na vocha,sigara nk..kumbuka anapoanza ataonekana kama jinga flani (watu hawajui target ya mwenzao ni ipi) ataanza kazi mdogo mdogo.

day 1 atauza kikonyagi kidogo,mara day 2 atamaliza konyagi kubwa ataenda akipanda mdogo mdogo hadi atakua akiuza Konyagi chupa zima,mtaji unakua alianza na mizinga miwili,ataenda akiongeza hadi atapoona inatosha,anahamia kinywaji kingine,hvyo hvyo.

Huyu mtu kufika mwakani atakua na kasehemu ambacho mtu kama hazard cfc akikatza tu pale lazima atafute kiti akae apashe koo,kwasababu huyu mtu ana malengo na anajua anapoelekea ukimtafuta baada ya miaka mi 5 Utamkuta na LIQUOR STORE yenye Wateja wa kutosha, ana channel za kutosha, anajua bei hadi za vizibo vya double kick humdanganyi kitu,anajua bei hadi za sticker za konyagi yani hamna asichojua kuhusu vinywaji vyake.

Huyu mtu biashara yake kufa ni Mumloge AFE ila sio mumloge mumuache hai,Mlogeni AFE ndio mtakua mmemuweza ila ukimloga akaumwa biashara ika drop Akipona akirudi uwanjani Hachukui round nyingi kufika alipokua, Kwanini unajua? Kwasababu hakutaka shortcut.

Mtaji wa biashara na ujasiriamali ni MUDA na wengi hili limewashindwa ndio mana anataka aanze biashara na mtaji wa mil.10 aanze biashara na mtaji wakupika kilo 6,aanze biashara na kununua bodaboda yake mwenyewe,aaanzie juuu Hamna anaetaka anzia huku sakafuni, na kama unajijua unafanya biashara hujui unachouza kinapatikana wapi Dear huna round wewe.

kuna mtu anauza majiko ya mkaa ila hajui majiko ya mkaa yanatengenezewa wapi,anachojua yeye majiko ya mkaa yakikarbia kuisha anapga simu analetewa,hadi alipo.

kuna mtu anauza mkaaa ila muulize mkaa una uza unautoa wapi,atakujibu easy tu "naletewaga na kaka mmoja yupo ruvu anamkaa mzuri bei nzuri kweli" muulize kawahi fika huko ruvu? ana uhakika na bei anayouziwa n nzuri kama anavyoipamba? watu ni wavivu watu wanapenda shortcut ndio mana wanafungua biashara mwaka tu zinakufa.

ila wapo ambao wataonekana wachawi,wameaga,wana bahati,nk kwasababu biashara zao hazifi,,biashara haina uchawi biashara inahtaji kufata utaratbu hatua kwa hatua usiruke hatua hata 1,ukijifanya unataka kukimbia tu ukaruka hatua tano mbele "siku 1 itaku cost" biashara hailazimishwi inajiendesha yenyewe taratbu mdogo mdogo.

Kuna watu wanataka nenepesha ng'ombe siku za minada,hatonenepa ila atavimbiwa,makundi ma 5 pale juu ni aina ya watu wapenda shortcut,akili yao inawaza pesa kuliko Biashara yenyewe.

Biashara si pesa tu,unapofanya biashara unahitaji faida mbili 1.wateja 2.pesa Faida namba 1 n wateja, sasa wewe unataka kuanza na mtaji wa mil.10 ili ukunje faida LAKI kwa siku, Hao wateja wakukupa laki per day unao? au unataka ukapge ramli?

Acheni shortcut,kubali kwamba biashara si pesa tu kuna siku watu wanarudi majumbani mwao hawana hata senti 5 faida yote kala mchana usiku na matumizi mengine,hajaweka akiba hata sent ila Ana amani ana furaha,kwanini unajua? hajapata pesa ya kuweka kwenye Kibubu ila kapata Faida ya Wateja,amepata wateja ambao siku 1 watakuja kumpa pesa mara mbili au tatu ya ambazo angezipata leo.

Badilika kama ulikua upo ktk kundi mojawapo pale juu, Biashara ina hela kweli (hata sio uongo) lakini ili uone pesa kimaukweliiiiii yakupasa ukubali kutoa sadaka muda wako na kila ulichonacho,nikisema muda siongelei masaa ua siku kadhaa naongelea ishu za miaka kadhaaa, Hakuna kirahisi wakuu anaewambia ni rahisi anawapotosha.

Asante kwa kusoma,naamini umepata kitu.
MImi nipo kwenye moja ya hayo makundi hapo basi sifungui tena biashara...
 
Umesahau wale wanaofungua banda la M-PESA akiona mwenye bar kafungua?

Unawaachaje wale wanaoona jirani yake anauza genge na yeye anafungua lake pembeni Mita tano na alipo.

Hiyo safi sana inatengeneza umaarufu wa sehemu hiyo mwisho wa siku pataitwa magengeni wateja wataongezeka ndio maana ukienda mjini utakuta sehemu moja karibuni nusu mtaa au mtaa wote ni maduka ya nguo au vyombo au mapambo yamepangana.
 
Mnaruhusiwa kufanya, Ukinipa mimi Mil. 10 kama nataka fungua duka la nguo

sitokodi frem,nitaificha 9m mahali,nitatoka na 1m nitaenda k.koo nitanunua nguo

nitakazotaka kuanzia,nitaanza kama machinga mahali nitafungua kakibanda changu (tuliii)

nitaanza kuuza huku nikisoma wateja wanataka nini,wanavaa nini,bei za nguo,nguo gan si nzuri,nk nk

halafu kakibanda changu nitaanza kukaongeza mdogo mdogo kulingana na mahitaji ya wateja wangu

kumbuka nina kale ka (9m) nimekaficha so nitakua nakadokoa kila nikiagzwa kitu na mteja,mkuu mpaka

ile 10m inakuja kuishia kwenye kibanda changu (kama bado nitakua hapo) nguo nitakazokua nazo,zote zinauzika sitokua na nguo yakumaliza mwezi haijanunuliwa.

ila leo hii wewe kafungue duka la 10m,nunua mzigo wa 10m nakuhakikishia utaingia chaka nguo nyingi sanaaaa na hutojua hilo kwasababu nguo ni mingi umenunua na hautojua kasoro zake ki ufupi una hatari ya kupoteza kuliko mimi.

Mkuu mimi nikitaka fungua biashara ya 20m naianza kimachinga,hutonielewa leo ila ukinitafuta baada ya mwaka kwenye biashara hyo hyo utaniita Mchawi,biashara si uchawi bro ni Calculations tu.
This mindset is superb[emoji123] Huyu jamaa anaongea point tupuuu acha kabisa. Nakuelewa sana controla
 
For real hamjawahi uona huo uzi?

Baada ya pale mchizi akapotea kisha akaja na uzi wa kudai amefiwa. Personally nikajua ni trick ya kutaka huruma.
Hahahaha kwa hiyo msiba kuna wezekano ni "man made mkuu."

Una maanisha Kwa hiyo mwamba akaamua kumuua baba'ke ili APATE huruma za wafuasi wa jf.!!
 
Sidhani kama atakuja, hizi allegations zipo toka mwanzoni mwa hii thread

Nigga anazipita tu....

Ugumu wa maisha na kukosa uelewa wa mambo unafanya watu wawe conned kirahisi mitandaoni humu

Amekaa kimya hadi sasa, most probably kijana ni con artist mwenye kiburi pro max
Tungepata na upande wa pili WA yule Dada ungekuwa vizuri sema ndo hivyo nasikia kala Ban ..na mchizi hajajibu chochote hadi sasa na kuna maboya lazima watapigwa tu.
 
Duh mdada wa watu akala ban.

Sasa mkuu tufanyeje? Tuilaumu serikali tu..

Vip ile connection ya mama j wa yanga ulipataga??
Sikuitafuta.

Tz utapeli mitandaoni ni rahisi kwakua mitandao imeingia huku bado watu hawana uelewa na exposure.

Mfano ukiingia insta au kupatana unakuta mtu kapost anauza PS4 Pro 350K. PS5 450K.

Na anapata watu mostly coz watu wengi wana kanuni ya 'Seeing is believing' so ataona nyuzi za mchizi atapenda anachoona then the rest ni maumivu.
 
Hahahaha kwa hiyo msiba kuna wezekano ni "man made mkuu."

Una maanisha Kwa hiyo mwamba akaamua kumuua baba'ke ili APATE huruma za wafuasi wa jf.!!
Well akili yake ndivyo ilivyomtuma. Na amefanikiwa kwakua ona jinsi watu wachache wanaoukumbuka huo uzi.

Katika psychology huyu anaitwa 'sociopath' yuko radhi kudanganya hata uongo wa kimiyeyusho ili mradi lengo litimie.
 
Sikuitafuta.

Tz utapeli mitandaoni ni rahisi kwakua mitandao imeingia huku bado watu hawana uelewa na exposure.

Mfano ukiingia insta au kupatana unakuta mtu kapost anauza PS4 Pro 350K. PS5 450K.

Na anapata watu mostly coz watu wengi wana kanuni ya 'Seeing is believing' so ataona nyuzi za mchizi atapenda anachoona then the rest ni maumivu.
Mtandaoni huku ukiwa mzuri kimaandishi na unaweza kuwashawishi basi ni rahisi sana kuwapiga.
 
1.Kapata Pesa za Ghafla

Hapa kuna wale wenzangu wa michezo ya bahati na sibu au kuna mirathi,kuuza kitu flani nk nk,hawa watu mara nyingi biashara huiwaza angali ameshika pesa,alikua hana hata mpango wa biashara ila kwakua kapata pesa na watu waliomzunguka wengi marafki majiran n wafanyabiashara wanamshawishi,anafungua.. huyu mtu hatoboi.

2.Nimechoka kuajiriwa nataka kufungua biashara yangu

Huyu nae ni wale wale yaniiii watu wa namna hii mimi nawaitaga ni wavivu,ukimuuliza kwann anasema amechoka kuajiriwa utamskia anakwambia kazi nyingi sanaa,naamka asubuhi sana narudi usiku,yani sina uhuru kila mahali kwenda hadi ruhusa, hana sababu ambayo ukiiskia unasema yes kweli huyu anahitaji kujiajiri, Hana Mawazo Hana kitu ni mweupe pee anachojua yeye ni afungue biashara yake.. Kamaliza. Asijue kuwa hamna adhabu kali kama kujiajiri.

3.Nina 2m hivi unanishauri nifungue biashara gani

Kuna watu nawasikitikiaga ila sina la kufanya nawajibu tu vile wanavyoniuliza,ila ki ukweli najua moyoni mwangu huyu na hii hela yake inaenda kupotea yoteee,ila ki ukweli watu wenye mitaji na hawajui waifanyie nini wapo kwenye risk sana.

4.Kuna biashara naskia ina hela sana,ngoja niifanye

Hawa ni wale watu ambao yeye anafanya hiyo biashara kwsabbu kasikia ina pesa,anaifungua hiyoo biashara kwasababu anamuona mtu inamlipa kama n mama ntilie na yeye anataka aige,hajui mwenzake faida anaipataje anachojua yeye ile biashaara ina pesa "naitaka namimi kuifanya".

5.Natafuta mtaji Mwakani hivi ntaanza Biashara yangu

Ukiona tu una mawazo ya hivi,jua huko mwakani kukifika utapata excuse ingine.. biashara hainaga cha kesho Ukiamua kuianza unaanza hapo hapo ulipo yani sasa hivi bila kujali una pesa au hauna hiyo ndio biashara na ujasiriamali,tunaaanzia na kile kilichopo hatusubiri kesho wala badae wala mwakani kwasababu mwakani kuna ratba zake zingine.

Hao ni watu watano ambao ktk wale ambao biashara zao nyingi zinakufa wengi hutokea kwenye 1 ya haya makundi matano,sasa unaweza ukajiuliza ni mtu gani akifungua biashara atafanikiwa,mbona kama makundi yote matano yamegusa kila mtu?

Hapana,kuna kundi 1 ambalo tunasema ni wale wenye "utayari" uthubutu na waliodhamiria kweli kufanya wanachokitaka bila kujali wana mtaji kiasi gani pale walipo.

Mfano kuna mtu ana lengo la kuja kufungua LIQUOR STORE ila amejiangalia akiba yake anajkuta ana sh.laki 1 au ana elfu hamsni tu,Mfanyabiashara wa kweli hutomsikia akikwambia ngoja nitafute mtaji halafu nitafungua mwakani au mwezi ujao...

mfanyabiashara OG huanza na alichonacho ana sh laki 1 mfukoni target yake si kuja kumiliki liquor store ya maana,anaweka target mbele ila kwasasa na hii laki yake ataenda nunua konyagi,valuer,double kick,na vinywaj vingine vya kupima pima ambavyo vitatoshea pesa yake...

Ataenda sehemu yenye mchanganyiko au atatafuta location yake atatega pale na mwamvuli wake atauza vyombo vyake, ataongezea na vocha,sigara nk..kumbuka anapoanza ataonekana kama jinga flani (watu hawajui target ya mwenzao ni ipi) ataanza kazi mdogo mdogo.

day 1 atauza kikonyagi kidogo,mara day 2 atamaliza konyagi kubwa ataenda akipanda mdogo mdogo hadi atakua akiuza Konyagi chupa zima,mtaji unakua alianza na mizinga miwili,ataenda akiongeza hadi atapoona inatosha,anahamia kinywaji kingine,hvyo hvyo.

Huyu mtu kufika mwakani atakua na kasehemu ambacho mtu kama hazard cfc akikatza tu pale lazima atafute kiti akae apashe koo,kwasababu huyu mtu ana malengo na anajua anapoelekea ukimtafuta baada ya miaka mi 5 Utamkuta na LIQUOR STORE yenye Wateja wa kutosha, ana channel za kutosha, anajua bei hadi za vizibo vya double kick humdanganyi kitu,anajua bei hadi za sticker za konyagi yani hamna asichojua kuhusu vinywaji vyake.

Huyu mtu biashara yake kufa ni Mumloge AFE ila sio mumloge mumuache hai,Mlogeni AFE ndio mtakua mmemuweza ila ukimloga akaumwa biashara ika drop Akipona akirudi uwanjani Hachukui round nyingi kufika alipokua, Kwanini unajua? Kwasababu hakutaka shortcut.

Mtaji wa biashara na ujasiriamali ni MUDA na wengi hili limewashindwa ndio mana anataka aanze biashara na mtaji wa mil.10 aanze biashara na mtaji wakupika kilo 6,aanze biashara na kununua bodaboda yake mwenyewe,aaanzie juuu Hamna anaetaka anzia huku sakafuni, na kama unajijua unafanya biashara hujui unachouza kinapatikana wapi Dear huna round wewe.

kuna mtu anauza majiko ya mkaa ila hajui majiko ya mkaa yanatengenezewa wapi,anachojua yeye majiko ya mkaa yakikarbia kuisha anapga simu analetewa,hadi alipo.

kuna mtu anauza mkaaa ila muulize mkaa una uza unautoa wapi,atakujibu easy tu "naletewaga na kaka mmoja yupo ruvu anamkaa mzuri bei nzuri kweli" muulize kawahi fika huko ruvu? ana uhakika na bei anayouziwa n nzuri kama anavyoipamba? watu ni wavivu watu wanapenda shortcut ndio mana wanafungua biashara mwaka tu zinakufa.

ila wapo ambao wataonekana wachawi,wameaga,wana bahati,nk kwasababu biashara zao hazifi,,biashara haina uchawi biashara inahtaji kufata utaratbu hatua kwa hatua usiruke hatua hata 1,ukijifanya unataka kukimbia tu ukaruka hatua tano mbele "siku 1 itaku cost" biashara hailazimishwi inajiendesha yenyewe taratbu mdogo mdogo.

Kuna watu wanataka nenepesha ng'ombe siku za minada,hatonenepa ila atavimbiwa,makundi ma 5 pale juu ni aina ya watu wapenda shortcut,akili yao inawaza pesa kuliko Biashara yenyewe.

Biashara si pesa tu,unapofanya biashara unahitaji faida mbili 1.wateja 2.pesa Faida namba 1 n wateja, sasa wewe unataka kuanza na mtaji wa mil.10 ili ukunje faida LAKI kwa siku, Hao wateja wakukupa laki per day unao? au unataka ukapge ramli?

Acheni shortcut,kubali kwamba biashara si pesa tu kuna siku watu wanarudi majumbani mwao hawana hata senti 5 faida yote kala mchana usiku na matumizi mengine,hajaweka akiba hata sent ila Ana amani ana furaha,kwanini unajua? hajapata pesa ya kuweka kwenye Kibubu ila kapata Faida ya Wateja,amepata wateja ambao siku 1 watakuja kumpa pesa mara mbili au tatu ya ambazo angezipata leo.

Badilika kama ulikua upo ktk kundi mojawapo pale juu, Biashara ina hela kweli (hata sio uongo) lakini ili uone pesa kimaukweliiiiii yakupasa ukubali kutoa sadaka muda wako na kila ulichonacho,nikisema muda siongelei masaa ua siku kadhaa naongelea ishu za miaka kadhaaa, Hakuna kirahisi wakuu anaewambia ni rahisi anawapotosha.

Asante kwa kusoma,naamini umepata kitu.
Asante.vipi sisi wazee wa kuahirisha mambo? Kesho unatakiwa kwenda kuanza mambo, unaingiza kasababu siku inaisha. Sisi unatuzungumziaje mkuu?
 
Back
Top Bottom